Nimepitia kwa makini sana michango ya wachangiaji wengi kwenye uzi huu.
Kutokana na uzoefu wangu na wachangiaji wengine, kukopa pesa ufanye biashara ikisimamiwa na ndugu au rafiki ni kujitakia kuishi kama shetani.
Watu hutofautiana uwezo na access ya kukopa. Wengine humu nimeona wanauwezo wa kukopeshwa million 10 wengine 20 na wengine mpaka million 200.
Kwenu nyinyi wenzangu tunaoweza kukopeshwa chini ya million 10, hakikisheni kama ndio kwanza tunanza kukopa kwa ajili ya kuanzisha biashara basi tubuni biashara inayoweza anza kwa mkopo ambao unaweza kuulipa kwa kipindi cha mwaka 1 tu deni liwe limeisha. Hii husaidia kupunguza ukubwa wa riba na hata ikitokea biashara imekufa muda wa kusota huwa mfupi sana.
Binafsi huwa na ndoto ya kuwa na mtaji wa hata million 50 lakini hujiambia biashara kubwa kiasi hicho sharti izaliwe na biashara nyingine ndogo niliyo ikopea kwa makato ya mwaka mmoja tu na si vinginevyo.
Kama hatuwezi kuanzisha biashara kwa makato ya mwaka mmoja tu basi hata tukikopa mapesa mengi ya kukatwa mika 4 biashara hiyo haiwezi fanikiwa.
Kama unataka kopa pesa kununua bodaboda ya biashara si kitu kibaya, ila jipime kwanza kama wewe mwenyewe utakuwa tayari kuipigia kazi in case madereva wanakusumbua alafu ukisha kuwa na bodaboda weka mashaliti magumu kwa dereva unayetaka kumkabidhi hasa juu ya upotevu kama itatokea.
Madereva wengi hupoteza bodaboda kizembe sana hivyo ni bora muandikishiane namna atakavyo wajibika kuilipa iwapo itatokea upotevu wowote ule na kama hajiwezi kabisa basi awe na mdhamini wake. Kumkabidhi mtu pikipiki bila mkataba ni sawa na kutupa pesa chooni.
Binasfi niko mbioni kwenda kopa pesa kununua bodaboda ya biashara lakini kama nitakosa dereva wa uhakika wa kumkabidhi mimi mwenyewe nitaingia barabarani kama ufanisi wangu wa kazi nilikoajiliwa utadhorota kutokana na mimi kwenda kazini nimechoka poa tu sito jali hilo maadam nisipopambana na hali yangu hakuna wa kunisaidia dunia hii.