muhoozi
JF-Expert Member
- Dec 16, 2015
- 231
- 244
yego nyambhuyeteeee wasuFunzo tosha mkuu aya maisha aya wakwaya wanasema omurume ni kwikaza ukiregeza abhakukaza wish you happy strong day aluta continue
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
yego nyambhuyeteeee wasuFunzo tosha mkuu aya maisha aya wakwaya wanasema omurume ni kwikaza ukiregeza abhakukaza wish you happy strong day aluta continue
Amang'ana mazomu wasu uliyo go ogenderera kutikiyego nyambhuyeteeee wasu
Dah mpe pole sana mkuu!! Kwasababu hana mtu jitahidi uwe nae karibu maana kwa upweke anaweza hata kuwa chizi asee!! Pia kama ukiweza mpe tafu jitahidi umuinue hata aanze biashara...mpe sapoti mkuu!!!Huyu ndugu yangu kakimbiwa na watu wengi wa karibu kwasababu wanajua kaishiwa. Anyway lesson learnt, Mimi namuomba Mungu aniepushe na haya. Bora niishi na salary au biashara ndogo kuliko kukopa. Ukikopa unakuwa mtumwa.
Utaibiwa hutasahauEti mkuu kuna nyingine ipo FB wanajiita VICOBA FOCUS.
Wanatangaza unaweza kukopa kuanzia 5m-10m kupitia hiyo app yao kwa kujaza fomu inayopatikana FB na kutakiwa ulipe amana ambayo ni10% ya mkopo unaohitaji.
Naomba kuthibitishiwa huo mkopo kweli upo? Maana nina shida ya kuongeza mtaji kama 2m hivi.
Samahan ndugu yangu sina maana mbaya ivi kwa mfano uo mshahara wa 197 000 kabla ujakatwa kodi yyt unalipwa sh ngapMimi nilikopa mwaka jana NMB Mi. 9 kwa miaka mitano. Nikachukua pikipiki mbili. Moja ya bodaboda na nyingine ya kwangu kutembelea. Mil.4 nikachukua kiwanja na shamba kwa ajili ya kilimo. Laki 5 nikalimisha shmaba na kupanda mahindi na laki tano nikafanyia mambo yangu menginene. Mshahara nikabaki 247,000
Matokeo yake;
i)Bodaboda ilidumu miezi sita ikaibiwa.
ii) mahindi sikupata hata nusu gunia,kwa sababu ya ukame.
iii)mipango yangu ilikuwa mwaka huu nioe kama mambo yangeenda vizur kinyume chake nimeshindwa,mchumba wangu alipoona hali imekuwa tete akaanza visa kumbe kashaanza mahusiano na mwanaume mwingine,nikabaki mimi kama mimi.
iv)Baada ya bodi ya mkopo kuanza kukata 15% nikaanza kuchukua 197,000/= kwa mwezi
v) kwa sasa siwezi saidia chochote kwa mama na ndugu zangu kibaya zaidi mdogo wangu kachaguliwa chuo cha afya diploma ada mil.2. 5 sijaweza kumpa hata mia.
Sina bahati kabisa
Unalipwa sh ngapMbona mnanitisha wakuu nataka inivute mil 15 crdb then nikachukue nyumba kuna jamaa kafail kufanya mrejesho so ameona bora aniuzie mimi nyumba yake kuliko kupigwa mnada daa kanitia nyege kichizi nataka nivumilie ila niwe nishapata nyumba maana kujenga ni mbinde siku hizi
Izo zinakua imani tu imagine ww bila kurubuniwa na mtu yyt unaamua kuweka nyumba dhamana umeshindwa kulipa kuna mtu atakua amekuonea zaidi upambane na hali yakoMimi katika vitu sitaweza kufanya ni kununua nyumba ya mtu aliyeshindwa kulipa deni inanipaka simanzi sana.
Napata hisia si nyumba yangu nakosa uhuru nayo hasa ukizingatia ilipigwa mnada au aliuza bila kupenda.
Kuna jamaa yangu alinunua nyumba iiyopigwa mnada na bank alikaa mwaka mmoja tu baada ya hapo aliondoka na kujenga nyumba nyingine na ile anauza mpaka leo hajapata mtu.
