Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Hahahhaa, watumishi wa serikali naona mikopo inawaumiza kweli, hii ni kwa sababu tu hamzijuwi mbilinge na mishe za mtaa. Mke wangu mimi naye anaendelea kulipa mkopo wa pesa nyingi ambazo alikopa, akafungua duka na kununua pikipiki kadhaa. Wakati anaenda kukopa hakuniomba ushauri wowote, lakini mimi niliziona forms za mkopo...skumuuliza kwa sababu ni non of my business.

Alipoingiziwa pesa akaja kunambia amechukua mkopo wa pesa kadhaa anataka kufungua duka la rejareja anaomba nimsaidie kupata wasambazaji wa bidhaa kwa bei nzuri na kumsaidia hesabu jioni. Skuwa na hiyana, nikamwambia Duka la rejareja sina uzoefu nalo, lakini to what I know linahitaji usimamizi wa karibu sana muda wote uwepo dukani, na wote ninaowafaham mimi waliofanikiwa kwa biashara hiyo wanashinda dukani full time, yeye akanijibu ameshaamua, na ana maono makubwa sana mbele juu ya biashara hiyo.

Basi nikamsaidia kupata wauzaji wa bidhaa ninaowafaham akajaza mzigo dukani, suala la kusimamia hesabu nilimwambia akomae yeye mimi muda wangu uko tight afanye yeye mwenyewe (nikweli sikuwa na muda, na skutaka kujihusisha na biashara nisiyo na uelewa nayo), akanunua na pikipiki nne mishe zikaanza. Haukuisha mwaka anaomba nimwongezee pesa ya pango la duka!!!

Pikipiki zote ameshauza kwa kugombana na madereva. Wakati huo sisi wazee wa mishemishe tunazama na kuibuka, ukigeukia huku unatandikwa ukiinuka unacharaza biashara zinakwenda na mikopo tunachukua yakushiba vilevile, nyumba za kukopea zipo na tunaendelea kkujenga, ukiona mkopo huu biashara unayofanyia imezingua unawauzia benki nyumba pesa unahamishia kwenye biashara nyingine kunakuchwa kunakucha mishe zinaendelea.

Nyie watoto wa mama mmezowea kuingiziwa pesa kwa mwenzi wengi wenu mnaishi kwa ndoto bila kujua kukaza, japo wapo wengi pia ambao tunapigana nao vikumbo mjini wanakomaa na wanafanya poa sana tu!
 
Hii mada imenigusa kidogo.... Inaonekana wadau wengi wanachukua mikopo withno gud plan.... Mkopo sio wakujengea nyumba au kuanzia biashara, mkopo ni mtam sana kwa ajili ya kuendeleza bzness, chukua mkopo kulingana na mahitaji ya biashara yaako kwani pesa ikizid mahtaji ndo hapo utakaponza kuitumia hovyo.

Kabla yakukopa fanya bzness kwa kpato kidogo ulichonacho ili upate uzoefu wa hyo bznar, mfano wewe ni wakala wa mpesa anza hata na mtaji wa laki7 mzunguko wako ndo utakwambia ukope shngapii...
 
Hii D9 hii ilitaka kunipiga dole la kijambio...
Jamaa yangu alinishawishi sana nitafute 4.8 Millioni nijiunge package ya Gold+ ya D9.
Kwa mahesabu ni kuwa kila week nalipwa 170 USD, hivo kwa mwezi napata 630 USD (baada ya makato) ambayo ni zaidi ya 1.3 Millioni.
Hivo nilikua na uhakika ule mtaji wa 4.8 Millioni ningerudisha ndani ya miezi mitatu hivi na week mbili...

Nikaenda kuomba mkopo taasisi moja hivi, mkopo wa 5 Millioni. Marejesho jumla ningetakiwa kulipa 6.5 Millioni.
Mkopo ilikua nipate cku hiyo hiyo tatizo nilikua sina Salary Slip ya mwezi mmoja hivi, ikabidi niende kuifatilia kesho waniingizie mpunga.
Kesho yake niko njiani kupeleka Slip, nikaingia Jamiiiforums, nakuta uzi watu wanasema Danilo Santana CEO wa D9 amekamatwa na Polisi wa Brazil... Account zake zimekua suspended...

