Uchaguzi 2020 Tuliosimamia Uchaguzi tukiri kuwa tumewatendea dhambi Watanzania kwa sababu ya kutii Mamlaka

Uchaguzi 2020 Tuliosimamia Uchaguzi tukiri kuwa tumewatendea dhambi Watanzania kwa sababu ya kutii Mamlaka

Abdul Mganyizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2019
Posts
1,042
Reaction score
2,005
Hatuna cha kueleza sisi tuliosimamia Uchaguzi tutabaki nafsi zikituuma lakini tulitii mamlaka zilizokuwa juu yetu.

Mkakati kuanzia juu mpaka chini kabisa kwenye ngazi ya mwisho mkakati ulitekelezwa na watendaji wakatimiza.

Narudia tena, ogopa mamlaka iliyoko juu yako. Tulifanya serikali za mitaa na tumemalizia uchaguzi mkuu.

Lazima kibaki chama kimoja kwa mujibu wa kauli za mamlaka, sasa wewe mtu mmoja unaanzaje kupinga?

Ili haya yote yaishe ni Katiba Mpya vingnevyo upinzani usahau kabisaaa uchaguzi huru.
 
Maafisa vipenyo walinikalia kooni nikakumbuka Nina watoto wadogo bado wanamuhitaji baba yao ikabidi nibadilishe tarakaimu ya chini iende juu ya juu iende chini.Moyo unauma Ila hamna namna na nimefanya toba kwa Hilo.
Pole sana mkuu
 
Hatuna cha kueleza sisi tuliosimamia uchaguzu tutabaki nafsi zikituuma lakini tulitii mamlaka zilizoka juu yetu.
Majuto ni mjukuu. Sasa mmeturudisha kwenye utawala wa Chama Kimoja. Sio peke yenu. Hata mawakala wa vyama vya upinzani wamechangia haya

Magufuli atasema ameshinda ila CCM na TANZANIA kwa ujumla tumepoteza
 
Maafisa vipenyo walinikalia kooni nikakumbuka Nina watoto wadogo bado wanamuhitaji baba yao ikabidi nibadilishe tarakaimu ya chini iende juu ya juu iende chini.Moyo unauma Ila hamna namna na nimefanya toba kwa Hilo.
Huu ujinga umefanyika maeneo mengi sana. Na policcm safari hii wamedhihirisha wazi namna wanavyotumiwa na bosi wao. Alichokisema yule OCD wa Hai, hakikuwa ni kitu cha kubahatisha.

Majibu yameonekana sehemu nyingi. Poleni wote mlio umizwa kwa kunyang'anywa ushindi wenu kibabe! Kisa kuna mtu mmoja tu alipiga marufuku wapinzani kutangazwa washindi.
 
Kwakweli mnalalamika mpaka roho inaniuma poleni sana wajameni ndio siasa hiyo jipangeni kwa uchaguzi ujao..

Congratulations in advance President Magufuli
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Vyama vya upinzani mawakala wote walifukuzwa.
Inawezekana kweli wengine walifukuzwa. Ila ukishakula pesa ya mtu, unaweza kutunga uongo wowote.

Wakala anayejielewa, aliyekula semina na akafundwa na Chama chake anafukuzwaje? Huu utaratibu wa kuokota mtu yeyote barabarani ‘akajitolee’ kusimamia nadhani iwe mwisho mwaka huu
 
Hatuna cha kueleza sisi tuliosimamia Uchaguzi tutabaki nafsi zikituuma lakini tulitii mamlaka zilizokuwa juu yetu.

Mkakati kuanzia juu mpaka chini kabisaa kwenye ngazi ya mwisho mkakati ulitekelezwa na watendaji wakatimiza....
Katiba iliyopo watu wameshindwa kuitumia.

Magufuli kapiga marufuku mikutano kinyume na katiba.

Hiyo mpya mkipewa halafu akaivunja hivyo hivyo, mtafanya kipi cha tofauti?

Mimi naona katiba mpya ni muhimu, ila mara nyingi inafanywa kuwa kisingizio tu.

Katiba haileti mabadiliko. Watu ndiyo huleta mabadiliko.

Sasa kama watu hawana muamko, katiba mpya itasaidiaje?
 
Back
Top Bottom