Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duh ya alishindwa kujieleza ofisini labda angesaidiwaKuna jamaa m1 alichukua kama mkopo benki moja sijui kiasi gani. Ananunua kiwanja kibaha akajenga kufika katika linta hela ikakata. Akakosa hata hela ya kodi alipopanga cz makato yalikuwa makubwa hakubalikiwa na kiasi cha kumtosheleza na alikuwa ameoa. Kelele za mama mwenye nyumba ikabidi mkewe akasirike arudi kwao Moshi. Yeye ikabidi ahamie kibaha hivyo hivyo. Sasa balaa hata nauli ya kwenda kazini ilikuwa mtihani. Ikawa mtoro kazini. Anaenda Mara 1 au 2 kwa wiki kazini. Kesi za utoro zikazidi akasimamishwa kazi. Jamaa kapagawa. Maana hana kitu kabisa. Mkewe wameachana na naskia aeolewa na mtu mwingine. Naskia yuko bagamoyo analima vibarua.
Pole sana MkuuHuu mkasa nilishautoaga humu, sio mbaya nikirudia. Okay nitaelezea in first person view.
Mwaka 2011, nilikuwa nimeacha kazi serikalini, nikaamua kuanza biashara ndogo ndogo kwani zililipa kuliko mshahara wa kazini. Hapa nilikuwa na girlfriend ambae nilimtambulisha nyumbani na kwao pia walinijua. Mimi na huyu gf wangu tulifungua kampuni moja, nitaaiita Xcorp. Gf wangu yeye alikuwa muajiriwa wa serikali(mwanasheria), kwahiyo alikuwa vizuri in terms of lifestyle. Basi tukaamua kuexpand business, tuliplan kujenga kumbi nne ambazo zitakuwa za kisasa... Tuliplan kuweka swimming pool, malls humo humo. Ilitakiwa 1bil. Tukasema we can make it. Wakati naendelea na vibiashara vidogo vidogo vya kwenda China, rafiki yangu wa kike akanitambulisha kwa rafiki yake. Nae alikuwa mdada. Huyu dada nitamuita Grace. Grace alionekana ni mtu mwenyewe mafanikio sana. Aliishi Masaki nyumba ina swimming pool, na counter, pia alikuwa akitumia magari ya bei; BMW X5, Hilux new model, Brevis, Mark X na Range Rover. Kwa kweli enzi hizo Mark X na Brevis zilikuwa za kuhesabu barabarani. Huyu dada akaniambia yeye ni mfanyakazi wa kampuni ya mtandao mkubwa hapa Tz. Basi akaniambia wanaproject lakini inaitaji investors. Hii project ilikuwa kama ndoto ya mchana kwani ndani ya mwaka mmoja ningepata 1B.
Nikamueleza gf, akanielewa. Basi mwanzo tukawekeza 40m tu. Kweli ndani ya wiki mbili tulipata faida ya 40m!!! So tukarudishiwa 80m!!! Aisee nikapiga picha, ile biashara ya China bora niiache kwanza mikiki mikiki ya bandarini na mzigo hapa Tz unakaa miezi miwili plus kuja kuisha na faida ni kama 40% tu. Basi Grace akanichombeza ningeongeza hela ya kuwekeza to 400m. Ningepata 800m faida na ningekaribia goal ya 1b. Nikauza viwanja vyote, magari yote(nilikuwa nayo 8) sikubakiza hata moja, mtaji wa China wote nikakusanya. Nikawa na kama 230m. Nikamuomba Gf aniongezee, akagoma, akaingiza maswala ya kwamba mimi natembea na Grace(hii story nyingine) ila sio kweli. Baadae Gf akaniambia kwanini usiombe mkopo kwa nyumba yako. Duh nikasema poa. Gf ndio alikuwa na connection na watu wa benki basi tukaomba mkopo kwa kutumia kampuni yetu, nikaweka nyumba dhamana. Hapa ndipo natamani ningerudisha siku nyuma.
