Tuliosoma nao wakishakuwa Madaktari wa Falsafa(PhD) wanajikuta sana. Hivi inawasaidia nini?

Tuliosoma nao wakishakuwa Madaktari wa Falsafa(PhD) wanajikuta sana. Hivi inawasaidia nini?

Aliyekuzidi kakuzidi Mtu mwenye Elimu huwezi mpata PhD sio mchezo Mkuu

Pesa huwezi mtambia mtu maana kila Mtu anazo tumezidiana viwango usicheze na Elimu
 
Mmoja wao ni Mwigulu elimu yangu ya uchumi ni Kali kumzidi, hawa wengine tunaokutana nao kwenye maeneo yetu, vina mshahara Milioni 4 hadi 5 vinavimba sasa huo mshahara au pesa ya kulimia tu na vibarua wangu.

Kuna mmoja nilishamuuliza na maringo yako ya hiko PhD unaweza kunywa Hennessy kila siku na mchepuko kila siku akabaki lofa tu, PhD ni ofisini kwako sio kitaa
Si kwa ubaya ila inaonekana wewe ndio mwenye shida.
 
Nina marafiki wengi wana PhD na wengine ma proffesor sihawahi kuona wanaringa . Tena wako humble sana sana. Sijui hao wanao ringa umekutana nao wapi?

Lakini inaonekana mtoa mada una infiriority complex. Yaani jamaa wanafanya yao kawaida wewe akili yako ndo inakuambia kuwa wanaringa au wanajidai.
 
Back
Top Bottom