huu uzi nimeusoma mwanzo mwisho......kila mtu ametoa lake la moyoni kuhusu changamoto alizopitia baada ya kuchukua mkopo....
changamoto nilizoziona ni:
a. mtu anakopa kabla ya kubuni afanye nn na hizo hela
b. mtu anakopa anaanzisha project anamweka ndugu
c. mtu anakopa, pale mwanzo kabla ya kuanzisha project anajikuta anazitumbua wee kuja kustuka robo au nusu ya hela inakua imeshakata
d. mtu unakopa let say 10mil, unajitutumua pale mwanzo mara paap 1m inapotea bila kufanya la maana, mara umenunua hiki, mara ulikua na kiporo cha deni siku nyingi, theni iliyobakia unatafuta frem kwa mda wa mwezi(nimekadiria mwezi kwa sababu unaweza pata sehem ambayo hujaridhika nayo kwa mazingira ya biashara,) unapata unalipia kodi, unanunua vitu muhimu kama fridge, mizani, meza, kiti, kabati, unatafuta leseni, mara paap inabaki na 3mil, unafungua kiduka kidogo biashara inayumba hapo unaanza kukabwa marejesho... ni lazma ufeli tu na kama uliweka nyumba dhamana itauzwa maana hauna namna... kwa wale waajiriwa hiki kipindi utakua unaishi kama lucifer mkuu..
ushauri
a. usikope hela kabla ya kujua hela utaifanyia nini, tena uwe na taarifa sahihi khs utakachokifanya mfano ufugaji, biashara ama kilimo
b. usikope hela ukajenge au ununue kiwanja, kopa hela uifanyie project hela iwe inazunguka
c.usikope hela ukaanzishe project ambayo hukuwahi kuifanya before, hata kama unazo taarifa sahihi khs unachotaka kwenda kukifanya, lazima utafeli
d. mkopo mzuri ule ambao unakopa kupanua kile ambacho tayari unacho mfano, una biashara yako ushaijulia mzunguko wake, lakn una mtaji mdogo, unaweza kukopa hela ukainedeleza
e. hii ni njia nzuri zaidi, ili ufaidi mkopo wako fanya haya... tufanye mfano wa duka,,, chukulia una duka moja lenye thamani ya 10mil,linakulipa vzr tu na mzunguko uko poa, then ghafla ukapata dili lingine mfano ufugaji wakuku, na inahtaj 4mils. kw a haraka haraka hiki kiasi ni kikubwa sana compared na mtaji wako wa 10mils, kuzipata mara moja ni ngumu hapa utalazimika kukopa,, sasa ukikopa fanya hivi, tengeneza utaratibu wa kufanya serving kwenye ile biashara yako then ufanye marejesho, mdogo mdogo, then ule mradi uliofungua kwa mkopo uwe unakua taratibu, aft one year piga hesabu angalia ni nini ambacho umeambulia kama faida ? then jilipe mwenyewe kwa kuwa ulikua unajikopa kwenye duka kulipa marejesho, hapo utajua faida na hasara iko wapi