Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Dah hii hatari
Habar wapendwa humu JF

Bila kupoteza muda katika pulukushani za maisha kuwa magumu kuna wakati unaona the only solutions ni kuchukua mkopo katika taasisi za fedha mbalimbali ili kufungua ofisi nyingine itakayokuingizia kipato zaidi.

Ila cha kushangaza sasa unakuta tunaangukia pua na maisha kuwa tete zaidi ya hapo nyuma ilivyokuwa.

Mfano ni mimi; 2013 nilikopa 5 milions kwenye benki ya NMB kwa muda wa miaka 4 ambapo nilipanga kufungua biashra zangu mjini ili sister angu ndio azisimamie huko town basi nikaongea nae akanipa michongo yake ya biashara za mahindi zinavyomlipa anatoa mahindi Dodoma anapeleka Dar.

Akaniambia mimi nitakuwa napata laki 300000 kila atakapouza mzigo at the same time my capital remains costant. Mimi nikachukulia kama biashara ndio hivyo basi nitatengeneza pesa ndefu ndani ya muda mfupi sababu ndani ya mwezi anaenda kufunga Mzigo Mara 3.

Nikamtumia 4.5 milions kwa akaunti na ile laki tano kama kawa nikaitia kibiriti na Toto's za mjini nkajua after 1 week ntaanza kupokea pesa zangu za faida. Hapo salary nlikuwa napokea 190000 net baada ya makato yote.

Kumbe nae sister ndio kawa tycoon wa mjini anazitumbua pesa tu na vibwana vyake mpaka na kuja kumpigia sim vipi mbona kimya hunitumii ile pesa yani amelewa haezi hata kuongea.

Nikampigia kesho yake eti akaniambia aliibiwa pesa yote na hapo alipo amebakiwa na laki 3 tu na ndio anataka alipe kodi ili asifukuzwe kwenye chumba alichopanga. Nilikaaa chini bado nusu nilie ila nikajikaza kiume namshukuru Mungu nlikuwa sina mke wala mtoto.

Maisha yakawa magumu zaidi loan board walipoanza kunikata nikawa sasa kutoka 190000 nkawa napokea salary 135000 na madeni yalikuwa yameniandama sana sikuona raha ya kufanya kazi sababu nlishidwa kumsaidia mtu yeyote nyumbani sio baba wala mama wala ndugu yeyote.

Mungu sio wewe wala mimi; mwaka huu deni likaisha na namshukuru Mungu naishi maisha ya furaha na mwaka huu nitaenda nyumban kuwasalimia since 2012 sijawahi kwenda kabisa.

Kwa wale mliochukua mikopo jamani kuweni makini na yale mtakayoenda kufanya msije mkachanyikiwa mkatamani kujinyonga kama mimi.
 
Mikopo inaumiza sana. Tangu nimalize mikopo, sina deni now sidaiwi na mtu, basi nalala usingizi mnono kama mtoto mchanga. Nilishawahi kukopa milioni kumi nikaongezea na za kwangu nikanunua gari ya biashara. Ndani ya mwezi mmoja gari ikala mzinga. Niliteseka sana kulipa deni na kuishi kigumu gumu. Nimeshaapa siku mtu akinona najaza fomu kuchukua mkopo kwenye taasisi ya fedha, basi mtu huyo anichinje kwa msumeno!
Dah! Wenzetu mnawezaje
 
Mbona mnanitisha wakuu nataka inivute mil 15 crdb then nikachukue nyumba kuna jamaa kafail kufanya mrejesho so ameona bora aniuzie mimi nyumba yake kuliko kupigwa mnada daa kanitia nyege kichizi nataka nivumilie ila niwe nishapata nyumba maana kujenga ni mbinde siku hizi
Ulifanikiwa?
 
Mimi huu ni mwaka wa 6 hati yangu ina hama tu kutoka benki hii kwenda benki hii.

