HOJA Tuliovaa Jeans, T-shirt, raba tumezuiwa kufanya usaili katika ajira ya TRC, hii ni sawa?

HOJA Tuliovaa Jeans, T-shirt, raba tumezuiwa kufanya usaili katika ajira ya TRC, hii ni sawa?

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Niliitwa kwenye usaili wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), nilipofika katika kituo nilichopangiwa nilikumbana na changamoto ambayo nimeona si sahihi.

Waombaji walikaguliwa vyeti pamoja na mavazi. Wale waliokuwa wamevaa jeans, T-shirt, raba au mavazi ambayo wasimamizi waliona hayakufaa, walipewa karatasi ya kuandika majina na namba zao za simu na wakaelekezwa kutofanya usaili.

Kilichonishangaza ni kwamba nilipouliza kwa nini hatukuona taarifa rasmi kuhusu aina ya mavazi yanayotakiwa, niliambiwa kuwa maelekezo hayo yalikuwa yamewekwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii wiki mbili zilizopita, na baadhi ya waombaji waliambiwa waangalie YouTube.

Kauli nyingine iliyotolewa ni kwamba kizazi cha vijana kimekuwa bize na TikTok. Swali langu ni: kwa nini taarifa muhimu kama hii isiambatishwe moja kwa moja kwenye ujumbe au taarifa ya mwaliko wa usaili?

Kwa kuwa waombaji waliitwa rasmi na kila mmoja akapangiwa kituo chake cha usaili, nadhani ingekuwa rahisi pia kutuma maelekezo yote muhimu, ikiwemo mavazi yanayotakiwa, kupitia njia hiyo hiyo.

Inadaiwa nafasi hiyo ya ufundi umeme ilikuwa na waombaji wengi, hivyo baadhi yetu tunajiuliza kama masharti kama haya yanaweza kuwa yanatumika kupunguza idadi ya wanaofanya usaili. Kama ndivyo, hilo si jambo sahihi na linahitaji ufafanuzi wa TRC ili mchakato wa ajira uwe wa haki, wazi na wenye usawa kwa waombaji wote.
ilitakiwa mtandikwe bakora kabisa.
 
Kwani mavazi nadhifu ni suti tu? Huwezi kuvaa suluari na shati za kawaida na ukaonekana nadhifu?
Sawa sawa mkuu, niliongelea suti kama ishu niionayo, si kama ndo vazi pekee nadhifu

* Niambie mkuu, je mavazi ya kiasili ya Tanzania siku hizi yanaruhusiwa bungeni?
Nilikerwa zamani hata shati la kitenge halikurusiwa.
Binafsi, ningependa kuona wabunge wanavaa mavazi ya kiasili... kwa mfano, Mbunge wa Monduli anaingia na fullu rubega la kimasai... bila silaha of course
 
Vijana wa kitanzania wamekuwa kama manguruwe siku hizi. Sisi miaka ya 70 kabla ya kwenda kwenye interview
🔸 Tulikuwa tunajiandaa nawonekano, tunatafuta na hata kuazima mavazi yatakauotupnyesha tupo smart na ya kiheshima

🔸 Tulikuwa tunanuoa nywele kiheshima , KUEPUKA kupaka manukato , viatu tuna brash

🔸 Tulikuwa tunafanya utafiti kwanza Kwa watu walioajiriwa kwenye kampuni hiyo kujua dressing code ikoje

🔸 Tulipeleleza possible questions na mitego ambayo wabobezi wa interview wa zamani walikuwa wanatutega kupima nidhamu yetu, mfano anazuga amefonfosha kalamu makusudi? tulikuwa tunapeleleza namna ya kusalimia

🔹 Lakini kizazi hiki Cha Nguruwe kinanda kutafuta maisha kina dred kichwani, visuruali havieleweki ni suruali au kaptula halafu kaweka kata k na Wala hakajali. Wa kike ndio balaa kabisa wanakwenda wamevalia kama changu
Hii si ilikuwa kwa ajili ya interview? Utajiandaa ivo kwenda dukani, tuseme supermarket?

Kijana unaemuona kitaani kapiga pamba za kihood... wengi wao bado wanajua nyakati, wakienda interview wanavaa ipasavyo.
 
Wabongo sisi ni wa wapumbavu, kila kitu n kulalamika tuu hata kwenye jambo ambalo ni jukumu lako bado utalalamika tuu.

H kitu hata haihitaji akili ya msingi kuelewa, unaendaje kwenye usaili umevaa tshirt na jinsi, hakuna cha mambo ya evil wala bibi ake evil.

Ww nae ndo wale wale tuu 🗑️
Imagine mtu kama huyo ndio anategemewa aje kuwa afisa kuhudumia wananchi na kichwani ndio yuko hivyo kuna kupata huduma bora hapo?
 
Back
Top Bottom