Hili sio jambo la kulalamikia maana Wanafunzi wanakatazwa mavazi yasiyo stahili tangu mkiwa chuo ila wengi wenu mnajifanya wajuaji na wala hamtaki kuelewa.
Rejea: Taasisi za Serikali na Vyuo vyote unakuta wamebandika kwenye mbao au tovuti ya chuo muongozo wa mavazi/dressing code
Mimi zamani nilikua naenda kwenye interview nimechomekea, baadaye nikawa naenda nimevaa shati na kadeti bila kuchomekea. Ila sijawahi kuwaza kwenda interview na jeans.
Jeans utavaa ukiajiriwa ile Ijumaa au Ijumaa na Jumatano
Wasomi ni wengi kuliko nafasi za ajira hivyo tunatumia interview na vigezo vingine vidogovidogo kupunguza jam,jitahidi kujali vigezo na masharti haiba inasema vingi juu yako kuliko hiyo manila kadi(cheti)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.