Kubabake, nikageuza kwanza kurudi ghetto. Jamaa wa mkopo kanipigia simu kishenz "Boss mbona hauji, si ushapata Salary Slip.. Wahi nakusubiri uweke signature hapa tukuwekee pesa yako"
Nikamwambia nampeleka mama yangu Kairuki nakuja kesho boss...

Nikasema ngoja kwanza nisikilizie hatma ya D9 kwanza...
Mpaka leo bado natembea na ile Salary Slip kwenye bag langu la Ofisini na bado sijajua D9 itarudi lini.
Kubabake leo hii ningelikua nakatwa mshahara kwa mkopo ulioyeyuka hewani.
Mkuu nimecheka mnoo . Dah mie kunajamaa ananishawishi niingie bitclub lakin moyo unagoma
 
Hahahhaa, watumishi wa serikali naona mikopo inawaumiza kweli, hii ni kwa sababu tu hamzijuwi mbilinge na mishe za mtaa. Mke wangu mimi naye anaendelea kulipa mkopo wa pesa nyingi ambazo alikopa, akafungua duka na kununua pikipiki kadhaa. Wakati anaenda kukopa hakuniomba ushauri wowote, lakini mimi niliziona forms za mkopo...skumuuliza kwa sababu ni non of my business. Alipoingiziwa pesa akaja kunambia amechukua mkopo wa pesa kadhaa anataka kufungua duka la rejareja anaomba nimsaidie kupata wasambazaji wa bidhaa kwa bei nzuri na kumsaidia hesabu jioni. Skuwa na hiyana, nikamwambia Duka la rejareja sina uzoefu nalo, lakini to what I know linahitaji usimamizi wa karibu sana muda wote uwepo dukani, na wote ninaowafaham mimi waliofanikiwa kwa biashara hiyo wanashinda dukani full time, yeye akanijibu ameshaamua, na ana maono makubwa sana mbele juu ya biashara hiyo. Basi nikamsaidia kupata wauzaji wa bidhaa ninaowafaham akajaza mzigo dukani, suala la kusimamia hesabu nilimwambia akomae yeye mimi muda wangu uko tight afanye yeye mwenyewe (nikweli sikuwa na muda, na skutaka kujihusisha na biashara nisiyo na uelewa nayo), akanunua na pikipiki nne mishe zikaanza. Haukuisha mwaka anaomba nimwongezee pesa ya pango la duka!!! Pikipiki zote ameshauza kwa kugombana na madereva. Wakati huo sisi wazee wa mishemishe tunazama na kuibuka, ukigeukia huku unatandikwa ukiinuka unacharaza biashara zinakwenda na mikopo tunachukua yakushiba vilevile, nyumba za kukopea zipo na tunaendelea kkujenga, ukiona mkopo huu biashara unayofanyia imezingua unawauzia benki nyumba pesa unahamishia kwenye biashara nyingine kunakuchwa kunakucha mishe zinaendelea. Nyie watoto wa mama mmezowea kuingiziwa pesa kwa mwenzi wengi wenu mnaishi kwa ndoto bila kujua kukaza, japo wapo wengi pia ambao tunapigana nao vikumbo mjini wanakomaa na wanafanya poa sana tu!
bado hujamalizia ilikuaje huo mkopo wa mkeo
 
Hii D9 hii ilitaka kunipiga dole la kijambio...
Jamaa yangu alinishawishi sana nitafute 4.8 Millioni nijiunge package ya Gold+ ya D9.
Kwa mahesabu ni kuwa kila week nalipwa 170 USD, hivo kwa mwezi napata 630 USD (baada ya makato) ambayo ni zaidi ya 1.3 Millioni.
Hivo nilikua na uhakika ule mtaji wa 4.8 Millioni ningerudisha ndani ya miezi mitatu hivi na week mbili...

