Uchaguzi 2020 Tuliosimamia Uchaguzi tukiri kuwa tumewatendea dhambi Watanzania kwa sababu ya kutii Mamlaka

Uchaguzi 2020 Tuliosimamia Uchaguzi tukiri kuwa tumewatendea dhambi Watanzania kwa sababu ya kutii Mamlaka

Mi siamini kwenye hilo. Kuna mengi mazuri yanakuja. Tutarajie kuona mafanikio mengi. Nchi hii ni yetu sote. Kama wapinzani ndio walikuwa wanakwamisha maendeleo naamini sasa ndio mda wa kuangalia visingizio vya wakati uliopita kama vitakuwa vilevile wakati ujao. Tuendelee kuwa wavumilivu kaka. Mda utatuambia
Tanzania iliwahi kuwa chini ya chama kimoja kwa muda mrefu, ni maendeleo gani tulipata? Na la pili tujiulize ni hoja au mpango gani wa serikali ulishindwa kupitishwa bungeni kutokana na kukataliwa na upinzani?
 
Tanzania tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kama Chama kimoja wakati wa Nyerere kuwakomboa wenzetu waliokuwa wakikandamizwa na ukoloni kusini mwa bara la Afrika.
Tukapiga hatua kuondoa ujinga kwa kiasi kikubwa.
Na hata sasa maendeleo yanaendelea kuonekana.
Bado tunaendelea kupambana na mabeberu
 
Siasa ni ushawishi, shawishini wapiga kura wawachague, kampeni mmepiga siku 60, kila siku mnaishia kutaja magufuri, Mara risasi, yaani mlishindwa hata kunadi ilani yenu afu mlitegemea tuwachague?
 
Kuna swali moja la msingi kabisa hujalijibu.

Ikiwa Magufuli anavunja katiba ya sasa, mathalani, anakataza mikutano ya kisiasa kinyume cha katiba, na hakuna aliyempinga na kuzuia hilo.

Mkipewa katiba mpya yenye vipengele vyote mnavyovitaka, akaivunja, mtakuwa na uwezo gani wa kumpinga?

Kumpinga Magufuli hakuhitaji katiba mpya, kwa sababu kuna vipengele vya katiba ya sasa anavivunja na watu hawampingi.

Tuna udhaifu katika watu, kabla hatujafika kwenye katiba.

Katiba mpya ni kama gari, gari zuri sana, tuseme Ferrari.

Sasa hivi tuna kigari kibovu, ki Volkswagen Beetle cha zamani.

Unachosema wewe ni kwamba, tupate gari zuri, Ferrari, litatuwezesha kwenda kasi.

Mimi nakuambia hivi, kuwa na gari zuri kama Ferrari ni muhimu, litatusaidia kwenda kasi.

Lakini, mbona dereva wetu hajui kuendesha gari, hata hili Volkswagen Beetle hawezi kuliendesha?

Kama kashindwa kuliendesha hili Volkswagen Beetle, hilo Ferrari atawezaje kuendesha?

Kama tatizo letu ni dereva asiyejua kuendesha gari, hata tukipewa Ferrari, bado atakuwa hawezi kuendesha tu.

Katiba mpya ni muhimu.Lakini, katiba mpya haileti mabadiliko, watu ndio wanaoleta mabadiliko.
Mie nijaribu kukueleza jinsi mamlaka yake ilivyo kubwa kwa sasa kama hizi organ za mihimili mitatu zitakuwa parallel ni raisi kumshitaki kwenye mahakama au bunge likes uadabisha,sio kama ulivyo sasa ukienda mahakani majudge ni wateule wake ukienda bungeni majority ya wabunge yeye ni mwenyekiti wao kwenye chama Kwenye katiba mpya imeweka hizi organ parallel majudge wana mfumo wao wa kupatikana ikiwemo kiongozi wao judge mkuuu nawabunge wachaguliwa na wananchi chini ya udhamini wa chama hivyo rais hawezi kuwa mwenyekiti wa chama yaani ni mkuu wa organ inayo wadhamini wabunge wabunge hapo lazima wawe vibogoyo
 
Hatuna cha kueleza sisi tuliosimamia Uchaguzi tutabaki nafsi zikituuma lakini tulitii mamlaka zilizokuwa juu yetu.

Mkakati kuanzia juu mpaka chini kabisa kwenye ngazi ya mwisho mkakati ulitekelezwa na watendaji wakatimiza.

Narudia tena, ogopa mamlaka iliyoko juu yako. Tulifanya serikali za mitaa na tumemalizia uchaguzi mkuu.

Lazima kibaki chama kimoja kwa mujibu wa kauli za mamlaka, sasa wewe mtu mmoja unaanzaje kupinga?

