Tuliowahi kuchunga wakati tukiwa wadogo tukutane hapa

Tuliowahi kuchunga wakati tukiwa wadogo tukutane hapa

kALEnga kidamali umenikumbusha mabali sana. Miaka hiyo tumekwenda machungani na watoto wenzangu tukafika mahali tukakutavkuna mti wa mwembe huko porini. Tukaoana maembe kwenye matawi ya juu yakiwa yameiva na yana mvuto hasa. ( yale maembe yanayokuwa kadhaa kwenye fungu moja)

Basi tukakubaliana tufanye mashindano ya kuuparamia ule mwembe ili kuyawahi yale maembe kule mtini. Kwamba atakayewahi kuyafikia, basi ndiye atakuwa mshindi na maembe yale yatakuwa yake. Basi nikakwea kwa spidi kubwa na kuwashinda wenzangu, huku uchu wa kula embe ukiwa umenijaa tele. Nilipoyafikia, bila kufanya ukaguzi wa mazingira ya eneo la tukio, nikayaparamia maembe ili niyachume kabla wenzangu hawajafika.

Ile nashika kile kikonyo kwa ajili ya kuchuma yale maembe, nilipigwa sindano kadhaa matata sana za manyigu, hadi nikachanaganyikiwa na kupoteza mwelekeo. Niliangua kilio kikubwa hatari. Sijui hata nilishukaje kwenye ule mti. Maana nilishitukia nipo chini. Na kichwa kilikuwa kimenyolewa upara. Manundu ya kutosha yakatokea kichwani, kichwa kinauma balaa. Habari ya kuchunga ikaishia hapo, ikabidi nirudi nyumbani huku nalia kwa maumivu makali.
 
Kitambo sana, Kuna kuchagua madume ya ng'ombe, kondoo au mbuzi kwa ajili ya kupigana. Nakumbuka tulikuwa na dume moja matata lilikuwa na pembe kali balaa. Kuna siku tulimpiganisha na dume kutoka Kijiji Cha jirani yule dume alichomwa pembe ya mbavuni mpaka utumbo ukawa unaonekana ndo ikawa sababu ya mpaka kuuzwa. Pia kutega tetele au mnawaita njiwa poli, mitego ya wanyama wadogo wadogo mpaka raha. kutengeneza ng'ombe wa udongo kisha unawapiganisha.
 
Hadi leo wengine bado tunachunga japo mara moja moja.

Kuna siku niliwahi kunywa lita 5 ya maji bila kupumzika ila baada ya kumaliza nilikuja kubebwa na baiskeli.

Nakumbuka ilikuwa miaka ya 2006 kiangazi cha mwezi wa 10 kuna Kijiji kinaitwa Namwawala (Ifakara) kipindi hicho malisho yalikuwa hakuna hivyo kulazimika kwenda mbali.

Just imagine kwa wanaopafahamu tulikuwa tunatoka Namwawala tunafuata malisho msitu wa Idete (Magereza) yaan unakula ugali saa 12:00 asubuh unarudi malishoni saa 1:00 usiku maji ya kunywa ng'ombe na wachungaji yalikuwa mto Narubungo ambao tulikuwa tunapita saa 2 asubuh wakat wa kwenda na kurudi saa 11 jioni.

Malisho yenyew ni majani yaliyochomwa moto (ule msitu wote ulikuwa unaungua moto) halafu yanachipua majani mengine mapya malaini ambayo ng'ombe wanayapenda sana.

Siku ya tukio nakumbuka sikunywa maji mtoni basi ile kufika saa 6 kiu ikaanza kunikamata kisawasawa. Nililia sana hadi nikanywa mkojo wangu lakini kiu haikuisha.
 
kama ulikuwa hudandii ng'ombe kama farasi basi hujachunga.
kama ni mkubwa sana unavizia akiwa anakula majani unatumia kichwa chake kama ngazi,kosea timing akanyage kidole cha mguu unaouacha chini[emoji1][emoji1][emoji1],niliishatolewa kucha kwa mkasa aina hii.

kosea mambo yote ila my friend usijevaa koti lenye kofia juu ukapita karibu na ng'ombe atakuzingua vibaya sana(sio hawa ngombe wenu wa maziwa).

kuna mang'ombe ilikuwa ukizubaa tu yanaenda kwenye mashamba ya watu.

kingine ngombe nayeye ana tabia kama ya mbwa, akijutisha ukajaa,anakuoshea.ila ukimkazia anatulia.

Kupiganisha ng'ombe pale mnapokutana wachungaji toka maeneo tofauti... ng'ombe wangu NANG'HIMA (RIP) alikuwa kinara wa muda wote, cha ajabu alikuwa ngombe mpole, anajua kuongoza wengine kama binaadam, yani akitulia mahali wengine wote wanatulia, hata uende wapi unawakuta. Huyu NANG'HOO alikuwa machachari, kwanza mbishi, akikutisha ukastuka anapita na wewe, hakuwa na pembe, mwembamba flani rangi ya kijivu ila kwa wenzake ni muoga balaaa.

