Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

This thread deserve An Oscar
mtena

pole sana mkuu
Acha Bob niliishi kama shetani kunywa soda ikawa ni anasa bi mkubwa nkawa hata sipokei simu zake coz alikuwa ananiambia kama sina pesa bora nirudi nyumban tukalime wote
Kuliko kila siku anabipigia simu nalia lia tu kuwa sina pesa na huku mm ni mfanyakazi
 
Uzi mzuri ila unantisha pia...maana panapo majaaliwa nategemea kuchukua mkopo next year,kwa ajili ya kujenga na kuanzisha biashara...

Wadau njooni mtiririke mauzoefu zaidi ili tujifunze kutokana na makosa na mafanikio pia.
Kama huna usimamizi wa moja kwa moja baba hiyo pesa itapotea kopa mkopo wa muda mfupi kwanza at least 1yr ufanye hizo biashara ujue hasara na faida zake then next year uchukue pesa nzur uiboreshe hiyo business au uachane nayo

Trust me hutajuta
 
Huu mkasa nilishautoaga humu, sio mbaya nikirudia. Okay nitaelezea in first person view.

Mwaka 2011, nilikuwa nimeacha kazi serikalini, nikaamua kuanza biashara ndogo ndogo kwani zililipa kuliko mshahara wa kazini. Hapa nilikuwa na girlfriend ambae nilimtambulisha nyumbani na kwao pia walinijua. Mimi na huyu gf wangu tulifungua kampuni moja, nitaaiita Xcorp. Gf wangu yeye alikuwa muajiriwa wa serikali(mwanasheria), kwahiyo alikuwa vizuri in terms of lifestyle. Basi tukaamua kuexpand business, tuliplan kujenga kumbi nne ambazo zitakuwa za kisasa... Tuliplan kuweka swimming pool, malls humo humo. Ilitakiwa 1bil. Tukasema we can make it. Wakati naendelea na vibiashara vidogo vidogo vya kwenda China, rafiki yangu wa kike akanitambulisha kwa rafiki yake. Nae alikuwa mdada. Huyu dada nitamuita Grace. Grace alionekana ni mtu mwenyewe mafanikio sana. Aliishi Masaki nyumba ina swimming pool, na counter, pia alikuwa akitumia magari ya bei; BMW X5, Hilux new model, Brevis, Mark X na Range Rover. Kwa kweli enzi hizo Mark X na Brevis zilikuwa za kuhesabu barabarani. Huyu dada akaniambia yeye ni mfanyakazi wa kampuni ya mtandao mkubwa hapa Tz. Basi akaniambia wanaproject lakini inaitaji investors. Hii project ilikuwa kama ndoto ya mchana kwani ndani ya mwaka mmoja ningepata 1B.

Nikamueleza gf, akanielewa. Basi mwanzo tukawekeza 40m tu. Kweli ndani ya wiki mbili tulipata faida ya 40m!!! So tukarudishiwa 80m!!! Aisee nikapiga picha, ile biashara ya China bora niiache kwanza mikiki mikiki ya bandarini na mzigo hapa Tz unakaa miezi miwili plus kuja kuisha na faida ni kama 40% tu. Basi Grace akanichombeza ningeongeza hela ya kuwekeza to 400m. Ningepata 800m faida na ningekaribia goal ya 1b. Nikauza viwanja vyote, magari yote(nilikuwa nayo 8) sikubakiza hata moja, mtaji wa China wote nikakusanya. Nikawa na kama 230m. Nikamuomba Gf aniongezee, akagoma, akaingiza maswala ya kwamba mimi natembea na Grace(hii story nyingine) ila sio kweli. Baadae Gf akaniambia kwanini usiombe mkopo kwa nyumba yako. Duh nikasema poa. Gf ndio alikuwa na connection na watu wa benki basi tukaomba mkopo kwa kutumia kampuni yetu, nikaweka nyumba dhamana. Hapa ndipo natamani ningerudisha siku nyuma.