Nikaenda kuomba mkopo taasisi moja hivi, mkopo wa 5 Millioni. Marejesho jumla ningetakiwa kulipa 6.5 Millioni.
Mkopo ilikua nipate cku hiyo hiyo tatizo nilikua sina Salary Slip ya mwezi mmoja hivi, ikabidi niende kuifatilia kesho waniingizie mpunga.
Kesho yake niko njiani kupeleka Slip, nikaingia Jamiiiforums, nakuta uzi watu wanasema Danilo Santana CEO wa D9 amekamatwa na Polisi wa Brazil... Account zake zimekua suspended...

Kubabake, nikageuza kwanza kurudi ghetto. Jamaa wa mkopo kanipigia simu kishenz "Boss mbona hauji, si ushapata Salary Slip.. Wahi nakusubiri uweke signature hapa tukuwekee pesa yako"
Nikamwambia nampeleka mama yangu Kairuki nakuja kesho boss...

Nikasema ngoja kwanza nisikilizie hatma ya D9 kwanza...
Mpaka leo bado natembea na ile Salary Slip kwenye bag langu la Ofisini na bado sijajua D9 itarudi lini.
Kubabake leo hii ningelikua nakatwa mshahara kwa mkopo ulioyeyuka hewani.
mkuu kuna jamaa mmoja alikuja pia kunipump sijui D9 inaleta usenge gani nikamwambia sina muda hata wa kukusikiliza we endelea na mambo yako... siku si nyingi nikasikia jamaa anatembea anaongea barabarani peke ake ..
 
Hebu nipe namba za huyo dada yako nimfunze adabu.
hahahaaaa babu bwana

unajua ndugu wengine ukitaka kufanya nao kazi au biashara wanakuwa hawaelewi umeptaje pesa mpaka mkaanza kuingia partner wao wanachojua ni kula tu hizo pesa pasipo kufanyia kitu chochote kwani haziwahumi hawajui kuwa mtu unatafutaje pesa kwa jasho hata mm ningemchapa viboko huyo sista hahaaa
 
Eti mkuu kuna nyingine ipo FB wanajiita VICOBA FOCUS.

Wanatangaza unaweza kukopa kuanzia 5m-10m kupitia hiyo app yao kwa kujaza fomu inayopatikana FB na kutakiwa ulipe amana ambayo ni10% ya mkopo unaohitaji.

Naomba kuthibitishiwa huo mkopo kweli upo? Maana nina shida ya kuongeza mtaji kama 2m hivi.
Watu kama nyie mkipigwa pesa mi huwa hata siumii.
 
Huu mkasa nilishautoaga humu, sio mbaya nikirudia. Okay nitaelezea in first person view.

Mwaka 2011, nilikuwa nimeacha kazi serikalini, nikaamua kuanza biashara ndogo ndogo kwani zililipa kuliko mshahara wa kazini. Hapa nilikuwa na girlfriend ambae nilimtambulisha nyumbani na kwao pia walinijua. Mimi na huyu gf wangu tulifungua kampuni moja, nitaaiita Xcorp. Gf wangu yeye alikuwa muajiriwa wa serikali(mwanasheria), kwahiyo alikuwa vizuri in terms of lifestyle. Basi tukaamua kuexpand business, tuliplan kujenga kumbi nne ambazo zitakuwa za kisasa... Tuliplan kuweka swimming pool, malls humo humo. Ilitakiwa 1bil. Tukasema we can make it. Wakati naendelea na vibiashara vidogo vidogo vya kwenda China, rafiki yangu wa kike akanitambulisha kwa rafiki yake. Nae alikuwa mdada. Huyu dada nitamuita Grace. Grace alionekana ni mtu mwenyewe mafanikio sana. Aliishi Masaki nyumba ina swimming pool, na counter, pia alikuwa akitumia magari ya bei; BMW X5, Hilux new model, Brevis, Mark X na Range Rover. Kwa kweli enzi hizo Mark X na Brevis zilikuwa za kuhesabu barabarani. Huyu dada akaniambia yeye ni mfanyakazi wa kampuni ya mtandao mkubwa hapa Tz. Basi akaniambia wanaproject lakini inaitaji investors. Hii project ilikuwa kama ndoto ya mchana kwani ndani ya mwaka mmoja ningepata 1B.