Mkopo huu wa mwisho nilichuwa 10,000,000 unanitesa sana, Kwani sehemu kubwa nilipeka kwenye ujenzi badala ya kwenye biashara lakini nashukuru Mungu hata hivyo nimehamia kwangu tangu Julay 2017. Ingawa sijamalizia vizuri hata hivyo nasave 250,000 ya kodi ya nyumba ya kila mwezi.

Shida sasa ni marejesho kurejesha 1m kila mwezi kwa kutumia biashara si mchezo kwani biashara zimeyumba sana.

Nimejikuta biashara moja inakufa na ya pili inawnda rijojo na hii ya tatu ninayoitegemea sana hali si nzuri sana lakini natumaini nitamaliza marejesho kwani yamebali mawili tu nikamilishe.

Ilifikia kipindi unazima simu nakumbuka siku moja nilichelewesha kama miezi 2 na nusu hivi kiafisa mikopo kikanipiga biti mbele za watu eti tutapiga mnada nyumba yako wee siku hiyo nilimuwakia kidogo nimpige makofi nilifoka pale mpaka wateja wakanisupport hata walipokuja polisi ingawa walinitoa lakini walinielewa. Siku hizi hata nikichelewa hawanipigii simu.

Kwa sisi wafanyabiashara hatuwezi kuendelea bila kokopa
Biashara siku hizi imeimarika?
 
130k 0788656975 africana mbeziView attachment 1838836
IMG_20210701_161517_2.jpg
 
Mimi nimechukua mwaka huu, lakini ni wa mwaka mmoja. Mwezi wa tatu namaliza deni. Nilichukua ninunue boda boda lakini huyu jamaa niliyempa boda boda badala ya kuleta hela analeta stories. ...
Yaan pikipiki yako halafu uteseke namna hiyo kisa unaogopa uchawi smh!!! Sijui issue yako iliishaje ila ulijikosea sana kama huchukua hatua ya kumnyang'anya huyo chalii pikipiki
 
Unakuta imefika siku inafanya marejesho huna kitu ukiangalia marejesho kama 1m ukiwa na 50,000 mgukoni unaenda kuzipiga maji zote kesho ukiamka mtu atakaye kusemesha masuala ya hela unakuwa mkali kama mbogo.

Wakati mwingine unakopa za riba unalipa benki kimbembe mwezi unaofuata benki wamadai mtaani ya riba wanadai.

Unazima simu siku mbili kwanza.
Acha kabisa. Me kuna wakati mambo yalinikaba koo. Nadaiwa Kodi ya nyumba, rejesho bank na mke wa bro yuko hospital kajifungua kwa operation wanataka mkwanja, hapo bro Hana kazi kampuni yao ilifilisika na ndo alietusomesha so ilibidi Tu niwajibike. Unaweza tamani ukimbie asee.

Nilitumia akili sana(japo sikuwa sahihi, Mungu anisamehe). Nilikuwa nachukua pikipiki ya boda anaeniamini, namwambia nna Safari nayo narudi baada ya wiki. Naenda weka Ile pikipiki bond, nachukua mkwanja naenda lipa rejesho na kiasi kingine hospital. Baada ya wiki nachukua pikipiki ingine, naweka bond sehemu nyingine afu naenda komboa pikipiki Ile ya Kwanza. Nilifanya hivyo kwa pikipiki kama nne ya tano nusura iniletee shida Ila nashukuru nilipata kampenyo na kuikomboa. Maisha haya, acheni tu jaman.
 
Acha kabisa. Me kuna wakati mambo yalinikaba koo. Nadaiwa Kodi ya nyumba, rejesho bank na mke wa bro yuko hospital kajifungua kwa operation wanataka mkwanja, hapo bro Hana kazi kampuni yao ilifilisika na ndo alietusomesha so ilibidi Tu niwajibike. Unaweza tamani ukimbie asee.