Yule jamaa baada ya kupigwa mnada nyumba yake amekuwa chizi kabisa na familia imesambaratika huwa anapita hapo kwenye nyumba karibu kila siku na kuchorachora chini mambo yasioelewa pia kutamka maneno yasioleweka jamaama akaona isiwe tabu amejenga nyumba nyingine ila ndiyo hiyo nyingine hauziki kila mtu anajua historia yake.
So mkuu kuwa makini jiridhishe kama kweli jamaa anauza kiroho safi na haitamletea msongo wa kimawazo huku mbeleni pia vipi familia yake wanajua hilo?
huko mbele ya safari urafiki wenu utadimu? Jamaa atakuwa huru kukutrmbelea kwenye nyumba yako ili hali labda yeye amepanga?
Nakushauri usichekelee tu faidi ya kwako binafsi, mbona hiyo hela unaweza kupata eneo zuri tu ukaanza ujenzi kwa nguvu zako.
Ni siri kaka mshaharaUnalipwa sh ngap
Kuna mmoja tunafanyanae kaz,likizo ilipokaribia akachukua loan 4m kwamba akifika hom arekebishe nyumba ya wazazi wake,alipoikamata 4m hata likizo akaahirisha kwenda hom,akabaki mjini akazitumbua zote zikaisha bila kununua hata kochi Mpya getoni kwake[emoji3] [emoji3] [emoji3]Ahsante sana trust no one aisee hasa ndugy coz huwezi kumfunga wala kumpeleka polisi
Dah, maneno mazito sana ndugu yangu, umetoa somo zito sana hongeraMimi katika vitu sitaweza kufanya ni kununua nyumba ya mtu aliyeshindwa kulipa deni inanipaka simanzi sana.
Napata hisia si nyumba yangu nakosa uhuru nayo hasa ukizingatia ilipigwa mnada au aliuza bila kupenda.
Kuna jamaa yangu alinunua nyumba iiyopigwa mnada na bank alikaa mwaka mmoja tu baada ya hapo aliondoka na kujenga nyumba nyingine na ile anauza mpaka leo hajapata mtu.
Yule jamaa baada ya kupigwa mnada nyumba yake amekuwa chizi kabisa na familia imesambaratika huwa anapita hapo kwenye nyumba karibu kila siku na kuchorachora chini mambo yasioelewa pia kutamka maneno yasioleweka jamaama akaona isiwe tabu amejenga nyumba nyingine ila ndiyo hiyo nyingine hauziki kila mtu anajua historia yake.
So mkuu kuwa makini jiridhishe kama kweli jamaa anauza kiroho safi na haitamletea msongo wa kimawazo huku mbeleni pia vipi familia yake wanajua hilo?
huko mbele ya safari urafiki wenu utadimu? Jamaa atakuwa huru kukutrmbelea kwenye nyumba yako ili hali labda yeye amepanga?
Nakushauri usichekelee tu faidi ya kwako binafsi, mbona hiyo hela unaweza kupata eneo zuri tu ukaanza ujenzi kwa nguvu zako.
Mpaka dakika hii inaonesha tayari jamaa kashakufanyia shiriki, hali ya kutokuwa huru na mali yako kwa mazingira kama haya, ni dalili tosha kuwa kuna shiriki imefanyika. Fanya mpango ujikwamue kwenye shiriki hiyo Mkuu.. Pole sana..Mimi nimechukua mwaka huu, lakini ni wa mwaka mmoja. Mwezi wa tatu namaliza deni. Nilichukua ninunue boda boda lakini huyu jamaa niliyempa boda boda badala ya kuleta hela analeta stories. Yaani najuta kwanini nilichukua. Kuna wakati natamani niichukue halafu nipige bei ili nikalipe deni lililosalia lakini nahofia jamaa ni Kachawi kweli na baba yake nadhani ni msaidizi wa Lucifer mwenyewe, asije akanifanya mbaya bure! Basi najikaza kiume hivyo hivyo
Pole zake hiyo jamaa, Kukopa si mbaya tatizo nidhamu ya kukopa ndiyo tatizoHuu mkasa nilishautoaga humu, sio mbaya nikirudia. Okay nitaelezea in first person view.