Ili haya yote yaishe ni Katiba Mpya vingnevyo upinzani usahau kabisaaa uchaguzi huru.
Usilie, mlifanya kazi nzuri ya kusimamia uchaguzi usiokuwa na dosari, hongereni sana.
 
Tanzania tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kama Chama kimoja wakati wa Nyerere kuwakomboa wenzetu waliokuwa wakikandamizwa na ukoloni kusini mwa bara la Afrika.
Tukapiga hatua kuondoa ujinga kwa kiasi kikubwa.
Na hata sasa maendeleo yanaendelea kuonekana.
Bado tunaendelea kupambana na mabeberu
Sara ya ukombozi wa Africa haikutusaidia jambo lolote, pesa zilizotumika kwenye vita hivyo pengine zingeweza kufanya uwezekaji wa maana. Viwanda vilivyojengwa na Nyerere viliuliwa na CCM yenyewe. Mabeberu yaliyo ndani ya CCM ni hatari kuliko hao wa nje tunaowasingizia.
 
Kwenye kipengele cha kuhusu demokrasia, niko sahihi bwashee. Mwalimu hakuwahi kuwa mtu wa kupenda demokrasia. Hata yeye mwenyewe huko aliko anatambua vizuri, kuna baadhi ya mambo alivurunda wakati wa Uongozi wake na mengine mengi tu aliyapatia.

Na ndiyo maana alifuta mfumo wa vyama vingi mwaka 1965, aliwashughulikia mpaka marafiki zake wa karibu mfano Oscar Kambona, Bibi Titi Mohamed, nk. Kwa sababu tu walitofautiana kwenye baadhi ya mambo. Ni kipindi hicho cha Mwalimu, msemo wa " Zidumu Fikra za Mwenyekiti" ulitamalaki.
Ni haya hapa uliyokongooka nayo.

Kwanza ni "enzi na nyakati" tofauti kabisa, mkuu 'Tate'.

Wakati ule ni wapi Afica ambako hapakuwa na chama kimoja> Nitajie kiongozi mmoja tu aliyefuata "demokrasia."
' Berlin wall' ilikuwa haija-'fall' mkuu wangu, na neno "Utandawazi" hakuna aliyejua kuwa lipo katika msamiati wa Kiswahili, na mambo mengi mengine yaliyofanya hali hiyo ya chama kimoja ndio uwe mfumo wa wakati huo, hapa kwetu na hata sehemu nyingi duniani.

Tulikuwa bado tunapigania uhuru wa wenzetu huko kusini mwa Afrika, n.k.

Unapolinganisha utawala huu na ule wa Mwalimu kwa jambo lolote lile ni lazima uwe mwangalifu sana. Hawa watu wawili ni mbalimbali kabisa kwa kila kitu. Mwalimu alieleza na kushawishi, huyu hawezi kueleza ila anajua tu kutumia mabavu. Mwalimu hakufanya kwa ubinafsi, kutafuta sifa au kujiona yeye ndie kila kitu; alifanya na kueleza kwa nini imefanyika hivyo na kwa maslahi ya nani.

Kama wewe huzioni tofauti hizi, basi utakuwa na sababu nyingine, na sio hizo unazozitumia hapa.

Umewataja Oscar na Bibi Titi - hivi kweli hujui sababu zilizofanya kukawa na tofauti kati yao na msimamo uliokuwa umechukuliwa na chama, hasa kwa Oscar? Hata kumtaja Bibi Titi kuwa kaonewa ni kujitoa ufahamu mkuu wangu 'Tate.'

Haya labda nikuache na mfano ambao wengi huutumia hapa Afrika Mashariki kuwa sehemu ya eneo walikodhani kuna (demokrasia na maendeleo?); Kenya ya Kenyatta, au wewe utatumia mfano gani katika enzi hizo? Sasa kawaulize akina Odinga yaliyowapata baba zao, akina JM Kariuki, akina Opio na wengi wengine walioonja utamu wa demokrasia unayoiongelea kwa wakati huo.

Busara, Hekima, Intellectual acumen, na sifa nyingi alizokuwa nazo Mwalimu huwezi kamwe ukamrundika kwenye kundi hili la ma-'gangsters.'
 
Siasa ni ushawishi, shawishini wapiga kura wawachague, kampeni mmepiga siku 60, kila siku mnaishia kutaja magufuri, Mara risasi, yaani mlishindwa hata kunadi ilani yenu afu mlitegemea tuwachague?
Mimi sina chama, kwa hiyo ukiniambia tushawishi sijui unaimanisha nini. Pia pamoja na kwamba niliamini JPM atashinda siyo kwa gape la kura hizo. Ushahidi wa wizi wa kura upo maeneo kadhaa na hili linatia shaka. Ila pia nchi yenye wapiga zaidi ya million 30 afu wapiga kura hawafiki million 15 ni shida nyingine na jiulize sababu ni nini.
 