Wiki ambayo mkopo ulikuwa unatakiwa utoke sikupigiwa wala nini. Nikakaa kimya. Wiki ya pili nikaenda ile benki. Wakaniambia mbona ulikuja kuchukua na ukasign kabisa. Duh nikaenda kuangalia, signature sio yangu, na hela kweli zimeingia, lakini ajabu zimeingia kwenye account ya Gf. Nikampigia hapo hapo. Nilimuwakia sana. Akaniambia hela alishampa Grace 400m. Mkopo tulipata 156m, ilibidi turudishe 200m in 1 year. Dadeki nikaona huu utani. Nikamfata Gf home tulifokeana sana(advice usioe/usiolewe na mwanasheria kama hujui ubishi) nikatulia. Akaingiza mambo ya mimi kutoka na Grace, mara haniamini. Ajabu ni kwamba asilimia kubwa ya vitu at risk ni vyangu yeye kwenye biashara ya China alinipaga kama 30m tu. Kwasababu nilimpenda nikakausha. Grace wiki ya kwanza tuliongea freshi tu, ila baada ya wiki akapotea.
Duh wasiwasi ukanijia. Ila nikasema tusubiri ule muda aliosema hela zitarudi. Muda ukapita Grace hatujui alipo. Gf akanigeuzia kibao mimi. Mara mimi ndio nilimtambulisha kwake. Basi nikamfata yule dada aliyenitambulisha. Akaniambia yeye hayupo karibu nae. Aisee nilitamani kuua mtu. Yeye mwenyewe kweli alivyoniunganisha nae sikumueleza yaliyoendelea. Kwanza alikuwa hajui kama nafanya biashara na Grace. Kwenda kwake Grace nakuta kahama na nyumba ilikuwa ya kupanga sio yake. Magari ya kukodi, yeye alikuwa na BMW X5 tu. Nikaenda kampuni ya simu aliosema ni mfanyakazi, hajulikani!!! Nilikaa chini kwenye floor. Miezi ikapita.
Gf alivyoona nimeishiwa, akawa distant, mara hapokei simu. Matusi kwa wingi, baada ya muda akaniacha. Life lilikuwa gumu. Mwezi uliobidi turudishe mkopo ukaingia, sina mia. Ndugu ndio wananitumia hela ya kula. Siku mbili zinaweza pita nyumbani giza, sina hela ya LUKU. Mboga nzuri ilikuwa dagaa mchele. Grace hajulikani halipo. Basi nikaanza kumkazia Gf, kumtishia kuwa alifoji signature yangu. Basi akawa na uwoga nae akaanza kunisaidia kumtafuta Grace. Akafanikiwa, alimuweka Grace ndani kama wiki nzima kabla hajapata mdhamana. Nikaja kujua ukweli, kumbe Grace ni tapeli hata zile hela za mwanzo zilirudi kwasababu aliwachimba wengine. Kiukweli life lake ni show tu ya kuwateka watu. Basi tukambana, akatupa documents za nyumba yake moja. Akasema ndio alichonacho, BMW lake kuna victim mwingine alishalichukua na bado ana mdai Grace 40m. Therefore nae akagangania documents za nyumba. Tukaongea na polisi, maana Mimi nadai 400m mwenzangu 40m bora nipewe Mimi. Polisi wakasema twende court, mwenyewe sina hata mia. Na yule mdai mwingine yupo vizuri kifedha, as you all know bila hela mahakamani... Acha nisimalizie. Nikaongea na mdai, nikamwambia tuuze nyumba nitamlipa 40m alafu nitachukua iliyobaki. Akakubali ila yeye abaki na documents.
Mzaa. Nyumba haina hati, kwanza value 260m ya kwangu ilikuwa 516m. Kwasababu sina kitu nikakubaliana na hali halisi. Nyumba ya Grace ilikuwa haijamalizika, matengenezo kama 40m, ilikuwa golofa. Nyumba haikuuzika mwaka mzima. Baada ya muda wa kupiga stop order, benki wakapiga mnada nyumba yangu nikahamia ghetto. Nikaanza kupaona kuzimu aisee. Nikasema nisue benki maana walicheza mchezo na Gf, na hela sina za kupambana nao. Nikaona nikimtubua Gf nitajiharibia mwenyewe. Basi Grace tukaachana nae kwani na yeye kapigika mbaya.
