Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Duh ya alishindwa kujieleza ofisini labda angesaidiwa
 
Financial literacy ni jambo muhimu sana. Mikopo ni mitamu asikwambie mtu, ila kulipa ni kuchungu kupita maelezo.

Kuna mambo mengi sana ya kuangalia ili usije kulia. Ni mkopo wa kiasi gani? Unarudisha kwa muda gani? Riba yake ni kiasi gani? Ni riba ya aina gani?

Vijana wengi sana wanaumizwa ni mikopo hasa hasa ya magari. Unakuta kijana kachukua mkopo 12m, interest 24% per annum. Mkopo wa miaka 3. Wengi hawapigi hesabu kujua ni kiasi gani watalipa mwishoni, kila mwezi etc. Mkopo kama huu, mwishoni mtu atalipa jumla karibu 20ml, by that time ki Alteza kimeshakufa na kimemtia gharama za kutosha.

Mkopo unahitaji umakini mkubwa, usijekuta unalia.
 
Thanks God,nimepitia comments zooteee.....nimejifunza mengi sana ingawa na mimi ni victim wa mkopo japokuwa mkopo wangu niliufanyia kitu cha maana na kinaonekana na sijutiii,ingawa naugulia maumivu ya kurejesha bado m3 tu ambazo naweza kuwalipakwa pamoja but naona km ni undezi acha wakate kwenye hako kamshahara...
 
Pole sana Mkuu
 
Pole sana Mkuu
Nmesoma uzi wote nimepata mwangaza mkubwa sana


Kuna Mkufunzi mmoja chuo fulani akati napita pita alisemaga "Ukiwa unafanya biashara ina mkopo ndani yake, unakuwa hauna tofauti na aliyeajiriwa" Pia akendelea kusema "Mkopo kutoka mabenki ya Tanzania ni sawa na ule utumwa wawaarabu" akasema TUJITAHIDI kusave kwa ajili ya uwekezaji kwenye kitu chochote kile katika maisha yetu.


Yote ya yote kwa jamii yetu ya Kitanzania kuhifadhi kwa ajili ya kuwekeza kuna ugumu fulani hivi, hvo bas mkopo ndo inakuwa kimbilio letu

Cha mhimu tuwe makini sana na mikopo, tuielekeze katika kazi iliyo kusudiwa,
Pia serekali yetu kupitia BOT ingeliangalia suala la riba kwa umakin zaid maana inaumiza sana.
 
Pole,wanaume wengine shida unapata mwanamke mpambanaji unadhulumu
 
What a life story..kama muvi man
 
Hebu mtushauri na sisi hatujawahi kukopa... Nna mpango wa kukopa 6m niongezee nivute ka gari maana kazini mbali kidogo...kwa take home ya 800k.

Je mnanishauri vipi hapo.?
Hilo gari linakuingizia? Namaanisha ni la biashara? Una chanzo kingine cha mapato tofauti na hiyo kazi yako? Kama majibu ni hapana kati ya maswali hayo mawili nakushauri usichukue.
 
Hebu mtushauri na sisi hatujawahi kukopa... Nna mpango wa kukopa 6m niongezee nivute ka gari maana kazini mbali kidogo...kwa take home ya 800k.

Je mnanishauri vipi hapo.?
Naassume labda utakatwa miaka 3 kwa asilimia 18 ya riba ambayo makadirio yatakuwa kama 7,080,000 ambayo utakatwa kama 197,000 kwa mwezi hivi..
1. Ukikopa kiasi fulani hutokipata exactly hichohicho hivyo hapo toa kama laki 3 watakupa 5.7

2. Take home 800,000-197,000=603,000 .. huu utakuwa mshahara wako kwa miaka mitatu kama hutopanda daraja au kukosa bonuses pia kama hutokuwa na jinamizi la HESLB

3. Gari itakudai regular services kila baada ya km's kadhaa, mafuta, FINE ZA TRAFIKI za halali na za kubambikiwa, malipo ya bima, na ada nyinginezo..sijui kuhusu malipo ya parking ( HIZI ADDITIONAL EXPENSES ZOTE ZINAINGIA KWENYE ALBAKI YA MSHAHARA WAKO WA 603,000..

4. jumlisha matumizi yako ya sasa kabla ya mkopo..kama kodi,umeme,maji,msosi,mawasiliano n.k

* usipojichanga vizuri kimahesabu uchungu wa makato utakufanya uichukie kazi ..
 
Balaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…