Wiki ambayo mkopo ulikuwa unatakiwa utoke sikupigiwa wala nini. Nikakaa kimya. Wiki ya pili nikaenda ile benki. Wakaniambia mbona ulikuja kuchukua na ukasign kabisa. Duh nikaenda kuangalia, signature sio yangu, na hela kweli zimeingia, lakini ajabu zimeingia kwenye account ya Gf. Nikampigia hapo hapo. Nilimuwakia sana. Akaniambia hela alishampa Grace 400m. Mkopo tulipata 156m, ilibidi turudishe 200m in 1 year. Dadeki nikaona huu utani. Nikamfata Gf home tulifokeana sana(advice usioe/usiolewe na mwanasheria kama hujui ubishi) nikatulia. Akaingiza mambo ya mimi kutoka na Grace, mara haniamini. Ajabu ni kwamba asilimia kubwa ya vitu at risk ni vyangu yeye kwenye biashara ya China alinipaga kama 30m tu. Kwasababu nilimpenda nikakausha. Grace wiki ya kwanza tuliongea freshi tu, ila baada ya wiki akapotea.

Duh wasiwasi ukanijia. Ila nikasema tusubiri ule muda aliosema hela zitarudi. Muda ukapita Grace hatujui alipo. Gf akanigeuzia kibao mimi. Mara mimi ndio nilimtambulisha kwake. Basi nikamfata yule dada aliyenitambulisha. Akaniambia yeye hayupo karibu nae. Aisee nilitamani kuua mtu. Yeye mwenyewe kweli alivyoniunganisha nae sikumueleza yaliyoendelea. Kwanza alikuwa hajui kama nafanya biashara na Grace. Kwenda kwake Grace nakuta kahama na nyumba ilikuwa ya kupanga sio yake. Magari ya kukodi, yeye alikuwa na BMW X5 tu. Nikaenda kampuni ya simu aliosema ni mfanyakazi, hajulikani!!! Nilikaa chini kwenye floor. Miezi ikapita.

Gf alivyoona nimeishiwa, akawa distant, mara hapokei simu. Matusi kwa wingi, baada ya muda akaniacha. Life lilikuwa gumu. Mwezi uliobidi turudishe mkopo ukaingia, sina mia. Ndugu ndio wananitumia hela ya kula. Siku mbili zinaweza pita nyumbani giza, sina hela ya LUKU. Mboga nzuri ilikuwa dagaa mchele. Grace hajulikani halipo. Basi nikaanza kumkazia Gf, kumtishia kuwa alifoji signature yangu. Basi akawa na uwoga nae akaanza kunisaidia kumtafuta Grace. Akafanikiwa, alimuweka Grace ndani kama wiki nzima kabla hajapata mdhamana. Nikaja kujua ukweli, kumbe Grace ni tapeli hata zile hela za mwanzo zilirudi kwasababu aliwachimba wengine. Kiukweli life lake ni show tu ya kuwateka watu. Basi tukambana, akatupa documents za nyumba yake moja. Akasema ndio alichonacho, BMW lake kuna victim mwingine alishalichukua na bado ana mdai Grace 40m. Therefore nae akagangania documents za nyumba. Tukaongea na polisi, maana Mimi nadai 400m mwenzangu 40m bora nipewe Mimi. Polisi wakasema twende court, mwenyewe sina hata mia. Na yule mdai mwingine yupo vizuri kifedha, as you all know bila hela mahakamani... Acha nisimalizie. Nikaongea na mdai, nikamwambia tuuze nyumba nitamlipa 40m alafu nitachukua iliyobaki. Akakubali ila yeye abaki na documents.

Mzaa. Nyumba haina hati, kwanza value 260m ya kwangu ilikuwa 516m. Kwasababu sina kitu nikakubaliana na hali halisi. Nyumba ya Grace ilikuwa haijamalizika, matengenezo kama 40m, ilikuwa golofa. Nyumba haikuuzika mwaka mzima. Baada ya muda wa kupiga stop order, benki wakapiga mnada nyumba yangu nikahamia ghetto. Nikaanza kupaona kuzimu aisee. Nikasema nisue benki maana walicheza mchezo na Gf, na hela sina za kupambana nao. Nikaona nikimtubua Gf nitajiharibia mwenyewe. Basi Grace tukaachana nae kwani na yeye kapigika mbaya.