Huu mwaka wa 5 tangu nyumba yangu iuzwe. Nakaa jumba amabalo mvua ikinyesha maji yanaingia godoro linaloa. Sina gari wala baiskeli. Nikiona mtu ana starlet namuona Mungu. Msosi nasaidiwa na ndugu. Bado nipo kwenye harakati za kutafuta mteja wa nyumba ya Grace hata kwa 150m nauza nianze upya.
Back to third person view. Gf ana life jingine na kidume mwingine, life is good. Ila Gf yupo hatarini, kwani soon TAKUKURU will be after her. Huu mkasa umemtokea ndugu yangu wa karibu sana. Siku anatimuliwa na polisi kwake alilala mpaka kwenye mchanga analia. Na nyumba yake mpaka leo wateja wanakuja na kuchomoa, haijauzwa. Mpaka watu wa benki wanaleta waganga wafanye manyanga. Nyumba imekaa haina watu mpaka walinzi wa benki wanapangisha vyumba vya ndani. Huyu ndugu yangu kakimbiwa na watu wengi wa karibu kwasababu wanajua kaishiwa. Anyway lesson learnt, Mimi namuomba Mungu aniepushe na haya. Bora niishi na salary au biashara ndogo kuliko kukopa. Ukikopa unakuwa mtumwa.
-callmeGhost
Nmesoma uzi wote nimepata mwangaza mkubwa sanaPole sana Mkuu
Pole,wanaume wengine shida unapata mwanamke mpambanaji unadhulumuBaada ya kuchoka mishahara ya wahindi niliamua kujiajiri, nikawa nafanya biashara ndogondogo maisha yanaenda, nilikuwa nachukia Mikopo Sana, baada kuingia Kwenye biashara hukuhuku nikaona bora niingie Kwenye vikundi vya wanawake pamoja na Vicoba, nilikuwa na Vicoba vitatu na vikundi vinne vyote nilikuwa na vihudumia naweka tu Pesa sikopi.
Baada ya story za Mikopo za wanachama wenzangu Sasa na Mimi nikaona acha nikope bank nifungue biashara yangu moja ya uwakika nikakopa mil 10 marejesho miaka mitatu, Pesa yote niliingiza Kwenye mzunguko wa biashara mwaka wa kwanza marejesho yalienda Safi Kabisa mwaka wa pili matatizo yakaanza biashara zikafa nikabaki na shamba la korosho na msimu Kama mnavyojua mwaka kwa mwaka. ikawa ikifika tarehe ya rejesho nakopa Kwenye kikundi napeleka bank ikafika wakati vikoba vyote vitatu na vikundi mpaka wanachama wananidai Huku rejesho bado halijaisha la bank.
Nikavuna korosho nikasema Pesa Itanisaidia kupunguza madeni, mwanaume niliyekuwa naye akanishauri usilipe Pesa yote madeni zungushia biashara Huku unalipa madeni kidokidogo. Pesa nikampa mpenzi tuzungushe biashara akanidhulumu ikafika wakati sina hata mia mfukoni marafiki wote wamenikimbia bank nadaiwa, kila kona na madeni Sina kazi Sina biashara nilala ndani Kisa madeni ya watu ya riba mitaan sitaki kukumbuka nilisota nakusota. Ndugu Zangu ikabidi wajichangishe kulipa Mkopo WA bank iliyobaki maana ilibaki miez michache niliiweka dhamana viwanja vyangu viwili. Wakaona bora wanisaidie kuliko vipigwe mnada wakati nilibakisha kidogo.
