akilindefu
Member
- Sep 5, 2020
- 69
- 63
wakishua kaeni pembeni muda wa kujimwaya mwaya huu nakumbuka tulienda kuchunga na dogo mtoto wa mjomba wangu kondoo akawa anamzingua jamaa alivomkamata ikabidi amtie adabu kwa kumla kiboga dah nlicheka sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tupo hapa. Ulichunga upande wa serengeti (ngoreme) au upamde wa tarime?
Bila shaka utakuwa mtu wa nyumbani kwetu tabora au shinyanga..Kitambo sana, Kuna kuchagua madume ya ng'ombe, kondoo au mbuzi kwa ajili ya kupigana. Nakumbuka tulikuwa na dume moja matata lilikuwa na pembe kali balaa. Kuna siku tulimpiganisha na dume kutoka Kijiji Cha jirani yule dume alichomwa pembe ya mbavuni mpaka utumbo ukawa unaonekana ndo ikawa sababu ya mpaka kuuzwa. Pia kutega tetele au mnawaita njiwa poli, mitego ya wanyama wadogo wadogo mpaka raha. kutengeneza ng'ombe wa udongo kisha unawapiganisha.
Dah! pole sana mkuuSitasahau siku moja nilisikia mbwa wakitoa milio fulani hivi pembeni ya kichaka kimoja nikaenda fasta kwa bashaha zote nikajua kuna mnofu umedakwa, ile kufika asalaaaaleee! Nikakuta mbwa mmoja anamalizia kukata roho kagongwa na nyoka aina ya koboko Kubwa hilo, zile mbio nilizotoka nazo hapo ilikuwa ni hatari yaani niliondoa ng'ombe haraka na kulihama lile pori na sikuwahi rudi tena lile pori. Niliambiwa koboko akikugonga nusu saa haifiki usha fika akhera sasa nikawa nimejawa hofu hatari.
Dah! ni hatari kwahyo ulikuwa unachunga kipindi uko shule ama nyumbani?Nilichunga ng'ombe sana kipindi niko Advance
Aisee wewe ni lijendi.Nakumbuka mengi coz am cowboy. Ntakuja na story kamili but kwa kuanzia
1. Kupewa maziwa mengi kabla ya kutoa mifugo na baada ya kumrudisha
2. Tulikuwa tunashindana nani atakaeenda ndani zaidi ya Pori
3. Kuwinda ndege na sungura
4. Kuogelea kwenye lambo la kunyweshea mifugo ,hapo panakuwaga na Mademu wanaochungaga nyumban
5. Hamna kitu raha kama mbuzi kuzaa mapacha kwenye zamu yako ,unawabeba vitoto vya mbuzi kifuani hadi nyumbani
HahaWe jamaa kama mimi mda wa kuludi nadandia kama star wa kichina.
Magepu hayo mkuuDah, tulikuwa tunachunga na madada makubwa makubwa! Tukiwa machungani yanatupa tenda ya kwenda kutoa ng'ombe karibu na mashamba ya watu halafu ukirudi yanakuzawadia kwichi-kwichi hotai una-do
Huku unalia Kama mbuzi meeeee! Meeeeee!!! Huku anakufuataNakumbuka mengi coz am cowboy. Ntakuja na story kamili but kwa kuanzia
1. Kupewa maziwa mengi kabla ya kutoa mifugo na baada ya kumrudisha
2. Tulikuwa tunashindana nani atakaeenda ndani zaidi ya Pori
3. Kuwinda ndege na sungura
4. Kuogelea kwenye lambo la kunyweshea mifugo ,hapo panakuwaga na Mademu wanaochungaga nyumban
5. Hamna kitu raha kama mbuzi kuzaa mapacha kwenye zamu yako ,unawabeba vitoto vya mbuzi kifuani hadi nyumbani
Kipindi cha mvua kuchunga nikugumu unakuta Zizi limekuwa tope, huko porini sasa ndiyo balaa maji na tope, alafu bado kunyeshewa na mvua ukiwa machungani, kwenye raha nilikuwa napenda kuchunga na rafiki zangu tunaenda na kibiriti tukifika huko tunaiba Maindi na viazi, kwenye mashamba ya wanakijiji tunaenda kuchoma, kiukweli nilikuwa nainjoy, ila sitasahau kuna siku tulikuwa tukicheza mbuzi [emoji238][emoji238] wakaingia kwenye shamba la mwanakijiji mm ndiye nilikuwa mdogo nikatumwa niende kuwafuata nilikuta mwenye shamba ana panga alinikamata nakuanza kunipiga ubapa hadi alinijeruhi mkono wa kushoto, wazazi walikaa wakaongea na mambo ya kijijini yalivyo ile kesi iliisha ila hadi leo nina kovu la kukatwa na panga mkononiJamani wale wote ambao tumewahi kuchunga wakati tukiwa wadogo kabla hatuja anza shule na hata baada ya kuanza shule yaani ukirudi shule unachunga na zile siku za wikiendi basi wewe ni kwenda porini/malishoni kuchunga mifugo kama vile ng'ombe, mbuzi na kondoo tukutane hapa kuelezea uzoefu wetu pamoja vituko, mikasa na masahibu ya huko porini/malishoni ulipokuwa unachunga.
