HOJA Tuliovaa Jeans, T-shirt, raba tumezuiwa kufanya usaili katika ajira ya TRC, hii ni sawa?

HOJA Tuliovaa Jeans, T-shirt, raba tumezuiwa kufanya usaili katika ajira ya TRC, hii ni sawa?

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Niliitwa kwenye usaili wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), nilipofika katika kituo nilichopangiwa nilikumbana na changamoto ambayo nimeona si sahihi.

Waombaji walikaguliwa vyeti pamoja na mavazi. Wale waliokuwa wamevaa jeans, T-shirt, raba au mavazi ambayo wasimamizi waliona hayakufaa, walipewa karatasi ya kuandika majina na namba zao za simu na wakaelekezwa kutofanya usaili.

Kilichonishangaza ni kwamba nilipouliza kwa nini hatukuona taarifa rasmi kuhusu aina ya mavazi yanayotakiwa, niliambiwa kuwa maelekezo hayo yalikuwa yamewekwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii wiki mbili zilizopita, na baadhi ya waombaji waliambiwa waangalie YouTube.

Kauli nyingine iliyotolewa ni kwamba kizazi cha vijana kimekuwa bize na TikTok. Swali langu ni: kwa nini taarifa muhimu kama hii isiambatishwe moja kwa moja kwenye ujumbe au taarifa ya mwaliko wa usaili?

Kwa kuwa waombaji waliitwa rasmi na kila mmoja akapangiwa kituo chake cha usaili, nadhani ingekuwa rahisi pia kutuma maelekezo yote muhimu, ikiwemo mavazi yanayotakiwa, kupitia njia hiyo hiyo.

Inadaiwa nafasi hiyo ya ufundi umeme ilikuwa na waombaji wengi, hivyo baadhi yetu tunajiuliza kama masharti kama haya yanaweza kuwa yanatumika kupunguza idadi ya wanaofanya usaili. Kama ndivyo, hilo si jambo sahihi na linahitaji ufafanuzi wa TRC ili mchakato wa ajira uwe wa haki, wazi na wenye usawa kwa waombaji wote.
 
Mkuu pole kwa kukosa usaili. Next time zingatia kuwa hizi kazi za Serikali zinakua governed na sheria, kanuni na miongozo mbali mbali ikiwemo Mwongozo wa Mavazi kwa Watumishi wa Umma ambao kama umesoma Elimu ya Juu hapa nchini na umefanya field work kwenye ofisi mbali mbali inatakiwa uwe tayari unalifahamu hilo. NeXT time jiandae vizuri na usisahau kuvaa “official”
 
Pole Sana Mkuu
Kama Ungekuwa Mtoto Wangu Ningekuzaba Kofi Moja Matata Mpaka Uone 🔥
Upuuzi Mkubwa Mno
Unakwendaje Kusailiwa Kwa Mavazi Hayo
Teratibu Za Mavazi Zipo Wazi
Wakristo Wanapopata Komnio/Kipaimara Kwa Wanaume Unaona Suit, Suruali Nyeusi, Shati Jeupe, Tai
Kuna Siri Ya Mavazi

Ungevaa Simple Suaruali Ya Kitambaa Rangi Black, Dark Blue, Shati, Kiatu Cha Ngozi
 
this is pure evil, vipi kama hauwezi kumudu kununua hayo mavazi wanayoyataka? sasa utapanda vipi daraja ktk chini ulipo kama unawekewa vizingiti vyote hivyo mpaka kwenye mavazi? hii nchi inatawaliwa na satanic people ...

angalia hawa watoto wakiwa darasani shuleni wakati wa Christians mwaka 1900 huko, kwa logic ya satanic tanzagiza leo (ambao wengi wao wasingesoma na kufikia kuvaa suti leo kama wangewekewa masharti na vizingiti wanaowawekea watoto wa masikini leo hii) hao watoto wa masikini wangezuiwa kusoma kwa sababu hawakuwa na uwezo wa kununua nguo, lkn cha muhimu ilikuwa ni elimu na ndio maana haikujalisha kama alikuwa ana nguo au hana lkn cha muhimu elimu ...
1787116421112.png
 
this is pure evil, vipi kama hauwezi kumudu kununua hayo mavazi wanayoyataka? sasa utapanda vipi daraja ktk chini ulipo kama unawekewa vizingiti vyote hivyo mpaka kwenye mavazi? hii nchi inatawaliwa na satanic people ...
Wabongo sisi ni wa wapumbavu, kila kitu n kulalamika tuu hata kwenye jambo ambalo ni jukumu lako bado utalalamika tuu.

H kitu hata haihitaji akili ya msingi kuelewa, unaendaje kwenye usaili umevaa tshirt na jinsi, hakuna cha mambo ya evil wala bibi ake evil.

Ww nae ndo wale wale tuu 🗑️
 
Mkuu pole kwa kukosa usaili. Next time zingatia kuwa hizi kazi za Serikali zinakua governed na sheria, kanuni na miongozo mbali mbali ikiwemo Mwongozo wa Mavazi kwa Watumishi wa Umma ambao kama umesoma Elimu ya Juu hapa nchini na umefanya field work kwenye ofisi mbali mbali inatakiwa uwe tayari unalifahamu hilo. NeXT time jiandae vizuri na usisahau kuvaa “official”
Mjadala uishie hapa.
 
this is pure evil, vipi kama hauwezi kumudu kununua hayo mavazi wanayoyataka? sasa utapanda vipi daraja ktk chini ulipo kama unawekewa vizingiti vyote hivyo mpaka kwenye mavazi? hii nchi inatawaliwa na satanic people ...

angalia hawa watoto wakiwa darasani shuleni wakati wa mkoloni, kwa logic ya satanic tanzagiza hao watoto wa masikini wangzuiwa kusoma kwa sababu hawakuwa nauwezo wa kununua nguo
View attachment 3652964
nina imani unatania. kuna suruali na mashati hadi ya 5000. na hizo taarifa mbona zinatolewa huko instagram,facebook,whatsap cahneel kila kukicha?
usitetee ujinga Chief
 
Back
Top Bottom