Mwaka 2011, nilikuwa nimeacha kazi serikalini, nikaamua kuanza biashara ndogo ndogo kwani zililipa kuliko mshahara wa kazini. Hapa nilikuwa na girlfriend ambae nilimtambulisha nyumbani na kwao pia walinijua. Mimi na huyu gf wangu tulifungua kampuni moja, nitaaiita Xcorp. Gf wangu yeye alikuwa muajiriwa wa serikali(mwanasheria), kwahiyo alikuwa vizuri in terms of lifestyle. Basi tukaamua kuexpand business, tuliplan kujenga kumbi nne ambazo zitakuwa za kisasa... Tuliplan kuweka swimming pool, malls humo humo. Ilitakiwa 1bil. Tukasema we can make it. Wakati naendelea na vibiashara vidogo vidogo vya kwenda China, rafiki yangu wa kike akanitambulisha kwa rafiki yake. Nae alikuwa mdada. Huyu dada nitamuita Grace. Grace alionekana ni mtu mwenyewe mafanikio sana. Aliishi Masaki nyumba ina swimming pool, na counter, pia alikuwa akitumia magari ya bei; BMW X5, Hilux new model, Brevis, Mark X na Range Rover. Kwa kweli enzi hizo Mark X na Brevis zilikuwa za kuhesabu barabarani. Huyu dada akaniambia yeye ni mfanyakazi wa kampuni ya mtandao mkubwa hapa Tz. Basi akaniambia wanaproject lakini inaitaji investors. Hii project ilikuwa kama ndoto ya mchana kwani ndani ya mwaka mmoja ningepata 1B.
Nikamueleza gf, akanielewa. Basi mwanzo tukawekeza 40m tu. Kweli ndani ya wiki mbili tulipata faida ya 40m!!! So tukarudishiwa 80m!!! Aisee nikapiga picha, ile biashara ya China bora niiache kwanza mikiki mikiki ya bandarini na mzigo hapa Tz unakaa miezi miwili plus kuja kuisha na faida ni kama 40% tu. Basi Grace akanichombeza ningeongeza hela ya kuwekeza to 400m. Ningepata 800m faida na ningekaribia goal ya 1b. Nikauza viwanja vyote, magari yote(nilikuwa nayo 8) sikubakiza hata moja, mtaji wa China wote nikakusanya. Nikawa na kama 230m. Nikamuomba Gf aniongezee, akagoma, akaingiza maswala ya kwamba mimi natembea na Grace(hii story nyingine) ila sio kweli. Baadae Gf akaniambia kwanini usiombe mkopo kwa nyumba yako. Duh nikasema poa. Gf ndio alikuwa na connection na watu wa benki basi tukaomba mkopo kwa kutumia kampuni yetu, nikaweka nyumba dhamana. Hapa ndipo natamani ningerudisha siku nyuma.
Wiki ambayo mkopo ulikuwa unatakiwa utoke sikupigiwa wala nini. Nikakaa kimya. Wiki ya pili nikaenda ile benki. Wakaniambia mbona ulikuja kuchukua na ukasign kabisa. Duh nikaenda kuangalia, signature sio yangu, na hela kweli zimeingia, lakini ajabu zimeingia kwenye account ya Gf. Nikampigia hapo hapo. Nilimuwakia sana. Akaniambia hela alishampa Grace 400m. Mkopo tulipata 156m, ilibidi turudishe 200m in 1 year. Dadeki nikaona huu utani. Nikamfata Gf home tulifokeana sana(advice usioe/usiolewe na mwanasheria kama hujui ubishi) nikatulia. Akaingiza mambo ya mimi kutoka na Grace, mara haniamini. Ajabu ni kwamba asilimia kubwa ya vitu at risk ni vyangu yeye kwenye biashara ya China alinipaga kama 30m tu. Kwasababu nilimpenda nikakausha. Grace wiki ya kwanza tuliongea freshi tu, ila baada ya wiki akapotea.
Duh wasiwasi ukanijia. Ila nikasema tusubiri ule muda aliosema hela zitarudi. Muda ukapita Grace hatujui alipo. Gf akanigeuzia kibao mimi. Mara mimi ndio nilimtambulisha kwake. Basi nikamfata yule dada aliyenitambulisha. Akaniambia yeye hayupo karibu nae. Aisee nilitamani kuua mtu. Yeye mwenyewe kweli alivyoniunganisha nae sikumueleza yaliyoendelea. Kwanza alikuwa hajui kama nafanya biashara na Grace. Kwenda kwake Grace nakuta kahama na nyumba ilikuwa ya kupanga sio yake. Magari ya kukodi, yeye alikuwa na BMW X5 tu. Nikaenda kampuni ya simu aliosema ni mfanyakazi, hajulikani!!! Nilikaa chini kwenye floor. Miezi ikapita.