Hii Mikopo mingine ya vikundi, vikoba na mitaani watu walinidai mpaka walikaa kimya na kuchoka maana Sina kitu Niko mweupeeeee. Baada ya kuumalizika Mkopo WA bank nikauza kiwanja kimoja nikalipa lipa madeni ya mitaani nikabakiza Pesa kidogo nikaaza na moja biashara
Sasa hivi sitaki kusikia Mikopo, vikoba Wala vikundi maana kwa wanawake wengi humo Ndio Huwa Chanzo cha matatizo na wahanga ni wengi maana humo watu wana ushawishi wa ajabu, Kama Sina najua Sina ila Sina Deni na mtu kuliko huna alafu udaiwe utatamani ufe kwa muda. Mikopo inaumiza .
What a life story..kama muvi manHuu mkasa nilishautoaga humu, sio mbaya nikirudia. Okay nitaelezea in first person view.
Mwaka 2011, nilikuwa nimeacha kazi serikalini, nikaamua kuanza biashara ndogo ndogo kwani zililipa kuliko mshahara wa kazini. Hapa nilikuwa na girlfriend ambae nilimtambulisha nyumbani na kwao pia walinijua. Mimi na huyu gf wangu tulifungua kampuni moja, nitaaiita Xcorp. Gf wangu yeye alikuwa muajiriwa wa serikali(mwanasheria), kwahiyo alikuwa vizuri in terms of lifestyle. Basi tukaamua kuexpand business, tuliplan kujenga kumbi nne ambazo zitakuwa za kisasa... Tuliplan kuweka swimming pool, malls humo humo. Ilitakiwa 1bil. Tukasema we can make it. Wakati naendelea na vibiashara vidogo vidogo vya kwenda China, rafiki yangu wa kike akanitambulisha kwa rafiki yake. Nae alikuwa mdada. Huyu dada nitamuita Grace. Grace alionekana ni mtu mwenyewe mafanikio sana. Aliishi Masaki nyumba ina swimming pool, na counter, pia alikuwa akitumia magari ya bei; BMW X5, Hilux new model, Brevis, Mark X na Range Rover. Kwa kweli enzi hizo Mark X na Brevis zilikuwa za kuhesabu barabarani. Huyu dada akaniambia yeye ni mfanyakazi wa kampuni ya mtandao mkubwa hapa Tz. Basi akaniambia wanaproject lakini inaitaji investors. Hii project ilikuwa kama ndoto ya mchana kwani ndani ya mwaka mmoja ningepata 1B.
Nikamueleza gf, akanielewa. Basi mwanzo tukawekeza 40m tu. Kweli ndani ya wiki mbili tulipata faida ya 40m!!! So tukarudishiwa 80m!!! Aisee nikapiga picha, ile biashara ya China bora niiache kwanza mikiki mikiki ya bandarini na mzigo hapa Tz unakaa miezi miwili plus kuja kuisha na faida ni kama 40% tu. Basi Grace akanichombeza ningeongeza hela ya kuwekeza to 400m. Ningepata 800m faida na ningekaribia goal ya 1b. Nikauza viwanja vyote, magari yote(nilikuwa nayo 8) sikubakiza hata moja, mtaji wa China wote nikakusanya. Nikawa na kama 230m. Nikamuomba Gf aniongezee, akagoma, akaingiza maswala ya kwamba mimi natembea na Grace(hii story nyingine) ila sio kweli. Baadae Gf akaniambia kwanini usiombe mkopo kwa nyumba yako. Duh nikasema poa. Gf ndio alikuwa na connection na watu wa benki basi tukaomba mkopo kwa kutumia kampuni yetu, nikaweka nyumba dhamana. Hapa ndipo natamani ningerudisha siku nyuma.
