HOJA Tuliovaa Jeans, T-shirt, raba tumezuiwa kufanya usaili katika ajira ya TRC, hii ni sawa?

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Niliitwa kwenye usaili wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), nilipofika katika kituo nilichopangiwa nilikumbana na changamoto ambayo nimeona si sahihi.

Waombaji walikaguliwa vyeti pamoja na mavazi. Wale waliokuwa wamevaa jeans, T-shirt, raba au mavazi ambayo wasimamizi waliona hayakufaa, walipewa karatasi ya kuandika majina na namba zao za simu na wakaelekezwa kutofanya usaili.

Kilichonishangaza ni kwamba nilipouliza kwa nini hatukuona taarifa rasmi kuhusu aina ya mavazi yanayotakiwa, niliambiwa kuwa maelekezo hayo yalikuwa yamewekwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii wiki mbili zilizopita, na baadhi ya waombaji waliambiwa waangalie YouTube.

Kauli nyingine iliyotolewa ni kwamba kizazi cha vijana kimekuwa bize na TikTok. Swali langu ni: kwa nini taarifa muhimu kama hii isiambatishwe moja kwa moja kwenye ujumbe au taarifa ya mwaliko wa usaili?

Kwa kuwa waombaji waliitwa rasmi na kila mmoja akapangiwa kituo chake cha usaili, nadhani ingekuwa rahisi pia kutuma maelekezo yote muhimu, ikiwemo mavazi yanayotakiwa, kupitia njia hiyo hiyo.

Inadaiwa nafasi hiyo ya ufundi umeme ilikuwa na waombaji wengi, hivyo baadhi yetu tunajiuliza kama masharti kama haya yanaweza kuwa yanatumika kupunguza idadi ya wanaofanya usaili. Kama ndivyo, hilo si jambo sahihi na linahitaji ufafanuzi wa TRC ili mchakato wa ajira uwe wa haki, wazi na wenye usawa kwa waombaji wote.
Unaenda kwenye usaili umevaa tshirt na jeans halafu unategemea nini?
 
nilihisi ulienda interview ya kuigiza filamu, kumbe ya TRC. Tunakoelekea utaenda na nguo za beach msibani na ukitimliwa uone unaonewa. Zingatia mavazi na tukio unaloenda kufanya, siwezi kuhitaji mchimba shimo la choo uje umevaa suti utegemee nikupe kazi.
 
this is pure evil, vipi kama hauwezi kumudu kununua hayo mavazi wanayoyataka? sasa utapanda vipi daraja ktk chini ulipo kama unawekewa vizingiti vyote hivyo mpaka kwenye mavazi? hii nchi inatawaliwa na satanic people ...

angalia hawa watoto wakiwa darasani shuleni wakati wa Christians mwaka 1900 huko, kwa logic ya satanic tanzagiza leo (ambao wengi wao wasingesoma na kufikia kuvaa suti leo kama wangewekewa masharti na vizingiti wanaowawekea watoto wa masikini leo hii) hao watoto wa masikini wangezuiwa kusoma kwa sababu hawakuwa na uwezo wa kununua nguo, lkn cha muhimu ilikuwa ni elimu na ndio maana haikujalisha kama alikuwa ana nguo au hana lkn cha muhimu elimu ...
View attachment 3652964
Kama aliweza kununua hizo alizovaa basi ana uwezo wa kununua nguo decent kwa ajili ya usaili. Kama alikwama basi hata angeazima.
 
Niliitwa kwenye usaili wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), nilipofika katika kituo nilichopangiwa nilikumbana na changamoto ambayo nimeona si sahihi.

Waombaji walikaguliwa vyeti pamoja na mavazi. Wale waliokuwa wamevaa jeans, T-shirt, raba au mavazi ambayo wasimamizi waliona hayakufaa, walipewa karatasi ya kuandika majina na namba zao za simu na wakaelekezwa kutofanya usaili.

Kilichonishangaza ni kwamba nilipouliza kwa nini hatukuona taarifa rasmi kuhusu aina ya mavazi yanayotakiwa, niliambiwa kuwa maelekezo hayo yalikuwa yamewekwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii wiki mbili zilizopita, na baadhi ya waombaji waliambiwa waangalie YouTube.

Kauli nyingine iliyotolewa ni kwamba kizazi cha vijana kimekuwa bize na TikTok. Swali langu ni: kwa nini taarifa muhimu kama hii isiambatishwe moja kwa moja kwenye ujumbe au taarifa ya mwaliko wa usaili?

Kwa kuwa waombaji waliitwa rasmi na kila mmoja akapangiwa kituo chake cha usaili, nadhani ingekuwa rahisi pia kutuma maelekezo yote muhimu, ikiwemo mavazi yanayotakiwa, kupitia njia hiyo hiyo.

