Tuliotembea umbali mrefu kwa miguu kwa sababu yoyote ile tukutane hapa

Wewe umewahi kutembea umbali gani kwa wakati mmoja?

Karibia wote humu tumewahi kuwa watoto wa kijijini!
Shule ya msingi niliyosoma ilikuwa 3km kutoka home,hapo Kuna watu wanakaaa mbali zaidi ya hapo lakini daily school wanaenda na kurudi.
 
Wewe umewahi kutembea umbali gani kwa wakati mmoja?

Karibia wote humu tumewahi kuwa watoto wa kijijini!
Wakati nipo primary nilikuwa natembea 6 Km daily.3Kwenda tatu kurudi.
Msimu wa kulima maharage mashamba yetu yalikuwa umbali mrefu tu lkn kwenda shamba masaaa matatu mpaka 4 kurudi masaa matatu mpaka 4.Mnatoka Nyumbani saa kumi na moja mnafika shamba saa mbili.Hapo mnachapa Mguu hasa.
Nimeenda Sekondary nilikuwa Nina kawaida ya kumwambia mzee atume nauli ili nipande basi tulikuwa tunabana hela.Tunakatiza shortcut ya pori natoka school saa kumi na mbili nafika home saa nane tisa au kumi.Huo umbali sio mdogo.Sijui ni km ngapi lakini ni nyingi
 
Samsung yangu inasema nimetembea step 346,890 sijui ni sawa na umbali gani!?
 
Nakumbuka nilikuwa kidato Cha nne wakati huo tulikuwa tunafanya mock..siku hiyo tulikuwa na mtihani tukatoka jioni..kulikuwa na mvua kubwa magari shida mjini dar..nilitembea kutoka fire to mbagala..niliumwa miguu siku mbili..
 
Mjini connection.
 
Hivi jamani hili neno ni root much au ni route xxxx... yaani hakuna hata wa kunirekebisha! Kiranga uko wapi? Halafu kuna siku niliwahi kuandika packed badala ya parked na sijamsikia mtu akinirekebisha
Warekebishaji wanadai mshahara wa Sekretari siku hizi.

Wamechoka kutoa huduma ya bure.
 
Kigarama mpaka Bukoba mjini
Bukoba mjini mpaka Kamachumu
Km 120 - kuanzia saa 11 alfajiri mpaka saa tatu usiku.. mfukoni nikiwa na sh 40.. 1988
 
Mkuu acha masikhara asee...

Lwangwa - mbambo- Tukuyu- kiwira- ndaga- uyole...

Ulitisha saana[emoji119]
 
Nilitembea kwa mguu kutoka dar mpaka zenji nilipofika zenji nikaambiwa mwenyeji wangu hayupo kwa wiki nzima ikabidi nirudi tena dar siku hiyohiyo
 
Kutembea kilometa 100 kwa siku moja ni ngumu sana. Fikiria mkimbiaji wa marathon anakimbia kilometa 42 Kwa masaa mawili.

Sasa huyo mkimbiaji km 100 anaweza kukimbia kwa saa sita.

Sasa ndo mtu wa kawaida atembee km 100 kwa siku moja??
 
Naliwahi tembea kutoka picha ya ndege Hadi pingu (karibu na chalinze)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…