Nikamueleza gf, akanielewa. Basi mwanzo tukawekeza 40m tu. Kweli ndani ya wiki mbili tulipata faida ya 40m!!! So tukarudishiwa 80m!!! Aisee nikapiga picha, ile biashara ya China bora niiache kwanza mikiki mikiki ya bandarini na mzigo hapa Tz unakaa miezi miwili plus kuja kuisha na faida ni kama 40% tu. Basi Grace akanichombeza ningeongeza hela ya kuwekeza to 400m. Ningepata 800m faida na ningekaribia goal ya 1b. Nikauza viwanja vyote, magari yote(nilikuwa nayo 8) sikubakiza hata moja, mtaji wa China wote nikakusanya. Nikawa na kama 230m. Nikamuomba Gf aniongezee, akagoma, akaingiza maswala ya kwamba mimi natembea na Grace(hii story nyingine) ila sio kweli. Baadae Gf akaniambia kwanini usiombe mkopo kwa nyumba yako. Duh nikasema poa. Gf ndio alikuwa na connection na watu wa benki basi tukaomba mkopo kwa kutumia kampuni yetu, nikaweka nyumba dhamana. Hapa ndipo natamani ningerudisha siku nyuma.

Wiki ambayo mkopo ulikuwa unatakiwa utoke sikupigiwa wala nini. Nikakaa kimya. Wiki ya pili nikaenda ile benki. Wakaniambia mbona ulikuja kuchukua na ukasign kabisa. Duh nikaenda kuangalia, signature sio yangu, na hela kweli zimeingia, lakini ajabu zimeingia kwenye account ya Gf. Nikampigia hapo hapo. Nilimuwakia sana. Akaniambia hela alishampa Grace 400m. Mkopo tulipata 156m, ilibidi turudishe 200m in 1 year. Dadeki nikaona huu utani. Nikamfata Gf home tulifokeana sana(advice usioe/usiolewe na mwanasheria kama hujui ubishi) nikatulia. Akaingiza mambo ya mimi kutoka na Grace, mara haniamini. Ajabu ni kwamba asilimia kubwa ya vitu at risk ni vyangu yeye kwenye biashara ya China alinipaga kama 30m tu. Kwasababu nilimpenda nikakausha. Grace wiki ya kwanza tuliongea freshi tu, ila baada ya wiki akapotea.

Duh wasiwasi ukanijia. Ila nikasema tusubiri ule muda aliosema hela zitarudi. Muda ukapita Grace hatujui alipo. Gf akanigeuzia kibao mimi. Mara mimi ndio nilimtambulisha kwake. Basi nikamfata yule dada aliyenitambulisha. Akaniambia yeye hayupo karibu nae. Aisee nilitamani kuua mtu. Yeye mwenyewe kweli alivyoniunganisha nae sikumueleza yaliyoendelea. Kwanza alikuwa hajui kama nafanya biashara na Grace. Kwenda kwake Grace nakuta kahama na nyumba ilikuwa ya kupanga sio yake. Magari ya kukodi, yeye alikuwa na BMW X5 tu. Nikaenda kampuni ya simu aliosema ni mfanyakazi, hajulikani!!! Nilikaa chini kwenye floor. Miezi ikapita.

