Umeisoma katiba mpya? Kuna mambo mke yanampunguzia madaraka rais hivyo ni rais kumu impeach rais, hata wakitenganisha kofia itasaidia maana hakuna sehemu rais anakutana na wabunge kama boss wao, judiciary lazima iwe parallel na mihimili mingine tutafute utaratibu wa kumfuata judge mkuu na ma judge na vyombo vya kumuimpeach view ndani ya judiciary
Kuna swali moja la msingi kabisa hujalijibu.
Ikiwa Magufuli anavunja katiba ya sasa, mathalani, anakataza mikutano ya kisiasa kinyume cha katiba, na hakuna aliyempinga na kuzuia hilo.
Mkipewa katiba mpya yenye vipengele vyote mnavyovitaka, akaivunja, mtakuwa na uwezo gani wa kumpinga?
Kumpinga Magufuli hakuhitaji katiba mpya, kwa sababu kuna vipengele vya katiba ya sasa anavivunja na watu hawampingi.
Tuna udhaifu katika watu, kabla hatujafika kwenye katiba.
Katiba mpya ni kama gari, gari zuri sana, tuseme Ferrari.
Sasa hivi tuna kigari kibovu, ki Volkswagen Beetle cha zamani.
Unachosema wewe ni kwamba, tupate gari zuri, Ferrari, litatuwezesha kwenda kasi.
Mimi nakuambia hivi, kuwa na gari zuri kama Ferrari ni muhimu, litatusaidia kwenda kasi.
Lakini, mbona dereva wetu hajui kuendesha gari, hata hili Volkswagen Beetle hawezi kuliendesha?
Kama kashindwa kuliendesha hili Volkswagen Beetle, hilo Ferrari atawezaje kuendesha?
Kama tatizo letu ni dereva asiyejua kuendesha gari, hata tukipewa Ferrari, bado atakuwa hawezi kuendesha tu.
Katiba mpya ni muhimu.Lakini, katiba mpya haileti mabadiliko, watu ndio wanaoleta mabadiliko.