Alichokifanya Magufuli ni kuua huo Muamko wa kisiasa katika uongozi wake, hii ni pamoja na kukataza mikutano, kufunga wapinzani na kuwafungulia makesi, kuteka na kuua watu, assassination attempt ya Lissu n.k
Kipindi cha JK, muamko ulikuwa mkubwa sana, wapinzani walikuwa wanafanya mikutano mingi ya kisiasa. Ni enzi za JK mbunge anaweza kufariki, uchaguzi ukapigwa na mpinzani akashinda mfn. Nassari, Jimbo la Chacha wangwe, n.k
Sasa Magufuli kajengea watu uoga, yani now days ukiwa nyumbani mkianza kumjadili magufuli lazima mfunge madirisha kwanza.
Lkn pia, naona Upinzani unapaswa kujipanga upya. Kwasasa Mbowe hapaswi kuwa mwenyekiti, ni muoga sana, hana ujasiri wa Lissu au hata Lemma.
Upinzani unapaswa kuwa na kiongozi ambaye ni jasiri, asie muoga ili kuwajengea wananchi ujasiri vilevile.
Muamko wa kisiasa kwa wananchi hujengwa na wanasiasa walio jasiri, wakiwa waoga na wananchi huogopa
Mwisho, upinzani umeshindwa kutengeneza Dar.
Dar ndio kitovu cha siasa, na Nchi ipo hapa.
Upinzani ulipaswa kusimamisha Wagombane wababe na wenye ujasiri.
Imagine Dar ingekuwa na Wabunge kama Lemma, Sugu, Heche, Zitto ingekuwaje?
Sasa wabunge hao wapo mikoani, ambako huko wanategemea Kusikia Dar inasema nn.
Sasa jiji zima unasimamisha wagombea wamepooza, wasio na hamsha hamsha. Mdee kidogo ndo anajikongoja ila hana supports.