Nilitumia akili sana(japo sikuwa sahihi, Mungu anisamehe). Nilikuwa nachukua pikipiki ya boda anaeniamini, namwambia nna Safari nayo narudi baada ya wiki. Naenda weka Ile pikipiki bond, nachukua mkwanja naenda lipa rejesho na kiasi kingine hospital. Baada ya wiki nachukua pikipiki ingine, naweka bond sehemu nyingine afu naenda komboa pikipiki Ile ya Kwanza. Nilifanya hivyo kwa pikipiki kama nne ya tano nusura iniletee shida Ila nashukuru nilipata kampenyo na kuikomboa. Maisha haya, acheni tu jaman.
Wanasema changamoto ndo huleta akili
 
nilishakopa zaidi ya mara kumi bank ila mikopo miwil ilinitesa sana ila sasa niko sawa, kwa sisi wafanyabiashara usichukue mkopo kwa sababu tu unakopesheka cha msingi angalia mahitaji yako ili usije ukatumia mkopo tofauti na kusudi la mkopo
 
Huu uzi nimeuona punde tu ulivyo anzishwa lakin nilisita kuchangia kutokana na maswahibu yaliyo nipata...Mikopo ilinifanya mpaka nikaathirika kisaikolojia...ingawa bado sija recover....nimeona nisitia neno kwanza...nijipe mda kidogo niweze kusahau...

Nilichanganyikiwa kweli kweli...ilifikia hatua hata bara bara ya vumbi navushwa na watoto wadogo....Mweh..Ndugu zangu kuwen makini na mikopo...na hiz banks za Tz nyingi ni wafanya biashara sidhan kama zina malengo ya kumnufaisha mkopaji...zina interest kubwa...kiasi kwamba lazma uwe makin sna..
Huu uzi nasoma nacheka mwenyewe hahaha maisha haya
 
Daaah!!mi wakati naanza kazi nilikopa 5mil,nilitoa hela yote kwenye account,nikanunua pikipiki ya kutembelea na iliyobaki niliweka gheto ktk bukta flan zile timberland si unajua zinakuaga na mifuko mingi!!bhas bhana mi nakula ugimbi nikiishiwa narudi gheto nazama ndani nachomoa mzigo nasepa naenda kula vyombo!sitosahau Kuna siku naingiza mkono kwenye mfuko imebaki 30,ikabidi niichomoe ile nguo kwenye msumali nikapekua mifuko yote na kukung'uta hamna kitu!!ikabidi nikatoka njee nikaingiza pikipiki ndani nikalala zangu!!
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].

Nimecheka kama mwehu......
 
Juzi kati tu hapo nimevuta milioni 5 na mpaka sasa ishaisha na sioni cha maana nilichofanyia.Nakatwa 800K kwa mwezi kwa mwaka mzima ila nashukuru ni mkopo wa ofisini hauna riba.

Nilikopa kabla ya kufanya tathmini nzuri ya biashara nikajikuta naipeleka kwenye mambo ambayo hayakuwa priority so nimejifunza kitu.
Yani unakatwa 800k kwa mwezi kwa mwaka mzima halafu unasema hauna riba are you serious?[emoji848] yani umekopa M5 unarudisha M9.6[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] aisee tamaa ya pesa za haraka haraka hzi
 
Huu mkasa nilishautoaga humu, sio mbaya nikirudia. Okay nitaelezea in first person view.

