HOJA Tuliovaa Jeans, T-shirt, raba tumezuiwa kufanya usaili katika ajira ya TRC, hii ni sawa?

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Pole Sana Mkuu
Kama Ungekuwa Mtoto Wangu Ningekuzaba Kofi Moja Matata Mpaka Uone 🔥
Upuuzi Mkubwa Mno
Unakwendaje Kusailiwa Kwa Mavazi Hayo
Teratibu Za Mavazi Zipo Wazi
Wakristo Wanapopata Komnio/Kipaimara Kwa Wanaume Unaona Suit, Suruali Nyeusi, Shati Jeupe, Tai
Kuna Siri Ya Mavazi

Ungevaa Simple Suaruali Ya Kitambaa Rangi Black, Dark Blue, Shati, Kiatu Cha Ngozi
wewe ndo lipuuzi promax! unaleta habari ya suti za komonio kwani aliomba kz kanisani? hovyo kbs!
 
Niliitwa kwenye usaili wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), nilipofika katika kituo nilichopangiwa nilikumbana na changamoto ambayo nimeona si sahihi.

Waombaji walikaguliwa vyeti pamoja na mavazi. Wale waliokuwa wamevaa jeans, T-shirt, raba au mavazi ambayo wasimamizi waliona hayakufaa, walipewa karatasi ya kuandika majina na namba zao za simu na wakaelekezwa kutofanya usaili.

Kilichonishangaza ni kwamba nilipouliza kwa nini hatukuona taarifa rasmi kuhusu aina ya mavazi yanayotakiwa, niliambiwa kuwa maelekezo hayo yalikuwa yamewekwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii wiki mbili zilizopita, na baadhi ya waombaji waliambiwa waangalie YouTube.

Kauli nyingine iliyotolewa ni kwamba kizazi cha vijana kimekuwa bize na TikTok. Swali langu ni: kwa nini taarifa muhimu kama hii isiambatishwe moja kwa moja kwenye ujumbe au taarifa ya mwaliko wa usaili?

Kwa kuwa waombaji waliitwa rasmi na kila mmoja akapangiwa kituo chake cha usaili, nadhani ingekuwa rahisi pia kutuma maelekezo yote muhimu, ikiwemo mavazi yanayotakiwa, kupitia njia hiyo hiyo.

Inadaiwa nafasi hiyo ya ufundi umeme ilikuwa na waombaji wengi, hivyo baadhi yetu tunajiuliza kama masharti kama haya yanaweza kuwa yanatumika kupunguza idadi ya wanaofanya usaili. Kama ndivyo, hilo si jambo sahihi na linahitaji ufafanuzi wa TRC ili mchakato wa ajira uwe wa haki, wazi na wenye usawa kwa waombaji wote.
Maelekezo ya mavazi na namna ya kuvaa kwenye usahili hua wanatoa kila mara wala siwatetei but next time unavyoenda kwenye usahili em jarib kuuliza au kutembelea page ya sekretariet utaona kila kitu kinacho hitajika
 
Kwa akili tu za kawaida nafasi labda 10 waombaji 200 unaanzaje kuwapunguza na mifumo yetu siyo rafiki ya kusaili watu wote hao kwa undani. Mwanzoni hatua zinzotumika ndio hizo mavazi, wazembe, wajuaji kama mleta mada, wachelewaji, n.k.

Mimi naamini hata ukiwa masikini kiasi gani huwezi kukosa suruali yako nzuri ya kitambaa, shati lako zuri na viatu pea moja vyote vya mtumba. Nguo zikafulia na kunyooshhwa vizuri tu na kiatu kung'arishwa vizuri tu na mtu akaonekana nadhifu.

Mwisho ofisi nyingi za serikali zina taratibu za mavazi na zipo wazi labda kama wewe sio raia wa nchi ndio hauzifahamu. Hivyo ulivyova mleta mada unaweza kwenda kwenye usaili wa kamapuni binafsi na ukaruhusiwa kufanya usaili vizuri tu na hata kuajiriwa bila shaka yoyote.
 
😁😂

Juzi kati nimepiga zangu konyagi ile nimetoka natembea

Njia nyembamba kwa mbele jamaa kasimama katikati ya barabara anachati anachati Hana habari kabisa na jezi ya Simba na kitumbo tumbo chake

Nikatembea nikampiga kikumbo ki makusudii aka Anza kulalamika nikamwambia njia nyembamba kama unataka kuchati au kuchezea simu simama pembeni TULIA maliza jambo lako endelea na mishe zakoo

Tukakoromeana tuka achana kimjini mjinii
Pombe ikakugawia confidence sio? Siku ingine utapigwa dokta🤣
 
Mkuu pole kwa kukosa usaili. Next time zingatia kuwa hizi kazi za Serikali zinakua governed na sheria, kanuni na miongozo mbali mbali ikiwemo Mwongozo wa Mavazi kwa Watumishi wa Umma ambao kama umesoma Elimu ya Juu hapa nchini na umefanya field work kwenye ofisi mbali mbali inatakiwa uwe tayari unalifahamu hilo. NeXT time jiandae vizuri na usisahau kuvaa “official”
Kwani yeye ni mtumishi wa umma?
 
