Unauliza maswali mepesi ambayo hayapaswi kutoka kwako
Hao watu ukiwaondoa kwenye mkono wa rais, utaweka utaratibu wa kuwapata na kuwapatia protection hasa security ya kazi zao baada ya uchaguzi , na hawatofanya kazi chini ya shinikizo la chombo chochote kilicho juu yao
manake wote wakati wanaapishwa waliambiwa "nakulipa mshahara, nakupa gari , nimekupa nyumba , nimekupa kazi alafu ukanitangazie mpinzani ameshinda" kwenye mazingira haya huyo mkurugenzi anatangaza vipi mpinzani wakati kibarua chake kiko hatarini
hao wanaohama ni issue nyingine ikiwa ni pamoja na ubovu wa katiba hii, hayo mazingira ya wao kutotangazwa hata wakishinda walisha yaona, mtu haoni namna ya kupenya akiwa huku ilihali kila kitu kina favor upande ule, wengine ni njaa ziliwapeleka kule etc etc
Usinipangie maswali ya kuuliza. Unaweza kuona swali jepesi kwa sababu hujaelewa kina cha swali.
Unatoa majibu mepesi kwa maswali magumu.
Tuna tatizo la utamaduni, utamaduni wa woga.
Tatizo hili halimalizwi na mabadiliko ya katiba. Kwa sababu hata provisions za katiba ya sasa hatuzitumii.
Nchi nzima imeambiwa na Magufuli hakuna kukutana katika mikutano ya siasa. Hiyo amri ni kinyume na katiba.
Hakuna aliyeipinga.
Hatukuhitaji katiba mpya kupinga hilo.
Na hatukupinga.
Sasa kama rais anavunja katiba iliyopo, na hakuna anayempinga, akiwapa hiyo mpya mnayoitaka na akaivunja tena mtakuwa na kipi kipya cha kuweza kuushinda woga wenu wa sasa?
Utasema asimteue huyu na yule, lakini bado atakuwa rais tu. Na kwa njia moja au nyingine bado atakuwa na nguvu.
Sasa kama mnabadili katiba tu, na Watanzania wanabaki kama walivyo wafuasi wa falsafa za hewala hewala, kamanda wq Polisi akiwaambia hakuna kuandamana (hakinyqo ya kikatiba), mkiqndamana mtapigwa kama mbwa koko. Wanafyata mkia. Katiba mpya itakusaidiaje kubadili mambo wakati watu hawajabadilika?
Serikali ya CCM ya sasa haina haya, haishindwi kupiga watu, kufunga, kuua, na mkapeleka kesi mahakamani, wakawafanyia visa huko huko mahakamani. Whether mahakimu na majaji wanateuliwa na rais ama sivyo.
Sasa ukibadili katiba bila kubadili uthubutu wa watu utawezaje kubadili mfumo?
Watu ndio wanaweka katiba ili kuleta mabadiliko.
Katiba haileti mabadiliko.