Inadaiwa nafasi hiyo ya ufundi umeme ilikuwa na waombaji wengi, hivyo baadhi yetu tunajiuliza kama masharti kama haya yanaweza kuwa yanatumika kupunguza idadi ya wanaofanya usaili. Kama ndivyo, hilo si jambo sahihi na linahitaji ufafanuzi wa TRC ili mchakato wa ajira uwe wa haki, wazi na wenye usawa kwa waombaji wote.
Ni sawa,msilete uhuni kwenye public service, dressing codes ni muhimu
 
Shida unatafuta utetezi sehemu ambayo sio sahihi kulingana na uelewa wako wa kisasa! Hata wasinge tangaza swala la mavazi unadhani kwa idadi ya watu walioomba nafasi hiyo wangepunguzwaje? Ishu ya kunyumbulika kwenye swala la utafutaji wa ajira ni muhimu, hiii inatoa picha ya wazi kwamba huna ushirikiano na watu ambao tayari walisha pita njia hizo za ajira maana kwa vyovyote vile ungeshirikisha watu baadhi ungekuwa umejipanga kiakili na muonekano na sio hayo pekee, sasa kwenye hili ndio liwe funzo kwako na kwa wengine jitahid Sana kujifunza makosa yaliyo pita.
 
Nakumbuka 2014 kipindi nafuatilia Passport yangu, hapo Posta ofisi za uhamiaji na makao makuu ya wizara ya mambo ya ndani...nilikuwa nimenyuka kinyamwez...beli white na pensi flani matata timber flani hivi....sijui kitu yoyote mzee....kuhusu protokali zao...

Naenda kuchukua Passport yangu(Intn'l)...! Nikwee pipa to Lubumbashi...

Nilizuiliwa Getini tu!......nilinunua jeans kwa machinga hapo nje kidogo kama mita 20 tokea getini hapo kwa 50k...

Jeans ambayo karume ningeipata kwa si zaidi ya 15k...

Ofisi yoyote ya serikali wako strict sana na swala mavazi chief....
 
Niliitwa kwenye usaili wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), nilipofika katika kituo nilichopangiwa nilikumbana na changamoto ambayo nimeona si sahihi.

Waombaji walikaguliwa vyeti pamoja na mavazi. Wale waliokuwa wamevaa jeans, T-shirt, raba au mavazi ambayo wasimamizi waliona hayakufaa, walipewa karatasi ya kuandika majina na namba zao za simu na wakaelekezwa kutofanya usaili.

Kilichonishangaza ni kwamba nilipouliza kwa nini hatukuona taarifa rasmi kuhusu aina ya mavazi yanayotakiwa, niliambiwa kuwa maelekezo hayo yalikuwa yamewekwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii wiki mbili zilizopita, na baadhi ya waombaji waliambiwa waangalie YouTube.

Kauli nyingine iliyotolewa ni kwamba kizazi cha vijana kimekuwa bize na TikTok. Swali langu ni: kwa nini taarifa muhimu kama hii isiambatishwe moja kwa moja kwenye ujumbe au taarifa ya mwaliko wa usaili?

Kwa kuwa waombaji waliitwa rasmi na kila mmoja akapangiwa kituo chake cha usaili, nadhani ingekuwa rahisi pia kutuma maelekezo yote muhimu, ikiwemo mavazi yanayotakiwa, kupitia njia hiyo hiyo.

Inadaiwa nafasi hiyo ya ufundi umeme ilikuwa na waombaji wengi, hivyo baadhi yetu tunajiuliza kama masharti kama haya yanaweza kuwa yanatumika kupunguza idadi ya wanaofanya usaili. Kama ndivyo, hilo si jambo sahihi na linahitaji ufafanuzi wa TRC ili mchakato wa ajira uwe wa haki, wazi na wenye usawa kwa waombaji wote.

Huku kuiga ng'ambo ya zamani kumezidi. Yaani eti mtu avae suti na kujinyonga na tai ndo mheshimiwa. Walounda suti wanaishi nchi za baridi, sisi bado tumeingia mkumbo... joto sasa, uwe umeivaa Dzm, kwa mfano.

Kitu kikubwa nilichoshangaa binafsi, ni vile wamesahau wewe ni mteja si mfanyakazi wao, wanafikiaje kumwambia mteja cha kuvaa?

anyway, kama jeans na t-shirt hazikuwa hood style, na ziling'ara usagi - basi sioni mlikosea nini.
 
Niliitwa kwenye usaili wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), nilipofika katika kituo nilichopangiwa nilikumbana na changamoto ambayo nimeona si sahihi.

Waombaji walikaguliwa vyeti pamoja na mavazi. Wale waliokuwa wamevaa jeans, T-shirt, raba au mavazi ambayo wasimamizi waliona hayakufaa, walipewa karatasi ya kuandika majina na namba zao za simu na wakaelekezwa kutofanya usaili.