Huu mwaka wa 5 tangu nyumba yangu iuzwe. Nakaa jumba amabalo mvua ikinyesha maji yanaingia godoro linaloa. Sina gari wala baiskeli. Nikiona mtu ana starlet namuona Mungu. Msosi nasaidiwa na ndugu. Bado nipo kwenye harakati za kutafuta mteja wa nyumba ya Grace hata kwa 150m nauza nianze upya.

Back to third person view. Gf ana life jingine na kidume mwingine, life is good. Ila Gf yupo hatarini, kwani soon TAKUKURU will be after her. Huu mkasa umemtokea ndugu yangu wa karibu sana. Siku anatimuliwa na polisi kwake alilala mpaka kwenye mchanga analia. Na nyumba yake mpaka leo wateja wanakuja na kuchomoa, haijauzwa. Mpaka watu wa benki wanaleta waganga wafanye manyanga. Nyumba imekaa haina watu mpaka walinzi wa benki wanapangisha vyumba vya ndani. Huyu ndugu yangu kakimbiwa na watu wengi wa karibu kwasababu wanajua kaishiwa. Anyway lesson learnt, Mimi namuomba Mungu aniepushe na haya. Bora niishi na salary au biashara ndogo kuliko kukopa. Ukikopa unakuwa mtumwa.

-callmeGhost
 
Sitasahau siku nilipokuwa nalipa madeni kila mwez takribani milion 1 na laki 2 mpaka na lak 5,mchana kutwa nnalala kama mgonjwa yaani mawazo tele,mpaka nikahisi sasa nafirisika,yaani nilikuwa mchungu hatari,nikajipa moyo japo kiugumu ugumu,biashara nayo ikayumba nikatamani kuweka Nyumba yangu bond kwenye Benk yoyote au taasisi ya kifedha,lakini moyo ukawa unasita,nilikuwa na mdogo wangu wa kiume nnakaa naye na kunisaidia biashara,nashukuru kwa uvumilivu wake na ushauri pia,tukakubaliana tupambane tuwezavyo hata kama ni majani tutakula lakini tuhakikishe tumemaliza madeni ya Watu il tuwe huru,nikajiingiza kwenye kilimo cha viaz vitamu,nililima kama ekar 4,nikajua ntampata pesa,changamoto soko lake,nikakopa tena pesa ili nisafirishie mzgo kwenda Dar,wakati madeni ya kwanza yapo nalipa,kufika Dar soko la mabibo limetapika,marol kila muda yanaingia,nilichoka,gharama ya usafiri milion moja,mauzo aliyonipa dalal lak sita,madeni yakaongezeka,yule jamaa aliyenikopesha pesa alijuta,dalali amekula zake laki 5,hapo ndipo nilichukia madalal na kuona wamelaaniwa,ina maana kila gunia anakula elfu 5, kwa gunia mia,na mimi nilikuwa napigia kama m 2500000,niliondoka Dar bila chochote kununua,nikazidi kupambana mpaka nikafanikiwa kumaliza japo cha moto nilikiona,nilijifunza sababu ya kufilisika ni vitu viwil vikubw,MADENI NA MATUMIZI MAKUBWA.
 
Yan habar hiyo isikie tu kwa mwenko
Kina jamaa alikuwa ughaibuni huko akawa anamtumia baba yake pesa amjengee nyumba na Raman akamtumia
Jamaa akarudi kumuulisa mshua nyumba iko WAP hamna nyumba ndio kwanza amechimba msingi na alishatafuna kama 75mls.
Sasa kama ndio ww utamfunga mzee wako au
Jamaa ucku ule ule aligeuka wakaenda kulala kwa hitel keshokesho yake hao Japan na mkewe
Hhaah Daah kweli wazee wa kitanzania wamepinda....

Sidhani kama jamaa atakuja kanyaga tena tanzania...
 
