Tuliotembea mikoa mingi tujuane

Tuliotembea mikoa mingi tujuane

Mtu amepita Pwani na Moro akielekea Dar anasema amefika Pwani.
Kaa hata siku kumi Pwani ndio useme umefika Pwani. Pwani Ni Kati ya mikoa inayoongoza kwa Imani za kishirikina Tanzania.
Pwani ukiona nyumba nzuri, gorofa, gari zuri ujue sio la mwenyeji wa Pwani. Majungu Sasa, chuma ulete, umalaya, masengenyo.
Pwani upende kuisikia tu.
 
Mikoa niliyofika na kuishi kwa zaidi ya mwaka mmoja

Dodoma
Dar Es Salaam
Mwanza
Simiyu
Mbeya
Rukwa.

Mikoa ambayo sijawahi hata kukanyaga
Arusha, Kilimanjaro, Mara, Manyara, Kagera, Kigoma, Lindi, Mtwara, Ruvuma.

kuna siku natamani nifanye road trip nianzie Katavi natokea Kigoma nakuja Tabora naingia Singida then naenda Manyara, naunga mpaka Arusha then Kilimanjaro- Tanga mpaka njia panda ya Ulaya Dar. (LIFE)
 
Nashukuru Mungu nimetembea mikoa yote ya nchi hii na asilimia kubwa ya makao makuu ya wilaya zake, zanzibar nimeishia unguja, pemba ndio bado, nilijifunza mambo mengi lakini wilaya zifuatazo vijijini kwao wamejenga majumba ya maana , mbinga, karagwe, muleba, moshi, mikoa kama kigoma, nwanza, singida, lindi, mtwara, singida, tabora, morogoro, bado pervijijini hakuna majengo ya kueleweka
Kama mimi tu sijatembea wilaya kadhaa tu, nyingi ni hizi mpya, ila Tanzania yote kiujumla nimetembea.
Lushoto nitapapenda daima..
 
Dar es salaam
Arusha
Kilimanjaro
Tanga
Manyara
Morogoro
Dodoma
Singida
Tabora
Geita

Nimeipangilia mikoa kutokana na safari yangu ya masomo ilipoanzia mpk namaliza

Nb:Ni mkaazi wa Zanzibar
 
lakini wilaya zifuatazo vijijini kwao wamejenga majumba ya maana moshi,

Moshi umekua Too general, ulifika Moshi Vijijini, Moshi mjini au wapi?? Pia watu wanashindwa-ga kutofautisha kati ya Moshi Manispaa, Moshi Vijijini, na wilaya ya Rombo wao kote wakiita Moshi.
 
Kupita kama njia nimepita mikoa mingi sana, sehemu sijapita Kama njia ni Katavi, Kigoma,Mara,Kagera.

Maeneo niliyofika bila kujali ni Mkoa ama wilaya gani
Mbeya jiji na vijijini na viunga vyake
Kyela
Tukuyu
Mwakaleli
Ileje
Tunduma
Chunya
Iringa mjini
Babati mjini
Mbulu na viunga vyake
Arusha mjini na viunga vyake
Hai (bomang'ombe)
Siha (West Kilimanjaro) mpaka Kamwanga-Rongai
Rombo
Mwika
Marangu
Holili
Himo
Moshi mjini na viunga vyake
Moshi vijijini
Mwanga mjini
Same ya milimani huko Vunta mpaka Njagu juu.
Bagamoyo (hapa nishakaa Bagamoyo Police post masaa karibia matano [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]) sehemu za Kihistoria zote za Bagamoyo, eneo la Kiromo nimekaa zaidi ya wiki 3.
Morogoro mjini na viunga vyake
Morogoro vijijini nimekaa zaidi ya miezi 04 maeneo ya Mkuyuni kwa Babu Tale, Matombo mpaka Tawa
Mwanza mjini Igoma by Night, Kisesa, Magu mpaka kwa Gen. Mabeyo
Nyegezi
Malimbe
Busega
Singida vijijini mwendo wa Punda na kula kuku kwa sana.
Singida mjini
Dodoma kisasa
Dar maeneo machache sana. Hapa huwa nakaa siku 1 au 2 na nikizidi sana ni wiki moja. Huwa sielewi watu wa Dar wanaishije!
 
Back
Top Bottom