Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Duh aise hii story imenigusa vilivyo
 
Leo ndio nimesoma huu Uzi. Nimesoma taratibu na kwa makini ila kwako hapa nimecheka sana japo kwingineko nilikuwa nahuzunika.

Dah nashindwa nishee kipi niache kipi ili wengine pia wajifunze toka kwangu nilichopitia, niliko sasa na nnakoenda.

Nna mengi ya kusimulia watu pia wakajifunza mengi yanafanana na waliokeisha simulia. Lakini kuinuka na nnakoenda na somo juu ya mikopo nnalo kubwa sana

Nitafungua uzi kisha nita utag huu ili nielimishe wengi
 
Pole sana
Mkasa wako umenikumbusha Jose

Gf wake alimshawishi akakope wawekeze kwenye zile pesa za majini,

Jose akakopa akauza mpaka gas ya ndani kwake ili wapate pesa

Jamaa walivyotoweka Gf akaanza kumtukana Jose, jamaa akapambana akalipa madeni mpaka leo maisha yake yamebadilika sana.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] poleeee
 
Very sad...
 
Uko sahihi
 
Nimecheka aiseee. Unazama unaibuka...siku zinakwenda
 
Wewe ulikuwa Unatuma pesaa bila Kufatilia Kama biashara ipo au vip??
 
Asilimia kubwa ya watu huangushwa na ndugu zao,mimi niwe muwazi huwa kwanza simkopeshi ndugu yangu,nampa tu kwa kile ninachokiweza na nisichokiweza simpi. Pili sijawahi Kumshirikisha ndugu yangu yeyote miradi yangu au biashara sababu ndugu zangu wana tamaa ya pesa,wanatamani mambo makunwa wakati hawana uwezo (kama samaki anaetamani kuishi nchi kavu) na wengi ndio wanakopa ela ndogo kama laki 3-5 na zwnyewe wanashindwa kulipa mpaka muda mwingine inabidi niingilie kati kuwasaidia maana wana dharirika sana,na nishawahi kudharirishwa mimi kwa mkopo wa ndugu yangu (sitokaa nisahau mpaka polisi yalifika).
So nachopenda kuwashauri,usimwamini mtu duniani hapa 100% weka na sehemu ya mashaka na use na sehemu ya kuamini mashaka yako,lakini wakati huo huo bakiza na sehemu ya kuamini.
Poleni kwa wote mliokutwa na visanga mbalimbali vya mikopo.
Natamani atokee mtu afungue Uzi jinsi ndugu walivyoturudisha nyuma,nadhani nitaandika na kuchangia huo Uzi huku nalia.
 

Tunasubiri uo uzi mkuu jitahidi uandike tupate chochote umo maana hii ni zaidi ya shule..
 
Nimecheka aiseee. Unazama unaibuka...siku zinakwenda
Uscheke mkuu wangu mjini balaa na biashara zina majaribu, unatakiwa uwe na roho sugu. 2016 niligombana na watu wa benki, nawaambia pesa imekata sina uwezo wa kulipa deni lenu uzeni tu nyumba wao wanaskiliza maneno ya wanafki pembeni wanadai nimeficha pesa, mnagombanaa unaweza sema hamji kuongea tena, baada ya mwaka unawaona wanakuja kukubembeleza ukope tena! Biashara nyingi bila mkopo haziendi.
 
Kweli kabisa, kama ulitoka kwenu kwenda mjini kutafuta endelea kutafuta mpaka upate...usirudishe excuses huko kwenu haziwasaidii kitu! Tafuta ukipata utaendaga tu hata uzeeni.
 
Unadhifu huficha mengi,watu wanakuona huna shida,unazo kumbeeeee.
Ila ni kweli mikopo husaidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…