Dah, nimechapwa sana kwa kujisahau Nang'hoo akapita na mahindi ya watu, michezo ya kugongesha vimbegu flani ivi(nimevisahau majina). Kuingia chaka la huko top of the mountain. Ukirudi umeshiba matunda, unakabidhiwa kombe la nusu lita la maziwa. Dah!

hili kombe lilitaka kunifanya nimtie mtu bisu. Ilikua kipindi cha ukame, nimeenda chimbo la mbali narudi zangu jioni sana njaa inauma kidume begani nina mzigo wa majani ya kuwatandiukia ng'ombe wangu. Napita zizini nawatandikia kisha naskilizia mida ya kukamua.... nikasema ngonja nikapige kombe langu la maziwa af nije kuendelea, dah!

Sista duu mmoja beki3 wa aunt kayanywa halafu ananipiga biti nisubiri menyu ya jioni, kumbe alikuwa anafanya makosa sana kunywa maziwa ya mzee ni mwiko hata awe mtu mzima kiasi gani.

Sasa ile kumuelekeza akaleta zile za kimjini mjini kwamba nasemaje sasa kama kunywa ndo keshakunywa. Daaaaaaa, alikuwa kanizidi sana tu umri lakini nikamtembezea makofi ya kumtoa wenge, mpwa wangu akaingiliaa, ni mkubwa pia yeye ni kama kiongozi wa familia kipindi hicho. Haloo, nlichokifanya hakuna mtu aliamini. Eti kisa kombe la maziwa, ilibaki kidogo nimtie bisu, sema akafanikiwa kunidhibiti ila ilibidi atumie nguvu kubwa sanaaaa kisha nikaingia zangu ndani nikachukua vitu vyangu paki kwe begi nikasepa, na hapo safari ya kupita pori kwa pori maana magari wakati huo hakuna, naishia hapo kwa kuwa stori ndefu sana.

Ila uzi huu umefanya nikumbuke mambo mengi sana.

Sharaut kwa wana tuliotoka kuchunga ngombe hadi sasa tunakula bia mjini na kusumbua watoto marinda chori chori.

Tulitamba porini na sasa tunatamba mjini.
 
Mkuu pole sana, hayo madude yamenigonga sana tena huwa hayakai mengi kwenye Yale masega yake unaweza kukuta yako mawili tu halafu huwa si rahisi kuyaona haraka yaani unaweza shituliwa kuwa yapo na ushagongwa teyari maumivu yake ni noma halafu unakuta mtoto kakaza tu halii wala nini kweli ujasiri unatokea mbali.

kALEnga kidamali umenikumbusha mabali sana. Miaka hiyo tumekwenda machungani na watoto wenzangu tukafika mahali tukakutavkuna mti wa mwembe huko porini. Tukaoana maembe kwenye matawi ya juu yakiwa yameiva na yana mvuto hasa. ( yale maembe yanayokuwa kadhaa kwenye fungu moja)

Basi tukakubaliana tufanye mashindano ya kuuparamia ule mwembe ili kuyawahi yale maembe kule mtini. Kwamba atakayewahi kuyafikia, basi ndiye atakuwa mshindi na maembe yale yatakuwa yake. Basi nikakwea kwa spidi kubwa na kuwashinda wenzangu, huku uchu wa kula embe ukiwa umenijaa tele. Nilipoyafikia, bila kufanya ukaguzi wa mazingira ya eneo la tukio, nikayaparamia maembe ili niyachume kabla wenzangu hawajafika.

Ile nashika kile kikonyo kwa ajili ya kuchuma yale maembe, nilipigwa sindano kadhaa matata sana za manyigu, hadi nikachanaganyikiwa na kupoteza mwelekeo. Niliangua kilio kikubwa hatari. Sijui hata nilishukaje kwenye ule mti. Maana nilishitukia nipo chini. Na kichwa kilikuwa kimenyolewa upara. Manundu ya kutosha yakatokea kichwani, kichwa kinauma balaa. Habari ya kuchunga ikaishia hapo, ikabidi nirudi nyumbani huku nalia kwa maumivu makali.
 
Kwa sababu ya kuchunga;

~Nilipokea vipigo kutoka kwa wakulima.
~Nilijeruhiwa na Mamba mtoni
~Niliwah kulala porini siku 2 kwa kupotea
~Niliwah kuburuzwa na ng'ombe aliyezaa
~Niliwah kulala selo n.k..

Kiufup nimepitia mikasa mingi sana kutokana na kuchunga.
Fimbo ni kawaida kama ulishachunga, nakumbuka nilikulaga fimbo kisa nilibeba hera machungoni mbugani vwawa alafu yule jamaa mkubwa wangu anaomba hera tunasema hazipo. Ilabidi atusachi kwenye ng'ombe kipindi hko hera ikiwa mfukoni kwa ndani unaufunga na kamba au mnati ili isipotee mtu akiingiza mkono kamfuko kafupii, jamaa akastukia bhana akanivua kipensi achukue hera akanunue miwa!

