Tuliowahi kuchukua mikopo tukafanya ndivyo sivyo

Pole sana mkuu....hata me Amazon wakalamba kaa $100, na wao pia wameyeyuka hivi hivi[emoji24]
 
Mimi nilikopa mwaka jana NMB Mi. 9 kwa miaka mitano. Nikachukua pikipiki mbili. Moja ya bodaboda na nyingine ya kwangu kutembelea. Mil.4 nikachukua kiwanja na shamba kwa ajili ya kilimo. Laki 5 nikalimisha shmaba na kupanda mahindi na laki tano nikafanyia mambo yangu menginene. Mshahara nikabaki 247,000

Matokeo yake;

i)Bodaboda ilidumu miezi sita ikaibiwa.
ii) mahindi sikupata hata nusu gunia,kwa sababu ya ukame.
iii)mipango yangu ilikuwa mwaka huu nioe kama mambo yangeenda vizur kinyume chake nimeshindwa,mchumba wangu alipoona hali imekuwa tete akaanza visa kumbe kashaanza mahusiano na mwanaume mwingine,nikabaki mimi kama mimi.
iv)Baada ya bodi ya mkopo kuanza kukata 15% nikaanza kuchukua 197,000/= kwa mwezi
v) kwa sasa siwezi saidia chochote kwa mama na ndugu zangu kibaya zaidi mdogo wangu kachaguliwa chuo cha afya diploma ada mil.2. 5 sijaweza kumpa hata mia.

Sina bahati kabisa
 
Pole sana mkuu wanaume tuliumbiwa mateso funga buti tusonge mbele safari bado ndefu
 
Boss hiyo taasisi ya fedha ni ipi? Embu nisaidie maana na mimi natafuta mkopo wa kama 5 million
 
Daah pole man! jikaze aluta continua
 
Mikopo ni noma, hasa ile unapo anza anza kazi. Kuna jamaa yangu amebaki na ufunguo wa gari tu (alichonga copy), gari alishauza na bado anadaiwa na bank. Bahati nzuri alikua staff wa bank hiyo aliyokopa. Anajuta bora angenunua hata kiwanja....
 
Mikopo inaumiza sana. Tangu nimalize mikopo, sina deni now sidaiwi na mtu, basi nalala usingizi mnono kama mtoto mchanga. Nilishawahi kukopa milioni kumi nikaongezea na za kwangu nikanunua gari ya biashara. Ndani ya mwezi mmoja gari ikala mzinga. Niliteseka sana kulipa deni na kuishi kigumu gumu. Nimeshaapa siku mtu akinona najaza fomu kuchukua mkopo kwenye taasisi ya fedha, basi mtu huyo anichinje kwa msumeno!
 
Mbona mnanitisha wakuu nataka inivute mil 15 crdb then nikachukue nyumba kuna jamaa kafail kufanya mrejesho so ameona bora aniuzie mimi nyumba yake kuliko kupigwa mnada daa kanitia nyege kichizi nataka nivumilie ila niwe nishapata nyumba maana kujenga ni mbinde siku hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…