Lengo la interview, ni kupunguza watu ili kupata wachache ambao wataweza kupewa kazi husika.
Hivyo basi, ni wajibu kwa anaefanyiwa usaili kujiepusha na sababu ndogo ndogo ikiwemo, mavazi, muda wa kufika, kufuata maelekezo. Otherwise usimlaumu mtu, hivi vitu ni known.
 
Niliitwa kwenye usaili wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), nilipofika katika kituo nilichopangiwa nilikumbana na changamoto ambayo nimeona si sahihi.

Waombaji walikaguliwa vyeti pamoja na mavazi. Wale waliokuwa wamevaa jeans, T-shirt, raba au mavazi ambayo wasimamizi waliona hayakufaa, walipewa karatasi ya kuandika majina na namba zao za simu na wakaelekezwa kutofanya usaili.

Kilichonishangaza ni kwamba nilipouliza kwa nini hatukuona taarifa rasmi kuhusu aina ya mavazi yanayotakiwa, niliambiwa kuwa maelekezo hayo yalikuwa yamewekwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii wiki mbili zilizopita, na baadhi ya waombaji waliambiwa waangalie YouTube.

Kauli nyingine iliyotolewa ni kwamba kizazi cha vijana kimekuwa bize na TikTok. Swali langu ni: kwa nini taarifa muhimu kama hii isiambatishwe moja kwa moja kwenye ujumbe au taarifa ya mwaliko wa usaili?

Kwa kuwa waombaji waliitwa rasmi na kila mmoja akapangiwa kituo chake cha usaili, nadhani ingekuwa rahisi pia kutuma maelekezo yote muhimu, ikiwemo mavazi yanayotakiwa, kupitia njia hiyo hiyo.

Inadaiwa nafasi hiyo ya ufundi umeme ilikuwa na waombaji wengi, hivyo baadhi yetu tunajiuliza kama masharti kama haya yanaweza kuwa yanatumika kupunguza idadi ya wanaofanya usaili. Kama ndivyo, hilo si jambo sahihi na linahitaji ufafanuzi wa TRC ili mchakato wa ajira uwe wa haki, wazi na wenye usawa kwa waombaji wote.
Unaruhusiwa kupinga mchakato wa usaili, kama unaamini haukupew taarifa ya kutosha. Usiishie kulalamika tu, nitafute twende mahakamani upate haki yako ya kufanyiwa usahili
 
Nyie genzii mnahitaji matambiko
Kuna wale waliwekewa viti wakae wasubiri wakaamua kutangantanga, eti hawataki kuwekwa kama mifugo sehemu moja, kumbe walikuwa wanachorwa kwenye makamera,
Wakaenda kufunga milango, walioko nje ndio imetoka wakaambiwa wapotee, waliobaki ndani wakaendelea na usaili.
 
Niliitwa kwenye usaili wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), nilipofika katika kituo nilichopangiwa nilikumbana na changamoto ambayo nimeona si sahihi.

Waombaji walikaguliwa vyeti pamoja na mavazi. Wale waliokuwa wamevaa jeans, T-shirt, raba au mavazi ambayo wasimamizi waliona hayakufaa, walipewa karatasi ya kuandika majina na namba zao za simu na wakaelekezwa kutofanya usaili.

Kilichonishangaza ni kwamba nilipouliza kwa nini hatukuona taarifa rasmi kuhusu aina ya mavazi yanayotakiwa, niliambiwa kuwa maelekezo hayo yalikuwa yamewekwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii wiki mbili zilizopita, na baadhi ya waombaji waliambiwa waangalie YouTube.

Kauli nyingine iliyotolewa ni kwamba kizazi cha vijana kimekuwa bize na TikTok. Swali langu ni: kwa nini taarifa muhimu kama hii isiambatishwe moja kwa moja kwenye ujumbe au taarifa ya mwaliko wa usaili?

Kwa kuwa waombaji waliitwa rasmi na kila mmoja akapangiwa kituo chake cha usaili, nadhani ingekuwa rahisi pia kutuma maelekezo yote muhimu, ikiwemo mavazi yanayotakiwa, kupitia njia hiyo hiyo.

Inadaiwa nafasi hiyo ya ufundi umeme ilikuwa na waombaji wengi, hivyo baadhi yetu tunajiuliza kama masharti kama haya yanaweza kuwa yanatumika kupunguza idadi ya wanaofanya usaili. Kama ndivyo, hilo si jambo sahihi na linahitaji ufafanuzi wa TRC ili mchakato wa ajira uwe wa haki, wazi na wenye usawa kwa waombaji wote.
Ni sawa mlivyorudishwa, kwanza ilitakiwa mfutwe kabisa , Mtaendaje kwenye interview na jeans na raba??? Hata kwa kutumia common sense tu hayo sio mavazi ya interview popote pale duniani. Mkome.
 
Back
Top Bottom