Akanipora hera nililia nikaondoka na chupi tu nikapita relini toka mbugani kwa mkusi hadi isangu (Mbozi) huku nalia lkn ile nmefika nyumbani nikajistukia na hera yenyewe niliiba so nikakaa kimya siku ikaisha jion jamaa karudisha ng'ombe na kaptura daaaaah sitakuja sahau hlo tukio maana nlikulaga fimbo saaana akati hera ni yangu.
 
Moment nyingine ilikuwa ni kurina au kupakua asali wakati wa mchana,moto ilikuwa tunapekecha kwa miti Fulani hivi kwenye hili nilishangaa kuja kusoma tena darasani kuwa ndio ilikuwa teknolojia ya mababu zetu huko nyuma wakati wagundua moto.

Sasa katika vitu hatari ni kupakua asali wakati wa mchana nyuki huwa ni wakali na wanang'ata ile mbaya siku moja huko maporini tuliona kichuguu na nyuki walikuwemo humo tukapanga mission ya kutoa asali nakumbuka ilikuwa mida ya SAA nane hivi nilikuwa na wenzangu walionizidi umri kidogo na sheria ni marufuku mtu yeyote kulia endapo utang'atwa yaani ukilia au kujitingisha unatandikwa vibao na unafukuzwa na hiyo asali hutaila hata kidogo.

Sasa wale walionizid umri kidogo wao wanaingiza mikono kutoa masega mimi nilikuwa natakiwa kuyapokea na kwenda kuweka pembeni kidogo, sasa katika siku nilizogongwa na nyuki ilikuwa ni siku hiyo yaani niligongwa hadi nikahisi naweza fariki kwa sababu mwili uliumuka ikafika mahali maumivu nikawa nayasikia kwa mbaali macho yalivimba hadi nikawa nashindwa fungua macho ila bado sikuonewa huruma, full kukaziana yaan.

Kukomaa kwangu kote ni kwamba nisije nyimwa asali kwa sababu kama haujashiriki hutaruhusiwa kula asali na ile asali ilikuwa inaletwa nyumbani inaweza tumika hata zaidi ya wiki sasa wakisema Fulani hakushiriki basi hata wale wa nyumbani hawakuruhusu kabisa kutumia.

Yaani Yale mazingira ya ukuaji ni nguvu za mungu tu ndio zimetufikisha huku yaani mwanzo mwisho ni kucheza mission za hatari bila hofu wala wasiwasi wa aina yoyote.
 
Mkuu hiyo kitu achana nayo hata awe ndama hajaonekana siku hiyo hamlali nyumbani atatafutwa hata iwe usiku tena wewe mchungaji kwenye utafutaji ndio unatangulizwa mbele kuonyesha ulikopita nao ng'ombe na ukizingua mkong'oto unakuhusu.
Ng'ombe mmoja akipotea porini. Unarudisha wengine zizini. Unarudi porini kumtafuta ng'ombe aliyepotea usiku kucha mpaka apatikane akiwa hai au amekufa
 
dah umenikumbusha mbali na mbuzi wangu wote walikua na majina na nilikua nazifaham tabia zao wote mara nlipotoka shule mm huyoo naingia zangu pori huko ntawakatia majani na kupga nao story ntawaimbia na vingne vingi tu nimeacha kuchunga nlpo fika kidato cha tatu
 
Binafsi kati ya wale waliochunga ng'ombe, mbuzi na kondoo ni pamoja na mimi. Nakumbuka mwaka 1961 mwaka wa uhuru na mwaka huo mvua zilinyesha sana hakuna siku ilipita bila kwenda kuchunga. Nakumbuka nilikuwa darasa la kwanza na wakati huo darasa la kwanza tulikuwa tunasoma asubuhi na kurudi saa sita hivyo ninapotoka shuleni baada ya kula ni kwenda kuchunga. Nilipenda sana kuchunga na iliniweza kunijenga kwa maeneo yafuatayo:- (1) Kula matunda kule porini na kuwa na afya kimwili. (2) kuwinda ndege wa porini(3) Kucheza michezo mingi hasa mpira na kuwa na afya nzuri (4) Kuogelea kwenye mito na kuwa mtalaam wa kuogelea. (5) Kuhakikisha kuwa msimamizi mzuri wa mifugo yetu, kuwalinda na kuwatunza. Mfano hai unapochunga utakuta ng'ombe anazaa machungani na ni kilomita tano toka nyumbani. Hapa lazima uhakikishe unamfikisha yule ndama aliyezaliwa kwa usalama nyumbani hata ikibidi kumbeba. Binafsi nimechunga sana na bado naipenda kazi hii ya kuchunga japo umri umeenda.
 
Back
Top Bottom