Tuliowahi kuchunga wakati tukiwa wadogo tukutane hapa

wakishua kaeni pembeni muda wa kujimwaya mwaya huu nakumbuka tulienda kuchunga na dogo mtoto wa mjomba wangu kondoo akawa anamzingua jamaa alivomkamata ikabidi amtie adabu kwa kumla kiboga dah nlicheka sana
 
Bila shaka utakuwa mtu wa nyumbani kwetu tabora au shinyanga..
 
Dah! pole sana mkuu
 
Aisee wewe ni lijendi.
 
Dah, tulikuwa tunachunga na madada makubwa makubwa! Tukiwa machungani yanatupa tenda ya kwenda kutoa ng'ombe karibu na mashamba ya watu halafu ukirudi yanakuzawadia kwichi-kwichi hotai una-do
Magepu hayo mkuu
 
Mimi kitu yenyewe sitaisahau ile kulima na ng'ombe, unaamshwa SAA tisa au kumi usiku, tulikuwa tunaita sheli, yaana unaenda kulima ukiwa na wenge la usingizi, njiani full kufakamia visiki
 
Huku unalia Kama mbuzi meeeee! Meeeeee!!! Huku anakufuata
 
Nimechunga sana hadi namaliza kidato cha nne. Niliyowahi kukutana nayo au kuyatenda ni mengi sana.

Nikiwa mdogo, siku moja nachunga pamoja na babu yangu, nikasikia mbuzi Analia kwa mfululizo. Nikataka kwenda ili niangalie kulikoni mbuzi alie hivyo? Babu yangu akanizuia nisiende huko na badala yake akaanza yeye kunyata kuelekea huko, name nikimfuata kwa nyuma. Kufika tukamkuta Chatu anajiviringisha akiwa amemkaba mbuzi. Babu alikuwa napenda kuchunga na Gobole lake. Aliachia risasi ya kwanza, lakini chatu akaendelea kumkunja mbuzi, akaongeza ya pili, hapo chatu alitulia kidogo. Alipoongeza ya nne, chatu alijikunjua na kumwacha mbuzi lakini tayari akiwa ameshakufa. Chatu alihangaika na baadae akatulia nae akiwa ameshakufa.

Nikiwa mkubwa nachunga mwenyewe, siku moja nikiwa nimetulia juu ya kichugu na mbwa wawili niliokuwa nao, niliwaona mbuzi wakiwa wanakimbia kutoka kichakani. Nikiwa nashangaa na kujiuliza kulikoni, mara mbwa mmojawapo alitoka juu ya kichuguu kwenda kule mbuzi wanakokimbia. Ghafla nilimsikia akitoa kilio cha uchungu sana. Kuchunguza vizuri nikiwa juu ya kichunguu, nikamwona nyoka akiwa amemng’ata yule mbwa na alipomwachia, nilimwona mbwa anadondoka chini na akawa anaangaza angaza tena. Nikawaza hapa nitafuatia mimi. Nilitoka nduki kwa spidi ambayo sijui ilitoka wapi. Nilienda mbali sanakuleamabko ng’ombe walikuwa wakielekea ng’ombe kuwasubiri wanifikie.

Niliwahi kuwapeleka ng’ombe kunywa maji mtoni, mto ambao una vichaka sana. Ng’ombe waliingia kunywa maji name nikabaki ng’ambo nawasubiri. Ajabu ni kwamba walirudi wachache sana kuliko idadi yao. Nikaingia mtoni na kufuata uelekeo walioufuata kunywa maji. Nikawaona ng’ombe wengi wako ng’ambo nyingine ya mto kwenye shamba la Mwalimu Nyerere. Niliwafuata na kuwaondoa kwa woga sana, maana sikutegemea kuwamaliza mle shambani bila kukamatwa. Nikawa nikiwapeleka pale natangulia huko wanakovukia kuingia shambani.

Nimekula sana karanga, Mihogo na Mahindi kwenye mashamba ya watu na hata ya kwetu.

Nimecheza michezo mingi sana huko, nimewinda wanyama na ndege na kuloa samaki kwenye mabwawa.
 
Kipindi cha mvua kuchunga nikugumu unakuta Zizi limekuwa tope, huko porini sasa ndiyo balaa maji na tope, alafu bado kunyeshewa na mvua ukiwa machungani, kwenye raha nilikuwa napenda kuchunga na rafiki zangu tunaenda na kibiriti tukifika huko tunaiba Maindi na viazi, kwenye mashamba ya wanakijiji tunaenda kuchoma, kiukweli nilikuwa nainjoy, ila sitasahau kuna siku tulikuwa tukicheza mbuzi [emoji238][emoji238] wakaingia kwenye shamba la mwanakijiji mm ndiye nilikuwa mdogo nikatumwa niende kuwafuata nilikuta mwenye shamba ana panga alinikamata nakuanza kunipiga ubapa hadi alinijeruhi mkono wa kushoto, wazazi walikaa wakaongea na mambo ya kijijini yalivyo ile kesi iliisha ila hadi leo nina kovu la kukatwa na panga mkononi
 
Mimi kuchunga kulinisababishia ninusurike kufa kifo kimoja hatar sana. Tangu siku hyo mzee ilibd aajir kijana kwa ajili tu ya kuchunga mbuzi.
Huyo kijana yeye alikuwa na kinga ya kifo?
 
Mbio.za kumuacha koboko ukiwa na ng'ombe,au uliwaacha kwanza?
 
Sema wachungaji wengi kwenye umri wa balehe huwa wanafanyaga mapenzi na ngombe, mbuzi, kondooo, tupe hii experience mkuu.
Nyanda za juu kusini ndiyo mambo yao ili wawe kama Bakhresa,Ushirombo huku,ni chale matakoni tu,ng'ombe wanazaana hatari
 
Bila kusahau walikuwa na majina.ukimuita anaitika na kutii amri
 
...kunyolewa upara tena?...wapi huko mkuu...manyigu yenyewe sawa
 
Nakumbuka nilikua mtoto pekee ambae sikuleta ubishi kwenye swala la kwenda kuchunga na kufanya iwe kama kazi yangu, lakini ilinifanya nichukiwe na watu wengi mtaani kwasababu mtaa wote familia yetu pekee ndiyo tulikuwa wafugaji na wengine wote wakulima. swala la kulisha kwenye mashamba ya watu kwangu ilikua kawaida sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…