Kilichonishangaza ni kwamba nilipouliza kwa nini hatukuona taarifa rasmi kuhusu aina ya mavazi yanayotakiwa, niliambiwa kuwa maelekezo hayo yalikuwa yamewekwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii wiki mbili zilizopita, na baadhi ya waombaji waliambiwa waangalie YouTube.

Kauli nyingine iliyotolewa ni kwamba kizazi cha vijana kimekuwa bize na TikTok. Swali langu ni: kwa nini taarifa muhimu kama hii isiambatishwe moja kwa moja kwenye ujumbe au taarifa ya mwaliko wa usaili?

Kwa kuwa waombaji waliitwa rasmi na kila mmoja akapangiwa kituo chake cha usaili, nadhani ingekuwa rahisi pia kutuma maelekezo yote muhimu, ikiwemo mavazi yanayotakiwa, kupitia njia hiyo hiyo.

Inadaiwa nafasi hiyo ya ufundi umeme ilikuwa na waombaji wengi, hivyo baadhi yetu tunajiuliza kama masharti kama haya yanaweza kuwa yanatumika kupunguza idadi ya wanaofanya usaili. Kama ndivyo, hilo si jambo sahihi na linahitaji ufafanuzi wa TRC ili mchakato wa ajira uwe wa haki, wazi na wenye usawa kwa waombaji wote.
Kwa kuwa ulikuwa unasaka ajira kwenye utumishi wa umma, jeans na tshirt sio mavazi rasmi. Jinsi ulivyotokea siku ya usaili ndivyo watu wanavyokuona ulivyo, kama uko nadhifu utaonekana nadhifu, kama uko shamble basi utaonekana hivyo hivyo. Waliokuzuia walikuwa sahihi kwa 100%.
 
Nyie genzii mnahitaji matambiko
Kuna wale waliwekewa viti wakae wasubiri wakaamua kutangantanga, eti hawataki kuwekwa kama mifugo sehemu moja, kumbe walikuwa wanachorwa kwenye makamera,
Wakaenda kufunga milango, walioko nje ndio imetoka wakaambiwa wapotee, waliobaki ndani wakaendelea na usaili.
Safi sana
 
Niliitwa kwenye usaili wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), nilipofika katika kituo nilichopangiwa nilikumbana na changamoto ambayo nimeona si sahihi.

Waombaji walikaguliwa vyeti pamoja na mavazi. Wale waliokuwa wamevaa jeans, T-shirt, raba au mavazi ambayo wasimamizi waliona hayakufaa, walipewa karatasi ya kuandika majina na namba zao za simu na wakaelekezwa kutofanya usaili.

Kilichonishangaza ni kwamba nilipouliza kwa nini hatukuona taarifa rasmi kuhusu aina ya mavazi yanayotakiwa, niliambiwa kuwa maelekezo hayo yalikuwa yamewekwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii wiki mbili zilizopita, na baadhi ya waombaji waliambiwa waangalie YouTube.

Kauli nyingine iliyotolewa ni kwamba kizazi cha vijana kimekuwa bize na TikTok. Swali langu ni: kwa nini taarifa muhimu kama hii isiambatishwe moja kwa moja kwenye ujumbe au taarifa ya mwaliko wa usaili?

Kwa kuwa waombaji waliitwa rasmi na kila mmoja akapangiwa kituo chake cha usaili, nadhani ingekuwa rahisi pia kutuma maelekezo yote muhimu, ikiwemo mavazi yanayotakiwa, kupitia njia hiyo hiyo.

Inadaiwa nafasi hiyo ya ufundi umeme ilikuwa na waombaji wengi, hivyo baadhi yetu tunajiuliza kama masharti kama haya yanaweza kuwa yanatumika kupunguza idadi ya wanaofanya usaili. Kama ndivyo, hilo si jambo sahihi na linahitaji ufafanuzi wa TRC ili mchakato wa ajira uwe wa haki, wazi na wenye usawa kwa waombaji wote.
Mbinu za kupunguza lawama za ukosefu wa Akira,na malalamiko ya upendeleo na rushwa,walengwa Wana weza kuwa na maelekezo ya do's and don't hivyo katika mazingira hayo itaonekana mwenyewe ndiyo umezingua,ila yote ya yote Akira unayoomba jifumzehata standard dress codes na hata do,'s and don't itakupa nafasi ya kulinda haki yako ya kupata KAZI na kufanya KAZI.
 
Unaenda zako kupiga usaili na raba ya FILA/NIKE/REEBOK... 😊

Kuhusu mada: Zama hizi za watu wengi kuhitaji kazi msaili/interviewer anaweza set kigezo chochote cha mchujo na akawa sahihi. 😊
Lengo ni kuwachuja, maana mpaka mmeitwa maana yake wote mna sifa ya kupata kazi hiyo.
Pole sana job seeker, siku nyingine usirudie huo uzembe.
 
Back
Top Bottom