Mimi nilikopa mwaka jana NMB Mi. 9 kwa miaka mitano. Nikachukua pikipiki mbili. Moja ya bodaboda na nyingine ya kwangu kutembelea. Mil.4 nikachukua kiwanja na shamba kwa ajili ya kilimo. Laki 5 nikalimisha shmaba na kupanda mahindi na laki tano nikafanyia mambo yangu menginene. Mshahara nikabaki 247,000

Matokeo yake;

i)Bodaboda ilidumu miezi sita ikaibiwa.
ii) mahindi sikupata hata nusu gunia,kwa sababu ya ukame.
iii)mipango yangu ilikuwa mwaka huu nioe kama mambo yangeenda vizur kinyume chake nimeshindwa,mchumba wangu alipoona hali imekuwa tete akaanza visa kumbe kashaanza mahusiano na mwanaume mwingine,nikabaki mimi kama mimi.
iv)Baada ya bodi ya mkopo kuanza kukata 15% nikaanza kuchukua 197,000/= kwa mwezi
v) kwa sasa siwezi saidia chochote kwa mama na ndugu zangu kibaya zaidi mdogo wangu kachaguliwa chuo cha afya diploma ada mil.2. 5 sijaweza kumpa hata mia.

Sina bahati kabisa
Usiseme hivyo dahhh !!
 
Uzi mzuri ila unantisha pia...maana panapo majaaliwa nategemea kuchukua mkopo next year,kwa ajili ya kujenga na kuanzisha biashara...

Wadau njooni mtiririke mauzoefu zaidi ili tujifunze kutokana na makosa na mafanikio pia.
Mkuu yaani pesa ya mkopo unataka ukajengee angalia usije anza kula mchanga kwako... Mimi Nakumbuka mother alikopaga kama milioni 20 kwa ajili ya biashara akachukua % fulani kumalizia nyumba muda wa marejesho ulivyofika nilimwonea huruma mpaka muda huu sitamani kuchukua mkopo sio kwa msoto ule alioupata mother.....

Bora nikope nikafungue Bar hata kama watu wasipokuja kunywa pombe kwa bar yangu nitazingonga mwenyewe mpaka ziishe.....

Mikopo Inarudisha nyuma maendeleo si mchezo.....
 
S
Mimi huu ni mwaka wa 6 hati yangu ina hama tu kutoka benki hii kwenda benki hii.

Mkopo huu wa mwisho nilichuwa 10,000,000 unanitesa sana, Kwani sehemu kubwa nilipeka kwenye ujenzi badala ya kwenye biashara lakini nashukuru Mungu hata hivyo nimehamia kwangu tangu Julay 2017. Ingawa sijamalizia vizuri hata hivyo nasave 250,000 ya kodi ya nyumba ya kila mwezi.

Shida sasa ni marejesho kurejesha 1m kila mwezi kwa kutumia biashara si mchezo kwani biashara zimeyumba sana.

Nimejikuta biashara moja inakufa na ya pili inawnda rijojo na hii ya tatu ninayoitegemea sana hali si nzuri sana lakini natumaini nitamaliza marejesho kwani yamebali mawili tu nikamilishe.

Ilifikia kipindi unazima simu nakumbuka siku moja nilichelewesha kama miezi 2 na nusu hivi kiafisa mikopo kikanipiga biti mbele za watu eti tutapiga mnada nyumba yako wee siku hiyo nilimuwakia kidogo nimpige makofi nilifoka pale mpaka wateja wakanisupport hata walipokuja polisi ingawa walinitoa lakini walinielewa. Siku hizi hata nikichelewa hawanipigii simu.

Kwa sisi wafanyabiashara hatuwezi kuendelea bila kokopa
Sisi ni mikopo mbele kwa mbele baba......
 
Huu mkasa nilishautoaga humu, sio mbaya nikirudia. Okay nitaelezea in first person view.

