Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Mbona mnanitisha wakuu nataka inivute mil 15 crdb then nikachukue nyumba kuna jamaa kafail kufanya mrejesho so ameona bora aniuzie mimi nyumba yake kuliko kupigwa mnada daa kanitia nyege kichizi nataka nivumilie ila niwe nishapata nyumba maana kujenga ni mbinde siku hizi
Niunganishe na huyo mtu mkuu hela ninayo
 
2013...naingia chuo..nakutana na boom....pesa nyingi ambayo sikuwahi kiishika kabla ya hapo....kwa mara ya kwanza akaunti yangu ikasoma 800,000/=....ukiongeza na vijisenti nilivyokuwa natafuta baada ya kumaliza form six akaunti ikasoma kama 1.2mil.....daaaaa.....nikaona sio mbaya nikianza kufanya biashara....basi nikaongea na mama yangu mdogo.....akanambia anaweza nisaidia....nikamtumia kama 400k....tukaongea tufanye biashara ya nguo ila baada ya kumaliza chuo nahitaji biashara yangu nisimamie mwenyewe au anipe pesa na faida kiasi iliyopatikana ili nikaendelee na biashara zingine....basi kila boom likitoka namtumia like 250k.. Wakati mwingine 300k....kwa miaka 4....nilipo maliza chuo sikukuta hata semti tano.....seriously.... Usimwamini ndugu kwenye biashara yako..
 
Mimi nilikopa mwaka jana NMB Mi. 9 kwa miaka mitano. Nikachukua pikipiki mbili. Moja ya bodaboda na nyingine ya kwangu kutembelea. Mil.4 nikachukua kiwanja na shamba kwa ajili ya kilimo. Laki 5 nikalimisha shmaba na kupanda mahindi na laki tano nikafanyia mambo yangu menginene. Mshahara nikabaki 247,000

Matokeo yake;

i)Bodaboda ilidumu miezi sita ikaibiwa.
ii) mahindi sikupata hata nusu gunia,kwa sababu ya ukame.
iii)mipango yangu ilikuwa mwaka huu nioe kama mambo yangeenda vizur kinyume chake nimeshindwa,mchumba wangu alipoona hali imekuwa tete akaanza visa kumbe kashaanza mahusiano na mwanaume mwingine,nikabaki mimi kama mimi.
iv)Baada ya bodi ya mkopo kuanza kukata 15% nikaanza kuchukua 197,000/= kwa mwezi
v) kwa sasa siwezi saidia chochote kwa mama na ndugu zangu kibaya zaidi mdogo wangu kachaguliwa chuo cha afya diploma ada mil.2. 5 sijaweza kumpa hata mia.

Sina bahati kabisa
Maisha siyo barabara iliyonyooka na kumbuka siku hazigandi yatapita kaza buti baba, ndo kwanza alfajiri.
 
Hizo akili ni zako? Unachukua milioni 4.5 unamkabidhi dada? Hujaiona biashara yake ila kakuhadithia tu. Laiti ungekuwa Mchaga ungeenda mpaka shamba ukafunge mzigo, uupeleke sokoni ukalijue soko faida na hasara uzijue. Pole lakini umejifunza kwa gharama kubwa sana kutokumuamini mtu yoyote ktk pesa kirahisi.
 
Mwaka jana nilikopa ml kadhaa na rafiki yangu, nia yetu tukalime matikiti, tulifanya utafiti kwanza na kutafuta shamba la kukodi ili tuanze kilimo. Dhamana niliweka ofisi niliyokuwa nafanyia kazi. Tukaenda kukopa kwa makubaliano kwamba tutashea rejesho nusu kwa nusu maana biashara inakuwa yetu wote, tukishavuna tutagawana faida.

Tulipata mkopo Access kwa muda wa miezi 9, tukalima tukafunga mabomba shambani maana kule maji ni ya dawasco, tukapanda matikiti vizuri, ilikuwa heka 2. Yakaota yakastawi vizuri na kuzaa yakazaa, kasheshe yalipofikia kukomaa maji yakakatika wiki mbili [emoji29] matikiti yakakosa maji, yakaungua jua na mwisho yakaoza doh! Hatukupata hata la kuonja yaani, heka mbili zote yameoza. Kuona hvyo rafiki yangu akanikimbia kagoma kulipa rejesho, hapo mkopo bado mmbichi ndo kwanza miezi mi3, we nilijuta, niliishi maisha magumu hakuna mfano. Miezi 6 ya kudaiwa niliona kama nipo jela aisee ila Mungu mkubwa nilifanikiw kumaliza deni na maisha yanaendelea. Urafiki ndo ulifikia tamati tena.
 
Back
Top Bottom