Tuliotembea umbali mrefu kwa miguu kwa sababu yoyote ile tukutane hapa

Kwa Dar ni kutoka Fire hadi kwenye kivuko cha kigs'
Kwa chugastan ni kutoka Kinana Sec hadi Moyo Safi Catholic Church..almost 15 km
 
Kuna siku nlikuwa natoka kariakoo, mida ya saa 11 naenda mbagala home, kulikuwa na foleni yaan toka kk hadi round about ya badari imechukua masaa 2 ikabidi nishuke nikajua foleni ipo bandari road na kilwa road nikapandie mivinjeni, kufika mivinjeni 55 zote zimezimwa nikasema labda ipo mandela nisogee nipandie uhasibu kufika gari zimezimwa foleni haisogei, nikaona nisogee hadi mtongani nako hali ile ile, nikasogea hadi ktm ndo angalau gari zinatembea na zingine za kwenda kijichi, home ni mbagala kizuiani, nikaona tu ni uchuro bora nienda kwa mguu
 
Nilitembea kwa miguu siku England waliposhinda Rugby World Cup. Barabara zilifungwa nilikuwa ninarudi nyumbani nilitembea mbali sana. Kutoka Holborn mpaka Elephant and Castle.
kumbe upo Brexit ndio maana hulali hovyo kabisa.
 
Mi huwa nshapiga kimara kkoo mwaka jana pekee karibu Mara kumi maana sometimez nauli sina inabidi niende town nikazuge tu ila yakurudi ntapata basi hyo kimara kkoo kwangu ni kawaida Massa yangu 2 nipo fire kitamboo.
 
Mwaka 2015 nikiwa wilayani BUNDA,mkoa wa MARA, kuna jamaa mmoja tulikuwa tunafahamiana nae sana alikuja kutuambia kuna Tsh 100 ya mwaka 1993 zinahitajika na wazungu fulani,hizo Tsh 100 za mwaka huo kwa ambao wanazifahamu ni kwamba zilikuwa na madini fulani ambapo endapo ungeumwa na nyoka,nge,tandu au wadudu wowote wenye sumu kali,basi ulikuwa ukichanja maeneo ya jeraha na ukiiweka hiyo hela basi inanatia kama sumaku na kunyonya sumu yote,wahenga bila shaka wanazifahamu(Kwa kule kwetu tuliziita BODO).Bila shaka yeyote ikabidi tuunganishwe na huyo mzungu kwa wakati huo alikuwa jijini Mwanza,Tanzania,na tuliongea nae sana japo niliongea kiingereza cha elimu ya form 4 alinielewa nami nilimwelewa na alinihakikishia ni kweli kabisa zinahitajika na endapo nitaipata basi yupo tayari kutupatia milioni 100 za kitanzania!,kiukweli ukiwa umekaa kijijini na umepigika kweli kweli unaweza ikawa kama umeamshiwa mashetani vile!,basi tulikaa chini mimi na ndugu yangu na tulihisi ni utapeli,ilibidi twende kwa jamaa mmoja ambaye tulimfahamu na tulimweleza namna mchongo ulivyo,jamaa alituambia hiyo issue ni kweli kabisa kwa maana kuna kipindi fulani zilihitajika Tsh 20 za mwaka fulani(sikumbuki mwaka) na yupo jamaa mmoja yeye aliipata na akaipeleka na akapewa milioni 10 ya wakati huo ( mwaka 2003),sasa ilibidi mimi na ndugu yangu tuelekezwe kwa huyo jamaa ambaye alipewa hela baada ya kupeleka hiyo sh 20.
Tulifika na tukamkuta na tulimweleza na akatuambia hiyo issue ni kweli kwa maana yeye pia liliwahi kumkita hilo zali na akapewa hiyo milioni 10,na akatuambia hata nyumba tuliyofikia aliijenga kwa hiyo hela milioni 10(kumbuka hapa tulikuja kupata confirmation),jamaa alituambia pambaneni japokuwa ni kazi sana kuipata kwa maana hampo peke yenu wapo na watu wengine, "mi ningwasaidia wadogo zangu kutafuta but for now nina kazi zangu na biashara zangu hivyo mambo hayo nimesha achana nayo kitambo" alisema jamaa.
Ilibidi tuanze kuzunguka kutafuta hiyo 100,tulizunguka maduka yote ya pale Bunda mjini bila mafanikio.

Kuna mama mmoja alituambia mara nyingi hizo hela za zamani zinapatikana kwa waganga,alikuwa akielewana na mganga mmoja yupo huko majita,wilaya ya musoma vijijini alituambia twende anaweza kuwa nayo kwa maana anazo pesa nyingi sana za zamani,ilibdi tulale mapema ili kesho yake tuanze safari mapema.

Tulidamka asubuhi ya saa kumi alfajiri tukaanza kutembea ,tulitembea kwa mguu kwa maana hatukuwa na nauli ya kutufikisha tunapokwenda,mimi nilivaa kanda mbili zangu zilizokuwa zimechoka japo si sana na ndugu yangu yeye alivaa kata mbuga zake alizokuwa akiaminia.
Kumbuka ni safari ya kutoka wilaya ya BUNDA kwenda MAJITA wilaya ya musoma vijijini,umbali bila shaka ni zaidi ya kilometa 95 mpaka ufike huko chaka.

