Baada ya kuchoka mishahara ya wahindi niliamua kujiajiri, nikawa nafanya biashara ndogondogo maisha yanaenda, nilikuwa nachukia Mikopo Sana, baada kuingia Kwenye biashara hukuhuku nikaona bora niingie Kwenye vikundi vya wanawake pamoja na Vicoba, nilikuwa na Vicoba vitatu na vikundi vinne vyote nilikuwa na vihudumia naweka tu Pesa sikopi.
Baada ya story za Mikopo za wanachama wenzangu Sasa na Mimi nikaona acha nikope bank nifungue biashara yangu moja ya uwakika nikakopa mil 10 marejesho miaka mitatu, Pesa yote niliingiza Kwenye mzunguko wa biashara mwaka wa kwanza marejesho yalienda Safi Kabisa mwaka wa pili matatizo yakaanza biashara zikafa nikabaki na shamba la korosho na msimu Kama mnavyojua mwaka kwa mwaka. ikawa ikifika tarehe ya rejesho nakopa Kwenye kikundi napeleka bank ikafika wakati vikoba vyote vitatu na vikundi mpaka wanachama wananidai Huku rejesho bado halijaisha la bank.
Nikavuna korosho nikasema Pesa Itanisaidia kupunguza madeni, mwanaume niliyekuwa naye akanishauri usilipe Pesa yote madeni zungushia biashara Huku unalipa madeni kidokidogo. Pesa nikampa mpenzi tuzungushe biashara akanidhulumu ikafika wakati sina hata mia mfukoni marafiki wote wamenikimbia bank nadaiwa, kila kona na madeni Sina kazi Sina biashara nilala ndani Kisa madeni ya watu ya riba mitaan sitaki kukumbuka nilisota nakusota. Ndugu Zangu ikabidi wajichangishe kulipa Mkopo WA bank iliyobaki maana ilibaki miez michache niliiweka dhamana viwanja vyangu viwili. Wakaona bora wanisaidie kuliko vipigwe mnada wakati nilibakisha kidogo.
Hii Mikopo mingine ya vikundi, vikoba na mitaani watu walinidai mpaka walikaa kimya na kuchoka maana Sina kitu Niko mweupeeeee. Baada ya kuumalizika Mkopo WA bank nikauza kiwanja kimoja nikalipa lipa madeni ya mitaani nikabakiza Pesa kidogo nikaaza na moja biashara
Sasa hivi sitaki kusikia Mikopo, vikoba Wala vikundi maana kwa wanawake wengi humo Ndio Huwa Chanzo cha matatizo na wahanga ni wengi maana humo watu wana ushawishi wa ajabu, Kama Sina najua Sina ila Sina Deni na mtu kuliko huna alafu udaiwe utatamani ufe kwa muda. Mikopo inaumiza .