Mwaka 2011, nilikuwa nimeacha kazi serikalini, nikaamua kuanza biashara ndogo ndogo kwani zililipa kuliko mshahara wa kazini. Hapa nilikuwa na girlfriend ambae nilimtambulisha nyumbani na kwao pia walinijua. Mimi na huyu gf wangu tulifungua kampuni moja, nitaaiita Xcorp. Gf wangu yeye alikuwa muajiriwa wa serikali(mwanasheria), kwahiyo alikuwa vizuri in terms of lifestyle. Basi tukaamua kuexpand business, tuliplan kujenga kumbi nne ambazo zitakuwa za kisasa... Tuliplan kuweka swimming pool, malls humo humo. Ilitakiwa 1bil. Tukasema we can make it. Wakati naendelea na vibiashara vidogo vidogo vya kwenda China, rafiki yangu wa kike akanitambulisha kwa rafiki yake. Nae alikuwa mdada. Huyu dada nitamuita Grace. Grace alionekana ni mtu mwenyewe mafanikio sana. Aliishi Masaki nyumba ina swimming pool, na counter, pia alikuwa akitumia magari ya bei; BMW X5, Hilux new model, Brevis, Mark X na Range Rover. Kwa kweli enzi hizo Mark X na Brevis zilikuwa za kuhesabu barabarani. Huyu dada akaniambia yeye ni mfanyakazi wa kampuni ya mtandao mkubwa hapa Tz. Basi akaniambia wanaproject lakini inaitaji investors. Hii project ilikuwa kama ndoto ya mchana kwani ndani ya mwaka mmoja ningepata 1B.

Nikamueleza gf, akanielewa. Basi mwanzo tukawekeza 40m tu. Kweli ndani ya wiki mbili tulipata faida ya 40m!!! So tukarudishiwa 80m!!! Aisee nikapiga picha, ile biashara ya China bora niiache kwanza mikiki mikiki ya bandarini na mzigo hapa Tz unakaa miezi miwili plus kuja kuisha na faida ni kama 40% tu. Basi Grace akanichombeza ningeongeza hela ya kuwekeza to 400m. Ningepata 800m faida na ningekaribia goal ya 1b. Nikauza viwanja vyote, magari yote(nilikuwa nayo 8) sikubakiza hata moja, mtaji wa China wote nikakusanya. Nikawa na kama 230m. Nikamuomba Gf aniongezee, akagoma, akaingiza maswala ya kwamba mimi natembea na Grace(hii story nyingine) ila sio kweli. Baadae Gf akaniambia kwanini usiombe mkopo kwa nyumba yako. Duh nikasema poa. Gf ndio alikuwa na connection na watu wa benki basi tukaomba mkopo kwa kutumia kampuni yetu, nikaweka nyumba dhamana. Hapa ndipo natamani ningerudisha siku nyuma.

Wiki ambayo mkopo ulikuwa unatakiwa utoke sikupigiwa wala nini. Nikakaa kimya. Wiki ya pili nikaenda ile benki. Wakaniambia mbona ulikuja kuchukua na ukasign kabisa. Duh nikaenda kuangalia, signature sio yangu, na hela kweli zimeingia, lakini ajabu zimeingia kwenye account ya Gf. Nikampigia hapo hapo. Nilimuwakia sana. Akaniambia hela alishampa Grace 400m. Mkopo tulipata 156m, ilibidi turudishe 200m in 1 year. Dadeki nikaona huu utani. Nikamfata Gf home tulifokeana sana(advice usioe/usiolewe na mwanasheria kama hujui ubishi) nikatulia. Akaingiza mambo ya mimi kutoka na Grace, mara haniamini. Ajabu ni kwamba asilimia kubwa ya vitu at risk ni vyangu yeye kwenye biashara ya China alinipaga kama 30m tu. Kwasababu nilimpenda nikakausha. Grace wiki ya kwanza tuliongea freshi tu, ila baada ya wiki akapotea.

Duh wasiwasi ukanijia. Ila nikasema tusubiri ule muda aliosema hela zitarudi. Muda ukapita Grace hatujui alipo. Gf akanigeuzia kibao mimi. Mara mimi ndio nilimtambulisha kwake. Basi nikamfata yule dada aliyenitambulisha. Akaniambia yeye hayupo karibu nae. Aisee nilitamani kuua mtu. Yeye mwenyewe kweli alivyoniunganisha nae sikumueleza yaliyoendelea. Kwanza alikuwa hajui kama nafanya biashara na Grace. Kwenda kwake Grace nakuta kahama na nyumba ilikuwa ya kupanga sio yake. Magari ya kukodi, yeye alikuwa na BMW X5 tu. Nikaenda kampuni ya simu aliosema ni mfanyakazi, hajulikani!!! Nilikaa chini kwenye floor. Miezi ikapita.