Mwaka 2011, nilikuwa nimeacha kazi serikalini, nikaamua kuanza biashara ndogo ndogo kwani zililipa kuliko mshahara wa kazini. Hapa nilikuwa na girlfriend ambae nilimtambulisha nyumbani na kwao pia walinijua. Mimi na huyu gf wangu tulifungua kampuni moja, nitaaiita Xcorp. Gf wangu yeye alikuwa muajiriwa wa serikali(mwanasheria), kwahiyo alikuwa vizuri in terms of lifestyle. Basi tukaamua kuexpand business, tuliplan kujenga kumbi nne ambazo zitakuwa za kisasa... Tuliplan kuweka swimming pool, malls humo humo. Ilitakiwa 1bil. Tukasema we can make it. Wakati naendelea na vibiashara vidogo vidogo vya kwenda China, rafiki yangu wa kike akanitambulisha kwa rafiki yake. Nae alikuwa mdada. Huyu dada nitamuita Grace. Grace alionekana ni mtu mwenyewe mafanikio sana. Aliishi Masaki nyumba ina swimming pool, na counter, pia alikuwa akitumia magari ya bei; BMW X5, Hilux new model, Brevis, Mark X na Range Rover. Kwa kweli enzi hizo Mark X na Brevis zilikuwa za kuhesabu barabarani. Huyu dada akaniambia yeye ni mfanyakazi wa kampuni ya mtandao mkubwa hapa Tz. Basi akaniambia wanaproject lakini inaitaji investors. Hii project ilikuwa kama ndoto ya mchana kwani ndani ya mwaka mmoja ningepata 1B.

Nikamueleza gf, akanielewa. Basi mwanzo tukawekeza 40m tu. Kweli ndani ya wiki mbili tulipata faida ya 40m!!! So tukarudishiwa 80m!!! Aisee nikapiga picha, ile biashara ya China bora niiache kwanza mikiki mikiki ya bandarini na mzigo hapa Tz unakaa miezi miwili plus kuja kuisha na faida ni kama 40% tu. Basi Grace akanichombeza ningeongeza hela ya kuwekeza to 400m. Ningepata 800m faida na ningekaribia goal ya 1b. Nikauza viwanja vyote, magari yote(nilikuwa nayo 8) sikubakiza hata moja, mtaji wa China wote nikakusanya. Nikawa na kama 230m. Nikamuomba Gf aniongezee, akagoma, akaingiza maswala ya kwamba mimi natembea na Grace(hii story nyingine) ila sio kweli. Baadae Gf akaniambia kwanini usiombe mkopo kwa nyumba yako. Duh nikasema poa. Gf ndio alikuwa na connection na watu wa benki basi tukaomba mkopo kwa kutumia kampuni yetu, nikaweka nyumba dhamana. Hapa ndipo natamani ningerudisha siku nyuma.

Wiki ambayo mkopo ulikuwa unatakiwa utoke sikupigiwa wala nini. Nikakaa kimya. Wiki ya pili nikaenda ile benki. Wakaniambia mbona ulikuja kuchukua na ukasign kabisa. Duh nikaenda kuangalia, signature sio yangu, na hela kweli zimeingia, lakini ajabu zimeingia kwenye account ya Gf. Nikampigia hapo hapo. Nilimuwakia sana. Akaniambia hela alishampa Grace 400m. Mkopo tulipata 156m, ilibidi turudishe 200m in 1 year. Dadeki nikaona huu utani. Nikamfata Gf home tulifokeana sana(advice usioe/usiolewe na mwanasheria kama hujui ubishi) nikatulia. Akaingiza mambo ya mimi kutoka na Grace, mara haniamini. Ajabu ni kwamba asilimia kubwa ya vitu at risk ni vyangu yeye kwenye biashara ya China alinipaga kama 30m tu. Kwasababu nilimpenda nikakausha. Grace wiki ya kwanza tuliongea freshi tu, ila baada ya wiki akapotea.

Duh wasiwasi ukanijia. Ila nikasema tusubiri ule muda aliosema hela zitarudi. Muda ukapita Grace hatujui alipo. Gf akanigeuzia kibao mimi. Mara mimi ndio nilimtambulisha kwake. Basi nikamfata yule dada aliyenitambulisha. Akaniambia yeye hayupo karibu nae. Aisee nilitamani kuua mtu. Yeye mwenyewe kweli alivyoniunganisha nae sikumueleza yaliyoendelea. Kwanza alikuwa hajui kama nafanya biashara na Grace. Kwenda kwake Grace nakuta kahama na nyumba ilikuwa ya kupanga sio yake. Magari ya kukodi, yeye alikuwa na BMW X5 tu. Nikaenda kampuni ya simu aliosema ni mfanyakazi, hajulikani!!! Nilikaa chini kwenye floor. Miezi ikapita.