Wiki ambayo mkopo ulikuwa unatakiwa utoke sikupigiwa wala nini. Nikakaa kimya. Wiki ya pili nikaenda ile benki. Wakaniambia mbona ulikuja kuchukua na ukasign kabisa. Duh nikaenda kuangalia, signature sio yangu, na hela kweli zimeingia, lakini ajabu zimeingia kwenye account ya Gf. Nikampigia hapo hapo. Nilimuwakia sana. Akaniambia hela alishampa Grace 400m. Mkopo tulipata 156m, ilibidi turudishe 200m in 1 year. Dadeki nikaona huu utani. Nikamfata Gf home tulifokeana sana(advice usioe/usiolewe na mwanasheria kama hujui ubishi) nikatulia. Akaingiza mambo ya mimi kutoka na Grace, mara haniamini. Ajabu ni kwamba asilimia kubwa ya vitu at risk ni vyangu yeye kwenye biashara ya China alinipaga kama 30m tu. Kwasababu nilimpenda nikakausha. Grace wiki ya kwanza tuliongea freshi tu, ila baada ya wiki akapotea.
Duh wasiwasi ukanijia. Ila nikasema tusubiri ule muda aliosema hela zitarudi. Muda ukapita Grace hatujui alipo. Gf akanigeuzia kibao mimi. Mara mimi ndio nilimtambulisha kwake. Basi nikamfata yule dada aliyenitambulisha. Akaniambia yeye hayupo karibu nae. Aisee nilitamani kuua mtu. Yeye mwenyewe kweli alivyoniunganisha nae sikumueleza yaliyoendelea. Kwanza alikuwa hajui kama nafanya biashara na Grace. Kwenda kwake Grace nakuta kahama na nyumba ilikuwa ya kupanga sio yake. Magari ya kukodi, yeye alikuwa na BMW X5 tu. Nikaenda kampuni ya simu aliosema ni mfanyakazi, hajulikani!!! Nilikaa chini kwenye floor. Miezi ikapita.
Gf alivyoona nimeishiwa, akawa distant, mara hapokei simu. Matusi kwa wingi, baada ya muda akaniacha. Life lilikuwa gumu. Mwezi uliobidi turudishe mkopo ukaingia, sina mia. Ndugu ndio wananitumia hela ya kula. Siku mbili zinaweza pita nyumbani giza, sina hela ya LUKU. Mboga nzuri ilikuwa dagaa mchele. Grace hajulikani halipo. Basi nikaanza kumkazia Gf, kumtishia kuwa alifoji signature yangu. Basi akawa na uwoga nae akaanza kunisaidia kumtafuta Grace. Akafanikiwa, alimuweka Grace ndani kama wiki nzima kabla hajapata mdhamana. Nikaja kujua ukweli, kumbe Grace ni tapeli hata zile hela za mwanzo zilirudi kwasababu aliwachimba wengine. Kiukweli life lake ni show tu ya kuwateka watu. Basi tukambana, akatupa documents za nyumba yake moja. Akasema ndio alichonacho, BMW lake kuna victim mwingine alishalichukua na bado ana mdai Grace 40m. Therefore nae akagangania documents za nyumba. Tukaongea na polisi, maana Mimi nadai 400m mwenzangu 40m bora nipewe Mimi. Polisi wakasema twende court, mwenyewe sina hata mia. Na yule mdai mwingine yupo vizuri kifedha, as you all know bila hela mahakamani... Acha nisimalizie. Nikaongea na mdai, nikamwambia tuuze nyumba nitamlipa 40m alafu nitachukua iliyobaki. Akakubali ila yeye abaki na documents.
Mzaa. Nyumba haina hati, kwanza value 260m ya kwangu ilikuwa 516m. Kwasababu sina kitu nikakubaliana na hali halisi. Nyumba ya Grace ilikuwa haijamalizika, matengenezo kama 40m, ilikuwa golofa. Nyumba haikuuzika mwaka mzima. Baada ya muda wa kupiga stop order, benki wakapiga mnada nyumba yangu nikahamia ghetto. Nikaanza kupaona kuzimu aisee. Nikasema nisue benki maana walicheza mchezo na Gf, na hela sina za kupambana nao. Nikaona nikimtubua Gf nitajiharibia mwenyewe. Basi Grace tukaachana nae kwani na yeye kapigika mbaya.