Ni haya hapa uliyokongooka nayo.

Kwanza ni "enzi na nyakati" tofauti kabisa, mkuu 'Tate'.

Wakati ule ni wapi Afica ambako hapakuwa na chama kimoja> Nitajie kiongozi mmoja tu aliyefuata "demokrasia."
' Berlin wall' ilikuwa haija-'fall' mkuu wangu, na neno "Utandawazi" hakuna aliyejua kuwa lipo katika msamiati wa Kiswahili, na mambo mengi mengine yaliyofanya hali hiyo ya chama kimoja ndio uwe mfumo wa wakati huo, hapa kwetu na hata sehemu nyingi duniani.

Tulikuwa bado tunapigania uhuru wa wenzetu huko kusini mwa Afrika, n.k.

Unapolinganisha utawala huu na ule wa Mwalimu kwa jambo lolote lile ni lazima uwe mwangalifu sana. Hawa watu wawili ni mbalimbali kabisa kwa kila kitu. Mwalimu alieleza na kushawishi, huyu hawezi kueleza ila anajua tu kutumia mabavu. Mwalimu hakufanya kwa ubinafsi, kutafuta sifa au kujiona yeye ndie kila kitu; alifanya na kueleza kwa nini imefanyika hivyo na kwa maslahi ya nani.

Kama wewe huzioni tofauti hizi, basi utakuwa na sababu nyingine, na sio hizo unazozitumia hapa.

Umewataja Oscar na Bibi Titi - hivi kweli hujui sababu zilizofanya kukawa na tofauti kati yao na msimamo uliokuwa umechukuliwa na chama, hasa kwa Oscar? Hata kumtaja Bibi Titi kuwa kaonewa ni kujitoa ufahamu mkuu wangu 'Tate.'

Haya labda nikuache na mfano ambao wengi huutumia hapa Afrika Mashariki kuwa sehemu ya eneo walikodhani kuna (demokrasia na maendeleo?); Kenya ya Kenyatta, au wewe utatumia mfano gani katika enzi hizo? Sasa kawaulize akina Odinga yaliyowapata baba zao, akina JM Kariuki, akina Opio na wengi wengine walioonja utamu wa demokrasia unayoiongelea kwa wakati huo.

Busara, Hekima, Intellectual acumen, na sifa nyingi alizokuwa nazo Mwalimu huwezi kamwe ukamrundika kwenye kundi hili la ma-gangestors.'
Ila huyu jamaa kweli ni janga. Tuombee tu asijegeuze kuwa Museveni itakapofika 2025!
 
Alichokifanya Magufuli ni kuua huo Muamko wa kisiasa katika uongozi wake, hii ni pamoja na kukataza mikutano, kufunga wapinzani na kuwafungulia makesi, kuteka na kuua watu, assassination attempt ya Lissu n.k

Kipindi cha JK, muamko ulikuwa mkubwa sana, wapinzani walikuwa wanafanya mikutano mingi ya kisiasa. Ni enzi za JK mbunge anaweza kufariki, uchaguzi ukapigwa na mpinzani akashinda mfn. Nassari, Jimbo la Chacha wangwe, n.k

Sasa Magufuli kajengea watu uoga, yani now days ukiwa nyumbani mkianza kumjadili magufuli lazima mfunge madirisha kwanza.

Lkn pia, naona Upinzani unapaswa kujipanga upya. Kwasasa Mbowe hapaswi kuwa mwenyekiti, ni muoga sana, hana ujasiri wa Lissu au hata Lemma.

Upinzani unapaswa kuwa na kiongozi ambaye ni jasiri, asie muoga ili kuwajengea wananchi ujasiri vilevile.

Muamko wa kisiasa kwa wananchi hujengwa na wanasiasa walio jasiri, wakiwa waoga na wananchi huogopa

Mwisho, upinzani umeshindwa kutengeneza Dar.
Dar ndio kitovu cha siasa, na Nchi ipo hapa.
Upinzani ulipaswa kusimamisha Wagombane wababe na wenye ujasiri.
Imagine Dar ingekuwa na Wabunge kama Lemma, Sugu, Heche, Zitto ingekuwaje?
Sasa wabunge hao wapo mikoani, ambako huko wanategemea Kusikia Dar inasema nn.

Sasa jiji zima unasimamisha wagombea wamepooza, wasio na hamsha hamsha. Mdee kidogo ndo anajikongoja ila hana supports.
Mkuu 'General', umeyasema mengi, baadhi yake nikikubaliana nayo.