Gf alivyoona nimeishiwa, akawa distant, mara hapokei simu. Matusi kwa wingi, baada ya muda akaniacha. Life lilikuwa gumu. Mwezi uliobidi turudishe mkopo ukaingia, sina mia. Ndugu ndio wananitumia hela ya kula. Siku mbili zinaweza pita nyumbani giza, sina hela ya LUKU. Mboga nzuri ilikuwa dagaa mchele. Grace hajulikani halipo. Basi nikaanza kumkazia Gf, kumtishia kuwa alifoji signature yangu. Basi akawa na uwoga nae akaanza kunisaidia kumtafuta Grace. Akafanikiwa, alimuweka Grace ndani kama wiki nzima kabla hajapata mdhamana. Nikaja kujua ukweli, kumbe Grace ni tapeli hata zile hela za mwanzo zilirudi kwasababu aliwachimba wengine. Kiukweli life lake ni show tu ya kuwateka watu. Basi tukambana, akatupa documents za nyumba yake moja. Akasema ndio alichonacho, BMW lake kuna victim mwingine alishalichukua na bado ana mdai Grace 40m. Therefore nae akagangania documents za nyumba. Tukaongea na polisi, maana Mimi nadai 400m mwenzangu 40m bora nipewe Mimi. Polisi wakasema twende court, mwenyewe sina hata mia. Na yule mdai mwingine yupo vizuri kifedha, as you all know bila hela mahakamani... Acha nisimalizie. Nikaongea na mdai, nikamwambia tuuze nyumba nitamlipa 40m alafu nitachukua iliyobaki. Akakubali ila yeye abaki na documents.

Mzaa. Nyumba haina hati, kwanza value 260m ya kwangu ilikuwa 516m. Kwasababu sina kitu nikakubaliana na hali halisi. Nyumba ya Grace ilikuwa haijamalizika, matengenezo kama 40m, ilikuwa golofa. Nyumba haikuuzika mwaka mzima. Baada ya muda wa kupiga stop order, benki wakapiga mnada nyumba yangu nikahamia ghetto. Nikaanza kupaona kuzimu aisee. Nikasema nisue benki maana walicheza mchezo na Gf, na hela sina za kupambana nao. Nikaona nikimtubua Gf nitajiharibia mwenyewe. Basi Grace tukaachana nae kwani na yeye kapigika mbaya.

Huu mwaka wa 5 tangu nyumba yangu iuzwe. Nakaa jumba amabalo mvua ikinyesha maji yanaingia godoro linaloa. Sina gari wala baiskeli. Nikiona mtu ana starlet namuona Mungu. Msosi nasaidiwa na ndugu. Bado nipo kwenye harakati za kutafuta mteja wa nyumba ya Grace hata kwa 150m nauza nianze upya.


Back to third person view. Gf ana life jingine na kidume mwingine, life is good. Ila Gf yupo hatarini, kwani soon TAKUKURU will be after her. Huu mkasa umemtokea ndugu yangu wa karibu sana. Siku anatimuliwa na polisi kwake alilala mpaka kwenye mchanga analia. Na nyumba yake mpaka leo wateja wanakuja na kuchomoa, haijauzwa. Mpaka watu wa benki wanaleta waganga wafanye manyanga. Nyumba imekaa haina watu mpaka walinzi wa benki wanapangisha vyumba vya ndani. Huyu ndugu yangu kakimbiwa na watu wengi wa karibu kwasababu wanajua kaishiwa. Anyway lesson learnt, Mimi namuomba Mungu aniepushe na haya. Bora niishi na salary au biashara ndogo kuliko kukopa. Ukikopa unakuwa mtumwa.

-callmeGhost
Duu nimepata SoMo kubwa kwako hapo. Wanaume huwa nasema kila siku kuwa twauangushwa na mbunye tu basi.vingekuwepo vidonge vya kuzima hisia
 
Back
Top Bottom