Gf alivyoona nimeishiwa, akawa distant, mara hapokei simu. Matusi kwa wingi, baada ya muda akaniacha. Life lilikuwa gumu. Mwezi uliobidi turudishe mkopo ukaingia, sina mia. Ndugu ndio wananitumia hela ya kula. Siku mbili zinaweza pita nyumbani giza, sina hela ya LUKU. Mboga nzuri ilikuwa dagaa mchele. Grace hajulikani halipo. Basi nikaanza kumkazia Gf, kumtishia kuwa alifoji signature yangu. Basi akawa na uwoga nae akaanza kunisaidia kumtafuta Grace. Akafanikiwa, alimuweka Grace ndani kama wiki nzima kabla hajapata mdhamana. Nikaja kujua ukweli, kumbe Grace ni tapeli hata zile hela za mwanzo zilirudi kwasababu aliwachimba wengine. Kiukweli life lake ni show tu ya kuwateka watu. Basi tukambana, akatupa documents za nyumba yake moja. Akasema ndio alichonacho, BMW lake kuna victim mwingine alishalichukua na bado ana mdai Grace 40m. Therefore nae akagangania documents za nyumba. Tukaongea na polisi, maana Mimi nadai 400m mwenzangu 40m bora nipewe Mimi. Polisi wakasema twende court, mwenyewe sina hata mia. Na yule mdai mwingine yupo vizuri kifedha, as you all know bila hela mahakamani... Acha nisimalizie. Nikaongea na mdai, nikamwambia tuuze nyumba nitamlipa 40m alafu nitachukua iliyobaki. Akakubali ila yeye abaki na documents.

Mzaa. Nyumba haina hati, kwanza value 260m ya kwangu ilikuwa 516m. Kwasababu sina kitu nikakubaliana na hali halisi. Nyumba ya Grace ilikuwa haijamalizika, matengenezo kama 40m, ilikuwa golofa. Nyumba haikuuzika mwaka mzima. Baada ya muda wa kupiga stop order, benki wakapiga mnada nyumba yangu nikahamia ghetto. Nikaanza kupaona kuzimu aisee. Nikasema nisue benki maana walicheza mchezo na Gf, na hela sina za kupambana nao. Nikaona nikimtubua Gf nitajiharibia mwenyewe. Basi Grace tukaachana nae kwani na yeye kapigika mbaya.

Huu mwaka wa 5 tangu nyumba yangu iuzwe. Nakaa jumba amabalo mvua ikinyesha maji yanaingia godoro linaloa. Sina gari wala baiskeli. Nikiona mtu ana starlet namuona Mungu. Msosi nasaidiwa na ndugu. Bado nipo kwenye harakati za kutafuta mteja wa nyumba ya Grace hata kwa 150m nauza nianze upya.


Back to third person view. Gf ana life jingine na kidume mwingine, life is good. Ila Gf yupo hatarini, kwani soon TAKUKURU will be after her. Huu mkasa umemtokea ndugu yangu wa karibu sana. Siku anatimuliwa na polisi kwake alilala mpaka kwenye mchanga analia. Na nyumba yake mpaka leo wateja wanakuja na kuchomoa, haijauzwa. Mpaka watu wa benki wanaleta waganga wafanye manyanga. Nyumba imekaa haina watu mpaka walinzi wa benki wanapangisha vyumba vya ndani. Huyu ndugu yangu kakimbiwa na watu wengi wa karibu kwasababu wanajua kaishiwa. Anyway lesson learnt, Mimi namuomba Mungu aniepushe na haya. Bora niishi na salary au biashara ndogo kuliko kukopa. Ukikopa unakuwa mtumwa.

-callmeGhost
Mmmmh hatar nipe link Mkuu ya huo Uzi nipite nao Mdogo Mdogo kuna mengi ya kujifunza


Stay strong mkuu
 
Wakuu hembu kwa anayeijua KUNET naomba anidadavulie mama yangu mzazi wamemshika kweli kweli na masemina yao .
 
Wafanyakazi wengi, Mkopo wa kwanza huwa wanakosea...wapo wengine makosa hayo, huendelea kuyafanya hata baada ya makosa ya Mkopo wa kwanza.

Biashara na kazi inahitaji plans iliyoenda Shule, na unapo anza Biashara kopa hata kwa rejesho la mwaka mmoja tu...ili makosa au hasara utako ipata kwenye Biashara yako kwa Mara ya kwanza, after a year utakuwa umeshajifunza mengi na hutarudia tena...then kopa tena kwa mwaka moja...baada ya kukomaa ktk Biashara....ndpo sasa unaweza kuongeza loan period hata 2-3yrs...ili uendelee kupata experience...
 
Wakuu hembu kwa anayeijua KUNET naomba anidadavulie mama yangu mzazi wamemshika kweli kweli na masemina yao .
mwambie aingie kichwa kichwa apigwe pesa. watanzania huwa hawasikii mpaka wanapomaliza kutapeliwa.
 
Kuna jamaa m1 alichukua kama mkopo benki moja sijui kiasi gani. Ananunua kiwanja kibaha akajenga kufika katika linta hela ikakata. Akakosa hata hela ya kodi alipopanga cz makato yalikuwa makubwa hakubalikiwa na kiasi cha kumtosheleza na alikuwa ameoa. Kelele za mama mwenye nyumba ikabidi mkewe akasirike arudi kwao Moshi. Yeye ikabidi ahamie kibaha hivyo hivyo.

Sasa balaa hata nauli ya kwenda kazini ilikuwa mtihani. Ikawa mtoro kazini. Anaenda Mara 1 au 2 kwa wiki kazini. Kesi za utoro zikazidi akasimamishwa kazi. Jamaa kapagawa. Maana hana kitu kabisa. Mkewe wameachana na naskia aeolewa na mtu mwingine. Naskia yuko bagamoyo analima vibarua.
 
Mimi nilikopa mwaka jana NMB Mi. 9 kwa miaka mitano. Nikachukua pikipiki mbili. Moja ya bodaboda na nyingine ya kwangu kutembelea. Mil.4 nikachukua kiwanja na shamba kwa ajili ya kilimo. Laki 5 nikalimisha shmaba na kupanda mahindi na laki tano nikafanyia mambo yangu menginene. Mshahara nikabaki 247,000

Matokeo yake;

i)Bodaboda ilidumu miezi sita ikaibiwa.
ii) mahindi sikupata hata nusu gunia,kwa sababu ya ukame.
iii)mipango yangu ilikuwa mwaka huu nioe kama mambo yangeenda vizur kinyume chake nimeshindwa,mchumba wangu alipoona hali imekuwa tete akaanza visa kumbe kashaanza mahusiano na mwanaume mwingine,nikabaki mimi kama mimi.
iv)Baada ya bodi ya mkopo kuanza kukata 15% nikaanza kuchukua 197,000/= kwa mwezi
v) kwa sasa siwezi saidia chochote kwa mama na ndugu zangu kibaya zaidi mdogo wangu kachaguliwa chuo cha afya diploma ada mil.2. 5 sijaweza kumpa hata mia.

Sina bahati kabisa
bahati unayo tu.

Ila pole... bado una mtaji wa million 4 ulipo... umiza ndonga utaiona braza
 
Kuna mshkaji wangu mmoja miyeyusho sana nikikumbuka nashindwa kumwelewa aliwaza nn..
Iko hv jamaa alikuwa amepungukiwa budget ya harusi yake alichowaza ni kuniomba hati ya kiwanja changu ili apewe mkopo na taasis flan ya fedha,ofisi yake haikuweza kumsponsor kwani alikuwa still under probation,nakumbuka nilimwangalia huku nikiwaza mengi na kumpa jibu rahisi tu HAIWEZEKANI.

Akaenda akapambana kivyake harusi ikafanyika kibishi...alipotoka tu honeymoon kakuta kibarua kimeota nyasi.
Niliwaza kimoyomoyo je ningeendekeza ushkaji nikampa hati yangu ili tu apate mkopo wa kuolea angekuja na stori gani,?

Nadhani kuna haja ya kuanzisha darasa kwa wakopaji wapate elimu tuelewa in deep lengo la uwepo wa mikopo ili tufunguke akili zaidi tusiingie kwenye mikopo kichwakichwa na kuambulia stress
 
Back
Top Bottom