Lakini niseme tu kwamba,'It is more complicated than that'!

Tundu Lissu ni jasiri, ndio, lakini watu hata kule kuvaa T-shirts' tu za kumwombea apone, watu waliogopa.

Leo hii, akifanya jambo la kijasiri na kuwekwa ndani, utamwona nani akisimama nyuma au mbele yake kutetea ujasiri huo?

Mbowe, umemtaja kama mfano hapo; lakini hata hukumbuki yaliyompata hapo Kinondoni kwenye mkutano wa uchaguzi mdogo? Hivi unajua kilichotokea hapo? Unataka ujasiri wa namna gani?

Labda niseme tu kwamba waTanzania hawajampata kiongozi anayeamsha mori na ari zao kiasi cha kutaka kufa au kupona.

Siwezi kamwe kuwalaumu waTanzania na kuwaita 'wajinga' au 'waoga', ni swala tu la apatikane kiongozi wanayemwamini na kusimama naye katika aina yoyote ile ya vitisho na misukosuko.
Mtu huyu, kwa bahati mbaya bado hatujampata, ingawaje najua wapo kadhaa ndani ya nchi yetu hii.
 
Hatuna cha kueleza sisi tuliosimamia Uchaguzi tutabaki nafsi zikituuma lakini tulitii mamlaka zilizokuwa juu yetu.

Mkakati kuanzia juu mpaka chini kabisa kwenye ngazi ya mwisho mkakati ulitekelezwa na watendaji wakatimiza.

Narudia tena, ogopa mamlaka iliyoko juu yako. Tulifanya serikali za mitaa na tumemalizia uchaguzi mkuu.

Lazima kibaki chama kimoja kwa mujibu wa kauli za mamlaka, sasa wewe mtu mmoja unaanzaje kupinga?

Ili haya yote yaishe ni Katiba Mpya vingnevyo upinzani usahau kabisaaa uchaguzi huru.
Katiba Mpya nayo itabaki njozi tu sababu wasioitaka ndio hao wamejitawadha na kujaa bungeni!! Hakuna hata wa kuianzisha hoja hiyo!
 
Katiba Mpya nayo itabaki njozi tu sababu wasioitaka ndio hao wamejitawadha na kujaa bungeni!! Hakuna hata wa kuianzisha hoja hiyo!
Kwa sasa Bunge zima litakua ni la Ndiyoooooo!!!!!!! Kila kitu ni Ndiyooooo!!! Vigeregere na vifijo vitatawala! Wabunge watatumia muda wao mwingi kumsifia Rais na serikali yao! Maslahi ya chama yatapewa kipaumbele zaidi kuliko maslahi ya Taifa, nk.
 
Hatuna cha kueleza sisi tuliosimamia Uchaguzi tutabaki nafsi zikituuma lakini tulitii mamlaka zilizokuwa juu yetu.

Mkakati kuanzia juu mpaka chini kabisa kwenye ngazi ya mwisho mkakati ulitekelezwa na watendaji wakatimiza.

Narudia tena, ogopa mamlaka iliyoko juu yako. Tulifanya serikali za mitaa na tumemalizia uchaguzi mkuu.

Lazima kibaki chama kimoja kwa mujibu wa kauli za mamlaka, sasa wewe mtu mmoja unaanzaje kupinga?

Ili haya yote yaishe ni Katiba Mpya vingnevyo upinzani usahau kabisaaa uchaguzi huru.
Naungana na wewe Mkuu! Nafsi yangu inaniuma Sana. Lakini sikuwa na namna,mamlaka iliyo juu ina nguvu sana. Nimeshindwa kukataa,mmoja alijidai mjuaji Sasa hivi yupo kikaangoni,maisha yake yanaenda kuwa ya hovyo hovyo tu,yupo chini ya uangalifu maalumu.
 
Mimi kwa kweli sielewi! Ina maana kura alizopata Lissu kwa hesabu ya Mawakala hata wale wachache walioingia vituoni ziko zaidi ya zile zilizotolewa taarifa na tume?
 
Ndiyo maana hata Wana CCM wenyewe wameshindwa kushangilia na kufurahia huu wanaoita ushindi, sababu roho zao zimejaa huzuni kwa dhuruma iliyofanyika
 
Sio kweli...usiwadharau Watanzania kiasi hicho.

Tanzania ipo kabla ya Mange na Kigogo kuwepo pia itaendelea kuwepo baada yao hivyo hao wawili hawawezi kuwa tegemeo kwa mamilioni ya Watanzania.
Sasa mbona tunashikwa matak.o wote alafu tegemeo letu ni Twitter kwa kina Mange na Kigogo
 
Back
Top Bottom