Tuliotembea umbali mrefu kwa miguu kwa sababu yoyote ile tukutane hapa

Jua la dar unalijua vizuri mkuu?

labda upige hizo ruti usiku ila dar hii

Jua litakukwmisha na ukijikaza hata siku 1

kesho utaamka umekua mweusi kama tairi la boxa
Na kwa Dar hali ya Hewa ndio tatizo kubwa.Isingekuwa joto watu wangetembea sana kwa mguu.Unakuta mtu anatoka Mapipa anaenda Fire au Muhimbili au Kariakoo anapanda gari ile sehemu ni ya kucharaza tu mguu
 
Wakati nipo Mdogo tuliwahi Kaa Kijiji kimoja cha Ikondo (Kipo Lupembe) Mkoani Njombe.Sasa Kuna watu toka vijiji vya Ukalawa Kanikelele Lupembe walikuwa wanaenda Mgololo kununua Mapipa ambayo walikuwa wanaenda kutumia kupika Pombe za Kienyeji,ule umbali sijui ni km ngapi lkn angalau ni parefu jamaa walikuwa wanachoka sio mchezo
 
Bila kusahau kwenda mashamba ya kilimo yaliyopo mpakani na kenya hasa kwa wachaga, umbali makadirio km 50 na zaidi kwa baadhi yao.
 
Hivi jamani hili neno ni root much au ni route xxxx... yaani hakuna hata wa kunirekebisha! Kiranga uko wapi? Halafu kuna siku niliwahi kuandika packed badala ya parked na sijamsikia mtu akinirekebisha
 
Vyombo vya usafili vingi hv hafu ntembee mguu huwa nawapiga fix nyingi sana za kisomi kisomi nahakikisha konda na dereva wote wapo mkononi sijawahi kutembea umbali mrefu labda nafanya mazoezi ,ila kama sina nauli hata kama ni km 200 ntapanda gali tu mbele mbelee tutaelewana.
 
Kimara hadi ubungo. Kulikuwa na foleni kutokea mbezi hadi ubungo siku hiyo usiku wa saa mbili. Nauli haitoshi kupanda pikipiki, na siku hiyo walikuwa wanatwanga watu bei kubwa sana.. Ikabidi nikanyage. Ilikuwa 2012 au 2011.
 
Shikamoo
 
Zaidi ya 120km, nilitoka wilaya ya Rungwe (saivi Busokelo) eneo linaitwa Rwangwa mpaka Mbeya mjini..bahati mbaya sijui cha shortcut wala nini kwahyo nanyoka tu na barabara. Nilitoka kule saa kumi na moja alfajiri mpaka saa mbili usiku ndo naingia Mbeya mjini, form three kipindi hicho. Nilitoroka home nikaenda kule wakawa hawanitaki kwahyo kunisema kila Siku, nikashundwa kuvumilia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…