Uchaguzi 2020 Tuliosimamia Uchaguzi tukiri kuwa tumewatendea dhambi Watanzania kwa sababu ya kutii Mamlaka

Uchaguzi 2020 Tuliosimamia Uchaguzi tukiri kuwa tumewatendea dhambi Watanzania kwa sababu ya kutii Mamlaka

Kituo nilichopigia kura mawakala wa upinzani hawakuwepo walifukuzwa kabisa kisa hawakupewa barua ya utambulisho na mkurugenzi..
Shida inaanzia hapo sasa. Kwanini hawakupewa barua? Kwanini walisubiri mpaka siku ya Uchaguzi then wakaibukia pale bila barua? Yaani sehemu nyingi Upinzani ulijiandaa/uliandaliwa kupigwa mapema.

Mambo ni mengi sana ya kujifunza na kuchukua hatua. 2025 sio mbali sana.
 
Mkuu mawakala wameanza kufatilia barua mda mrefu mkurugenzi akawapa barua ccm, wao wakabaki hawana akasema hatoi mpaka asubuhi na asubuhi wanafatilia barua haziji wakafukuzwa, so nchi nzima mawakala wa upinzani walinyimwa huku ccm wakipewa kwa niliyo shuhudia kuwalaumu upinzani sio fair, tena mawakala wengine walipigwa wako ICU Sasa hvi
 
Amewanyima tu hao wapinzani ajira ya ubunge, udiwani na hata huo Urais! Ila upinzani hauwezi kufa kamwe. Hata ndani ya hicho chama chake, upinzani na makundi yatendelea tu kushamiri.

Yaani tumerudishwa enzi za Mwalimu! Hovyo kabisa.
Naamini hata hayo makundi atayathibiti vizuri tu.Anaonekana kajipanga barabara.Hakuna fyoko fyoko.Yetu macho.
 
Inawezekana kweli wengine walifukuzwa. Ila ukishakula pesa ya mtu, unaweza kutunga uongo wowote.

Wakala anayejielewa, aliyekula semina na akafundwa na Chama chake anafukuzwaje? Huu utaratibu wa kuokota mtu yeyote barabarani ‘akajitolee’ kusimamia nadhani iwe mwisho mwaka huu
Waliogoma kutoka walikamatwa na polisi ndani ya vituo

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Green guards walivalishwa mavazi ya polisi.
JKT walivalishwa mavazi ya polisi.
Na wale walioitwa jeshi la akiba walivalishwa mavazi ya polisi.

Kisha kazi ikaanza kuteka mawakala usiku, kuteka mawakala vituoni na kuingiza maboksi ya kura fake.

Wakati wa kuhesabu kura mawakala walitolewa zikaingizwa form walizojaza za matokeo.

Hata ukiyaangalia matokeo hayareflect uhalisia wenyewe.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Inawezekana kweli wengine walifukuzwa. Ila ukishakula pesa ya mtu, unaweza kutunga uongo wowote.

Wakala anayejielewa, aliyekula semina na akafundwa na Chama chake anafukuzwaje? Huu utaratibu wa kuokota mtu yeyote barabarani ‘akajitolee’ kusimamia nadhani iwe mwisho mwaka huu

Ooh my friend mambo hayakuwa rahisi hivyo
It was one against all jua tu na wakala wamezungushwa huku na kule ili mambo mengine yaendelee
 
Chadema Ianzishe Chuo Cha Mawakala.

Hongera CCM kwa elimu ya Siasa na Uchaguzi mnayotupatia Mara kwa Mara.
 
Katiba iliyopo watu wameshindwa kuitumia.

Magufuli kapiga marufuku mikutqno kinyume na katiba.

Hiyo mpya mkipewa halafu akaivunja hivyo hivyo, mtafanya kipi cha tofauti?

Mimi naona katiba mpya ni muhimu, ila mara nyingi inafanywa kuwa kisingizio tu.

Katiba haileti mabadiliko. Watu ndiyo huleta mabadiliko.

Sasa kama watu hawana muamko, katiba mpya utasaidiaje?
Imeshindikana kumwajibisha Kwasababu ya idadi ya wabunge, upande wake wako wengi sana,

kukiwa na uwiano sawa hata yeye anawajibishwa ,

kwasasa haitaweza kumuajibisha mkuu, ila wa chini mnalalao nao mbele vizuri tu
 
Hatuna cha kueleza sisi tuliosimamia Uchaguzi tutabaki nafsi zikituuma lakini tulitii mamlaka zilizokuwa juu yetu.

Mkakati kuanzia juu mpaka chini kabisaa kwenye ngazi ya mwisho mkakati ulitekelezwa na watendaji wakatimiza.

Narudia tena, ogopa mamlaka iliyoko juu yako. Tulifanya serikali za mitaa na tumemalizia uchaguzi mkuu.

Lazima kibaki chama kimoja kwa mujibu wa kauli za mamlaka, sasa wewe mtu mmoja unaanzaje kupinga?

Ili haya yote yaishe ni Katiba Mpya vingnevyo upinzani usahau kabisaaa uchaguzi huru.
Mlifanyaje?
 
Maafisa vipenyo walinikalia kooni nikakumbuka Nina watoto wadogo bado wanamuhitaji baba yao ikabidi nibadilishe tarakaimu ya chini iende juu ya juu iende chini. Moyo unauma Ila hamna namna na nimefanya toba kwa Hilo.
Umefanya toba kwa nani ?
 
Back
Top Bottom