Gf alivyoona nimeishiwa, akawa distant, mara hapokei simu. Matusi kwa wingi, baada ya muda akaniacha. Life lilikuwa gumu. Mwezi uliobidi turudishe mkopo ukaingia, sina mia. Ndugu ndio wananitumia hela ya kula. Siku mbili zinaweza pita nyumbani giza, sina hela ya LUKU. Mboga nzuri ilikuwa dagaa mchele. Grace hajulikani halipo. Basi nikaanza kumkazia Gf, kumtishia kuwa alifoji signature yangu. Basi akawa na uwoga nae akaanza kunisaidia kumtafuta Grace. Akafanikiwa, alimuweka Grace ndani kama wiki nzima kabla hajapata mdhamana. Nikaja kujua ukweli, kumbe Grace ni tapeli hata zile hela za mwanzo zilirudi kwasababu aliwachimba wengine. Kiukweli life lake ni show tu ya kuwateka watu. Basi tukambana, akatupa documents za nyumba yake moja. Akasema ndio alichonacho, BMW lake kuna victim mwingine alishalichukua na bado ana mdai Grace 40m. Therefore nae akagangania documents za nyumba. Tukaongea na polisi, maana Mimi nadai 400m mwenzangu 40m bora nipewe Mimi. Polisi wakasema twende court, mwenyewe sina hata mia. Na yule mdai mwingine yupo vizuri kifedha, as you all know bila hela mahakamani... Acha nisimalizie. Nikaongea na mdai, nikamwambia tuuze nyumba nitamlipa 40m alafu nitachukua iliyobaki. Akakubali ila yeye abaki na documents.
Mzaa. Nyumba haina hati, kwanza value 260m ya kwangu ilikuwa 516m. Kwasababu sina kitu nikakubaliana na hali halisi. Nyumba ya Grace ilikuwa haijamalizika, matengenezo kama 40m, ilikuwa golofa. Nyumba haikuuzika mwaka mzima. Baada ya muda wa kupiga stop order, benki wakapiga mnada nyumba yangu nikahamia ghetto. Nikaanza kupaona kuzimu aisee. Nikasema nisue benki maana walicheza mchezo na Gf, na hela sina za kupambana nao. Nikaona nikimtubua Gf nitajiharibia mwenyewe. Basi Grace tukaachana nae kwani na yeye kapigika mbaya.
Huu mwaka wa 5 tangu nyumba yangu iuzwe. Nakaa jumba amabalo mvua ikinyesha maji yanaingia godoro linaloa. Sina gari wala baiskeli. Nikiona mtu ana starlet namuona Mungu. Msosi nasaidiwa na ndugu. Bado nipo kwenye harakati za kutafuta mteja wa nyumba ya Grace hata kwa 150m nauza nianze upya.
Back to third person view. Gf ana life jingine na kidume mwingine, life is good. Ila Gf yupo hatarini, kwani soon TAKUKURU will be after her. Huu mkasa umemtokea ndugu yangu wa karibu sana. Siku anatimuliwa na polisi kwake alilala mpaka kwenye mchanga analia. Na nyumba yake mpaka leo wateja wanakuja na kuchomoa, haijauzwa. Mpaka watu wa benki wanaleta waganga wafanye manyanga. Nyumba imekaa haina watu mpaka walinzi wa benki wanapangisha vyumba vya ndani. Huyu ndugu yangu kakimbiwa na watu wengi wa karibu kwasababu wanajua kaishiwa. Anyway lesson learnt, Mimi namuomba Mungu aniepushe na haya. Bora niishi na salary au biashara ndogo kuliko kukopa. Ukikopa unakuwa mtumwa.
-callmeGhost
Asante mkuu,your advice will be considered...Kama huna usimamizi wa moja kwa moja baba hiyo pesa itapotea kopa mkopo wa muda mfupi kwanza at least 1yr ufanye hizo biashara ujue hasara na faida zake then next year uchukue pesa nzur uiboreshe hiyo business au uachane nayo
Trust me hutajuta
Ila mishahara wanaolipwa wachezaji hauna siri!hivi kwa nn?Ni siri kaka mshahara
Mishahara inajulikana haswa kada za serikali but kuuanika mitandaoni unaweza ukaonekana kama una kaakili ambacho hakijakaa vizuri.Ndivyo ilivyozoelekaIla mishahara wanaolipwa wachezaji hauna siri!hivi kwa nn?