Huu mwaka wa 5 tangu nyumba yangu iuzwe. Nakaa jumba amabalo mvua ikinyesha maji yanaingia godoro linaloa. Sina gari wala baiskeli. Nikiona mtu ana starlet namuona Mungu. Msosi nasaidiwa na ndugu. Bado nipo kwenye harakati za kutafuta mteja wa nyumba ya Grace hata kwa 150m nauza nianze upya.
Back to third person view. Gf ana life jingine na kidume mwingine, life is good. Ila Gf yupo hatarini, kwani soon TAKUKURU will be after her. Huu mkasa umemtokea ndugu yangu wa karibu sana. Siku anatimuliwa na polisi kwake alilala mpaka kwenye mchanga analia. Na nyumba yake mpaka leo wateja wanakuja na kuchomoa, haijauzwa. Mpaka watu wa benki wanaleta waganga wafanye manyanga. Nyumba imekaa haina watu mpaka walinzi wa benki wanapangisha vyumba vya ndani. Huyu ndugu yangu kakimbiwa na watu wengi wa karibu kwasababu wanajua kaishiwa. Anyway lesson learnt, Mimi namuomba Mungu aniepushe na haya. Bora niishi na salary au biashara ndogo kuliko kukopa. Ukikopa unakuwa mtumwa.
-callmeGhost
Hilo gari linakuingizia? Namaanisha ni la biashara? Una chanzo kingine cha mapato tofauti na hiyo kazi yako? Kama majibu ni hapana kati ya maswali hayo mawili nakushauri usichukue.Hebu mtushauri na sisi hatujawahi kukopa... Nna mpango wa kukopa 6m niongezee nivute ka gari maana kazini mbali kidogo...kwa take home ya 800k.
Je mnanishauri vipi hapo.?
Oh majibu ni hapana..nilitaka ya kwenda nayo kazini tu.Hilo gari linakuingizia? Namaanisha ni la biashara? Una chanzo kingine cha mapato tofauti na hiyo kazi yako? Kama majibu ni hapana kati ya maswali hayo mawili nakushauri usichukue.
Hebu mtushauri na sisi hatujawahi kukopa... Nna mpango wa kukopa 6m niongezee nivute ka gari maana kazini mbali kidogo...kwa take home ya 800k.
Je mnanishauri vipi hapo.?
Naassume labda utakatwa miaka 3 kwa asilimia 18 ya riba ambayo makadirio yatakuwa kama 7,080,000 ambayo utakatwa kama 197,000 kwa mwezi hivi..Hebu mtushauri na sisi hatujawahi kukopa... Nna mpango wa kukopa 6m niongezee nivute ka gari maana kazini mbali kidogo...kwa take home ya 800k.
Je mnanishauri vipi hapo.?
BalaaNaassume labda utakatwa miaka 3 kwa asilimia 18 ya riba ambayo makadirio yatakuwa kama 7,080,000 ambayo utakatwa kama 197,000 kwa mwezi hivi..
1. Ukikopa kiasi fulani hutokipata exactly hichohicho hivyo hapo toa kama laki 3 watakupa 5.7
2. Take home 800,000-197,000=603,000 .. huu utakuwa mshahara wako kwa miaka mitatu kama hutopanda daraja au kukosa bonuses pia kama hutokuwa na jinamizi la HESLB
3. Gari itakudai regular services kila baada ya km's kadhaa, mafuta, FINE ZA TRAFIKI za halali na za kubambikiwa, malipo ya bima, na ada nyinginezo..sijui kuhusu malipo ya parking ( HIZI ADDITIONAL EXPENSES ZOTE ZINAINGIA KWENYE ALBAKI YA MSHAHARA WAKO WA 603,000..
4. jumlisha matumizi yako ya sasa kabla ya mkopo..kama kodi,umeme,maji,msosi,mawasiliano n.k
* usipojichanga vizuri kimahesabu uchungu wa makato utakufanya uichukie kazi ..