Gf alivyoona nimeishiwa, akawa distant, mara hapokei simu. Matusi kwa wingi, baada ya muda akaniacha. Life lilikuwa gumu. Mwezi uliobidi turudishe mkopo ukaingia, sina mia. Ndugu ndio wananitumia hela ya kula. Siku mbili zinaweza pita nyumbani giza, sina hela ya LUKU. Mboga nzuri ilikuwa dagaa mchele. Grace hajulikani halipo. Basi nikaanza kumkazia Gf, kumtishia kuwa alifoji signature yangu. Basi akawa na uwoga nae akaanza kunisaidia kumtafuta Grace. Akafanikiwa, alimuweka Grace ndani kama wiki nzima kabla hajapata mdhamana. Nikaja kujua ukweli, kumbe Grace ni tapeli hata zile hela za mwanzo zilirudi kwasababu aliwachimba wengine. Kiukweli life lake ni show tu ya kuwateka watu. Basi tukambana, akatupa documents za nyumba yake moja. Akasema ndio alichonacho, BMW lake kuna victim mwingine alishalichukua na bado ana mdai Grace 40m. Therefore nae akagangania documents za nyumba. Tukaongea na polisi, maana Mimi nadai 400m mwenzangu 40m bora nipewe Mimi. Polisi wakasema twende court, mwenyewe sina hata mia. Na yule mdai mwingine yupo vizuri kifedha, as you all know bila hela mahakamani... Acha nisimalizie. Nikaongea na mdai, nikamwambia tuuze nyumba nitamlipa 40m alafu nitachukua iliyobaki. Akakubali ila yeye abaki na documents.

Mzaa. Nyumba haina hati, kwanza value 260m ya kwangu ilikuwa 516m. Kwasababu sina kitu nikakubaliana na hali halisi. Nyumba ya Grace ilikuwa haijamalizika, matengenezo kama 40m, ilikuwa golofa. Nyumba haikuuzika mwaka mzima. Baada ya muda wa kupiga stop order, benki wakapiga mnada nyumba yangu nikahamia ghetto. Nikaanza kupaona kuzimu aisee. Nikasema nisue benki maana walicheza mchezo na Gf, na hela sina za kupambana nao. Nikaona nikimtubua Gf nitajiharibia mwenyewe. Basi Grace tukaachana nae kwani na yeye kapigika mbaya.

Huu mwaka wa 5 tangu nyumba yangu iuzwe. Nakaa jumba amabalo mvua ikinyesha maji yanaingia godoro linaloa. Sina gari wala baiskeli. Nikiona mtu ana starlet namuona Mungu. Msosi nasaidiwa na ndugu. Bado nipo kwenye harakati za kutafuta mteja wa nyumba ya Grace hata kwa 150m nauza nianze upya.

Back to third person view. Gf ana life jingine na kidume mwingine, life is good. Ila Gf yupo hatarini, kwani soon TAKUKURU will be after her. Huu mkasa umemtokea ndugu yangu wa karibu sana. Siku anatimuliwa na polisi kwake alilala mpaka kwenye mchanga analia. Na nyumba yake mpaka leo wateja wanakuja na kuchomoa, haijauzwa. Mpaka watu wa benki wanaleta waganga wafanye manyanga. Nyumba imekaa haina watu mpaka walinzi wa benki wanapangisha vyumba vya ndani. Huyu ndugu yangu kakimbiwa na watu wengi wa karibu kwasababu wanajua kaishiwa. Anyway lesson learnt, Mimi namuomba Mungu aniepushe na haya. Bora niishi na salary au biashara ndogo kuliko kukopa. Ukikopa unakuwa mtumwa.

-callmeGhost
Pole sana ni dhahiri ulikuwa pazuri kibiashara ila tamaa ndiyo wa kutaka utajiri wa haraka ndiyo umekuharibia mambo yote,baada ya Grace kukuhadaa na kuuza mali zako zote il kupata mtaji wa milion mia nne mara mbili yake,zidi kumuomba Mungu kwani maisha ni changamoto na umejifunza vitu nasi pia kutokana makosa,muhimu uzima tu usikate tamaa zidi kupambana bado una nafas mkuu.

Sent from my TECNO H5 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom