HOJA Tuliovaa Jeans, T-shirt, raba tumezuiwa kufanya usaili katika ajira ya TRC, hii ni sawa?

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Niliitwa kwenye usaili wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), nilipofika katika kituo nilichopangiwa nilikumbana na changamoto ambayo nimeona si sahihi.

Waombaji walikaguliwa vyeti pamoja na mavazi. Wale waliokuwa wamevaa jeans, T-shirt, raba au mavazi ambayo wasimamizi waliona hayakufaa, walipewa karatasi ya kuandika majina na namba zao za simu na wakaelekezwa kutofanya usaili.

Kilichonishangaza ni kwamba nilipouliza kwa nini hatukuona taarifa rasmi kuhusu aina ya mavazi yanayotakiwa, niliambiwa kuwa maelekezo hayo yalikuwa yamewekwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii wiki mbili zilizopita, na baadhi ya waombaji waliambiwa waangalie YouTube.

Kauli nyingine iliyotolewa ni kwamba kizazi cha vijana kimekuwa bize na TikTok. Swali langu ni: kwa nini taarifa muhimu kama hii isiambatishwe moja kwa moja kwenye ujumbe au taarifa ya mwaliko wa usaili?

Kwa kuwa waombaji waliitwa rasmi na kila mmoja akapangiwa kituo chake cha usaili, nadhani ingekuwa rahisi pia kutuma maelekezo yote muhimu, ikiwemo mavazi yanayotakiwa, kupitia njia hiyo hiyo.

Inadaiwa nafasi hiyo ya ufundi umeme ilikuwa na waombaji wengi, hivyo baadhi yetu tunajiuliza kama masharti kama haya yanaweza kuwa yanatumika kupunguza idadi ya wanaofanya usaili. Kama ndivyo, hilo si jambo sahihi na linahitaji ufafanuzi wa TRC ili mchakato wa ajira uwe wa haki, wazi na wenye usawa kwa waombaji wote.
Muwe mnazingatia code za mavazi ya watumishi wa Umma.

Wadogo zangu wa UDSM naamini Profesa Anangisye atakuwa amewajenga sana kwenye eneo la mavazi ya staha au decent wearing.
 
Kijana umesoma mpaka chuo kikuu halafu hujui mavazi stahiki kwa kazi unayoomba, hii ni aibu! Mojawapo ya mbinu ya kushinda usaili wa kuomba kazi ni namna ya ulivyovaa kwenye usaili
 
Wewe ni mzembe 😁😁😁 maana ua usaili wa mchujo ni kwamba watu wapo wengi sana wanatafuta kigezo cha kupunguza baadhi ya waombaji. Vigezo hivyo huwa kama vile mavazi kutokufuata sheria, kutozingatia maelezo, siku nyingine ukiitwa kwenye issue yoyote inayohusu serikali vaa official dress code
 
sasa unafikiri kila mtu an uwezo wa kutoa shilingi 5000? kwa kuwa tu wewe unaweza siyo kila mtu anaweza, mko soo out touch with reality na jamii yenuu wenyewe iliowanguka na ndiyo maana hatuwezi kutoka hapa, kwa maana mlio juu hamjali walio chini, kwangu mimi hata kama wangekuja kifua wazi kama hawawezi kumudu kununua lkn wana akili wanapata kazi ...
Waombe kazi siku wakiweza kupata hiyo 5000 ya kununua suruali nzuri. Waache usumbufu.
 
Niliitwa kwenye usaili wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), nilipofika katika kituo nilichopangiwa nilikumbana na changamoto ambayo nimeona si sahihi.

Waombaji walikaguliwa vyeti pamoja na mavazi. Wale waliokuwa wamevaa jeans, T-shirt, raba au mavazi ambayo wasimamizi waliona hayakufaa, walipewa karatasi ya kuandika majina na namba zao za simu na wakaelekezwa kutofanya usaili.

Kilichonishangaza ni kwamba nilipouliza kwa nini hatukuona taarifa rasmi kuhusu aina ya mavazi yanayotakiwa, niliambiwa kuwa maelekezo hayo yalikuwa yamewekwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii wiki mbili zilizopita, na baadhi ya waombaji waliambiwa waangalie YouTube.

Kauli nyingine iliyotolewa ni kwamba kizazi cha vijana kimekuwa bize na TikTok. Swali langu ni: kwa nini taarifa muhimu kama hii isiambatishwe moja kwa moja kwenye ujumbe au taarifa ya mwaliko wa usaili?

Kwa kuwa waombaji waliitwa rasmi na kila mmoja akapangiwa kituo chake cha usaili, nadhani ingekuwa rahisi pia kutuma maelekezo yote muhimu, ikiwemo mavazi yanayotakiwa, kupitia njia hiyo hiyo.

Inadaiwa nafasi hiyo ya ufundi umeme ilikuwa na waombaji wengi, hivyo baadhi yetu tunajiuliza kama masharti kama haya yanaweza kuwa yanatumika kupunguza idadi ya wanaofanya usaili. Kama ndivyo, hilo si jambo sahihi na linahitaji ufafanuzi wa TRC ili mchakato wa ajira uwe wa haki, wazi na wenye usawa kwa waombaji wote.

Pole sana,

Kabla ya kwenda kwenye usaili ni muhimu kufanya maandalizi na uchunguzi kidogo wa kampuni au taasisi husika ili ujue utaratibu wao kuendesha mambo ikiwemo uvaaji nk.

Siku hizi mitandao imejaa elimu kuhusu namna ya kujiandaa na kukabili usaili (interview) kwa hiyo jifunze humo na utafanikiwa.

Kila la kheri.
 
Pole Sana Mkuu
Kama Ungekuwa Mtoto Wangu Ningekuzaba Kofi Moja Matata Mpaka Uone 🔥
Upuuzi Mkubwa Mno
Unakwendaje Kusailiwa Kwa Mavazi Hayo
Teratibu Za Mavazi Zipo Wazi
Wakristo Wanapopata Komnio/Kipaimara Kwa Wanaume Unaona Suit, Suruali Nyeusi, Shati Jeupe, Tai
Kuna Siri Ya Mavazi

Ungevaa Simple Suaruali Ya Kitambaa Rangi Black, Dark Blue, Shati, Kiatu Cha Ngozi

No hakuna aliyezaliwa akajua so mpe darasa akirudi fanya utakayo.
 
Niliitwa kwenye usaili wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), nilipofika katika kituo nilichopangiwa nilikumbana na changamoto ambayo nimeona si sahihi.

Waombaji walikaguliwa vyeti pamoja na mavazi. Wale waliokuwa wamevaa jeans, T-shirt, raba au mavazi ambayo wasimamizi waliona hayakufaa, walipewa karatasi ya kuandika majina na namba zao za simu na wakaelekezwa kutofanya usaili.

Kilichonishangaza ni kwamba nilipouliza kwa nini hatukuona taarifa rasmi kuhusu aina ya mavazi yanayotakiwa, niliambiwa kuwa maelekezo hayo yalikuwa yamewekwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii wiki mbili zilizopita, na baadhi ya waombaji waliambiwa waangalie YouTube.

Kauli nyingine iliyotolewa ni kwamba kizazi cha vijana kimekuwa bize na TikTok. Swali langu ni: kwa nini taarifa muhimu kama hii isiambatishwe moja kwa moja kwenye ujumbe au taarifa ya mwaliko wa usaili?

Kwa kuwa waombaji waliitwa rasmi na kila mmoja akapangiwa kituo chake cha usaili, nadhani ingekuwa rahisi pia kutuma maelekezo yote muhimu, ikiwemo mavazi yanayotakiwa, kupitia njia hiyo hiyo.

Inadaiwa nafasi hiyo ya ufundi umeme ilikuwa na waombaji wengi, hivyo baadhi yetu tunajiuliza kama masharti kama haya yanaweza kuwa yanatumika kupunguza idadi ya wanaofanya usaili. Kama ndivyo, hilo si jambo sahihi na linahitaji ufafanuzi wa TRC ili mchakato wa ajira uwe wa haki, wazi na wenye usawa kwa waombaji wote.
Dressing code ni muhimu hasa serikalini na mashirika yake. Vaa nguo za kawida tu. Suruali na gauni za kawaida ndio nzuri
 
WEWE KILAZA WALIKUWA SAHIHI KUWAKATA.
 
Back
Top Bottom