Safari ikaanza na ilipofika saa sita mchana tukawa kama tumefika nusu ya safari ilibidi twende kwenye mji mmoja huko huko njiani kuomba chakula,tulipokewa kikarimu sana na tulisongewa ugali wa muhogo na kisamvu,kiukweli tulikula sana ukizingatia tulikuwa na njaa ya kufa mtu,tulimaliza kula na tukaaga na tukaanza safari,tulifika huko porini saa 4 usiku na kiukweli mi nilikuwa nimechoka sana mithiri ya kufa!,tulilala nje kwa maana hakukuwa na nyumba kubwa,kwa waganga mara nyingi kuna kuwa na tuvijumba tudogo tudogo na vyote vilikuwa na wateja wake,hivyo tulikoka moto tukalala nje!!

Jamani story ni ndefu but nacho taka kusema ni kwamba,SITASAHAU HIYO SAFARI YA UMBALI MREFU,KISA TU MAISHA MAZURI.
Duuh pole Mkuu
 
pole sana jaji.
leta story mkuu. Vipi mlirudi kwa miguu? mlikuwa mnaenda makojo nyie sio bure
 
Ni kama kutoka makongo juu mpaka vikindu..
Nilifika hoi na kulala style za ajabu
mkuu mimi siku nimerudi home, nikalala na mdau mmoja nilisumbuka usiku hadi jamaa akadhani namajini. Maana nilikuwa nakoroma hovyo, narusha mateke, sijitambui ila jamaa sikumuambia nini chanzo
 
Upanga-Muhimbili, Bonde la Msimbazi, Magomeni,Mwananyamala, Kijitonyama, Sinza.

Challenge ilikuwa si umbali tu, hapo kati kuna viboda unavuka mtokwa daraja la gogo, ukianguka tu umeangukia maji machafu yanatoka Breweries.

Border lingine Upanga, Muhimbili, Jangwani, Kigogo mpaka Tabata Mandela Road kwenda Ubaya Ubaya.

Ni katika kuujua mji kwa kutembea tu.
mkuu ubaya ubaya hapo unapitia boda ya st mary's chuo cha ualimu unakata dampo kigogo hapo nakubali utafika mapema.

hizo chocho utakuwa umepunguza zaidi ya km 10 na ushee kama ungeenda road kwa road.

nimefurahi kupajua ubayaubaya. Hiyo mitaa alikuwa anaishi mdau wangu mmoja nyuma ya shule ya st marys primary
 
Tuliokulia vijijini kutembea umbali mrefu wala siyo story.

Moja kufuata huduma za kijamii kama hospital, maduka etc

Mbili,kwenda kusaga mahindi vijiji jirani vyenye machine ya diesel.

Kwenda minadani kuuza mazao kilometa kadhaa ili kupata kipata cha familia
 
Hivi unazijua vizuri KM 100? Hafu uzitembee siku 1 hii chai
mkuu soma vizuri.
nimeenda 50, nikalala asubuhi nikageuza 50+ maana wakati wa kwenda nilipitia shortcut ambayo hata wanakijiji ukiwaambia wanashika midomo kwa mshangao maana wao wanapaogopa.
kurudi nilienda road kwa road. Nilikuwa nimevaa viatu vizito kama vya jeshi flani nilipofika vikawa useless maana viliharibika, ilikuwa milimani na kwenya mawe japo kurudi ilikuwa road.
 
mkuu ubaya ubaya hapo unapitia boda ya st mary's chuo cha ualimu unakata dampo kigogo hapo nakubali utafika mapema.

hizo chocho utakuwa umepunguza zaidi ya km 10 na ushee kama ungeenda road kwa road.

nimefurahi kupajua ubayaubaya. Hiyo mitaa alikuwa anaishi mdau wangu mmoja nyuma ya shule ya st marys primary
Nishakaa pande hizo nilikuwa nafanya social experiment kukaa Uswahilini nyumba za kupanga. Nilikaa mwaka mmoja lakini vituko nilivyoona sitasahau maisha yangu yote.

Sasa hapo ilikuwa siku nyegw za kutembea zikinipanda nakatiza kutoka hapo mpaka Segerea. Enzi hizo mapori mapori hakujajengeka sana huko.

Siku hizi Segera kote majumba.
 
Tuliokulia vijijini kutembea umbali mrefu wala siyo story.

Moja kufuata huduma za kijamii kama hospital, maduka etc

Mbili,kwenda kusaga mahindi vijiji jirani vyenye machine ya diesel.

Kwenda minadani kuuza mazao kilometa kadhaa ili kupata kipata cha familia
mkuu kijijini umbali kwa kutoka Gomzi hadi Tegeta kupitia mwenge, unakuwa umefuta vijiji vya kutosha.

nimekuja kugundua dsm unaweza kutembea umbali ambao ukiupeleka kijijini utaonekana shujaa
 
Yeah DSM ni kutokana eneo kubwa kuwa tambalale....ila vijiji vya kwetu ni milima ya hatari na mitelemko mikali......na Gomzi-Tegeta nikaribu sana,sidhani kama km 30 zinafika
 
Back
Top Bottom