Mimi nilikuwa nikipenda sana kutokana na zile raha za kupata kila aina za matunda huko maporini pia kulikuwa na kuwinda wanyama wadogowadogo kama vile digidigi, pimbi, sungura pamoja na kanga na kware yaani ilikuwa wewe mchungaji unaporudi unapokelewa kwa heshima Kubwa ukirudi hasa ukiwa na mnyama uliyewinda huko machungoni, yaani ilikuwa kijana anayechunga anajaliwa na kuheshimiwa nyumbani mda wote kabla ya kutoka na baada ya kurudi machungoni anapewa chakula kizuri cha kushiba bila kusahau maziwa ya kutosha hata kama chakula ni kidogo basi atakula mchungaji kwanza wengine mtasubiri baadae wasiowachungaji walitamani kuwa wachungaji kutokana na mchungaji anavyojaliwa pale nyumbani kwetu.
Kingine nilichokuwa nakipenda ni kutembea na jeshi la mbwa wakali waliofundishwa kuwinda huku kila mbwa akiwa kapewa jina lakie kama vile chui, simba, nyati, mbogo, mwitu, jeshi, polisi, n.k
Hawa mbwa kwanza wakati wa kwenda machungoni ilikuwa ni mwiko kuwapa chakula(asiwe mvivu kuwinda) yaani mbwa akiwa na njaa akifika porini dakika kumi nyingi digidigi kadakwa hapo utasikia mbwa akitoa mlio wa sauti kuashiria mimi niende kuna jambo limetokea kwani wakikamata mnyama yeyote hawamli hadi mimi niende nikamchukue kama ni kumalizia kumchinja nifanye mimi na hapo mbwa watafurahi sana kwani kichwa ,miguu,matumbo ya ndani ndio mlo wao yaani nilikuwa nawapikia supu moja matata mno, baada ya kuja huku dsm nimeshangaa kuona supu lile ndio linaitwa kongoro.
Aisee ninayo mengi, hebu share na wewe yako.
Huyo kijana yeye alikuwa na kinga ya kifo?Mimi kuchunga kulinisababishia ninusurike kufa kifo kimoja hatar sana. Tangu siku hyo mzee ilibd aajir kijana kwa ajili tu ya kuchunga mbuzi.
Mbio.za kumuacha koboko ukiwa na ng'ombe,au uliwaacha kwanza?Sitasahau siku moja nilisikia mbwa wakitoa milio fulani hivi pembeni ya kichaka kimoja nikaenda fasta kwa bashaha zote nikajua kuna mnofu umedakwa, ile kufika asalaaaaleee! Nikakuta mbwa mmoja anamalizia kukata roho kagongwa na nyoka aina ya koboko Kubwa hilo, zile mbio nilizotoka nazo hapo ilikuwa ni hatari yaani niliondoa ng'ombe haraka na kulihama lile pori na sikuwahi rudi tena lile pori. Niliambiwa koboko akikugonga nusu saa haifiki usha fika akhera sasa nikawa nimejawa hofu hatari.
Nyanda za juu kusini ndiyo mambo yao ili wawe kama Bakhresa,Ushirombo huku,ni chale matakoni tu,ng'ombe wanazaana hatariSema wachungaji wengi kwenye umri wa balehe huwa wanafanyaga mapenzi na ngombe, mbuzi, kondooo, tupe hii experience mkuu.
Za Shule?Nilichunga ng'ombe sana kipindi niko Advance
Bila kusahau walikuwa na majina.ukimuita anaitika na kutii amriKama ulikuwa hudandii ng'ombe kama farasi basi hujachunga.
Kama ni mkubwa sana unavizia akiwa anakula majani unatumia kichwa chake kama ngazi,kosea timing akanyage kidole cha mguu unaouacha chini[emoji1][emoji1][emoji1],niliishatolewa kucha kwa mkasa aina hii.
Kosea mambo yote ila my friend usijevaa koti lenye kofia juu ukapita karibu na ng'ombe atakuzingua vibaya sana(sio hawa ngombe wenu wa maziwa).
Kuna mang'ombe ilikuwa ukizubaa tu yanaenda kwenye mashamba ya watu.
Kingine ngombe nayeye ana tabia kama ya mbwa,akijutisha ukajaa,anakuoshea, ila ukimkazia anatulia.
...kunyolewa upara tena?...wapi huko mkuu...manyigu yenyewe sawakALEnga kidamali umenikumbusha mabali sana. Miaka hiyo tumekwenda machungani na watoto wenzangu tukafika mahali tukakutavkuna mti wa mwembe huko porini. Tukaoana maembe kwenye matawi ya juu yakiwa yameiva na yana mvuto hasa. ( yale maembe yanayokuwa kadhaa kwenye fungu moja)
Basi tukakubaliana tufanye mashindano ya kuuparamia ule mwembe ili kuyawahi yale maembe kule mtini. Kwamba atakayewahi kuyafikia, basi ndiye atakuwa mshindi na maembe yale yatakuwa yake. Basi nikakwea kwa spidi kubwa na kuwashinda wenzangu, huku uchu wa kula embe ukiwa umenijaa tele. Nilipoyafikia, bila kufanya ukaguzi wa mazingira ya eneo la tukio, nikayaparamia maembe ili niyachume kabla wenzangu hawajafika.
Ile nashika kile kikonyo kwa ajili ya kuchuma yale maembe, nilipigwa sindano kadhaa matata sana za manyigu, hadi nikachanaganyikiwa na kupoteza mwelekeo. Niliangua kilio kikubwa hatari. Sijui hata nilishukaje kwenye ule mti. Maana nilishitukia nipo chini. Na kichwa kilikuwa kimenyolewa upara. Manundu ya kutosha yakatokea kichwani, kichwa kinauma balaa. Habari ya kuchunga ikaishia hapo, ikabidi nirudi nyumbani huku nalia kwa maumivu makali.