kALEnga kidamali
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 542
- 735
- Thread starter
-
- #61
Kundi la mbwa ndio lilisaidia kupoteza makini ya koboko, yaani mbwa wawindaji huwa hawashindwi kizeme walikuwa bado wakimzonga zonga licha ya kuwà mbwa mmoja aligongwa na kupoteza maisha,Mbio.za kumuacha koboko ukiwa na ng'ombe,au uliwaacha kwanza?
Hatari hiyo mzee,ukifika hapo nyumban hushoboki na MTU maana wewe ni shujaaHuku unalia Kama mbuzi meeeee! Meeeeee!!! Huku anakufuata
Duu kweli watu tuna vipaji tofauti! tofauti kuchunga ngombe? jua lako, mvua yako!Mimi nimechunga sana. Mwaka 1961 mwaka mzima nilichunga na sikupata kuugua. Ije mvua ije jua wewe na mifugo. Ng'ombe akizaa machungani lazima unahakikisha ndama wake anafika salama nyumbani na kama hana uwezo wa kutembea ni jukumu lako kumbeba mpaka nyumbani. Furaha ya kuchunga ni kula matunda pori huko porini na kweli yanajenga mwili sana na pia michezo mbalimbali huko porini. Kwa kweli nilipenda kuchunga.
Ulikuw mpumbavu Sana,unalisha Kwenye mashamba ya watu?Nakumbuka nilikua mtoto pekee ambae sikuleta ubishi kwenye swala la kwenda kuchunga na kufanya iwe kama kazi yangu, lakini ilinifanya nichukiwe na watu wengi mtaani kwasababu mtaa wote familia yetu pekee ndiyo tulikuwa wafugaji na wengine wote wakulima. swala la kulisha kwenye mashamba ya watu kwangu ilikua kawaida sana.
My favorite part ilikua ni wabhademi yaani ugali mkubwa wa moto wa kwenye chungu wa asubuhi ukute na maziwa au ng'homele aka bbq iliyopikwa na maziwa plus kisamvu cha kulala utachunga sana na njaa hutasikia hadi jua lizameJamani wale wote ambao tumewahi kuchunga wakati tukiwa wadogo kabla hatuja anza shule na hata baada ya kuanza shule yaani ukirudi shule unachunga na zile siku za wikiendi basi wewe ni kwenda porini/malishoni kuchunga mifugo kama vile ng'ombe, mbuzi na kondoo tukutane hapa kuelezea uzoefu wetu pamoja vituko, mikasa na masahibu ya huko porini/malishoni ulipokuwa unachunga.
Mimi nilikuwa nikipenda sana kutokana na zile raha za kupata kila aina za matunda huko maporini pia kulikuwa na kuwinda wanyama wadogowadogo kama vile digidigi, pimbi, sungura pamoja na kanga na kware yaani ilikuwa wewe mchungaji unaporudi unapokelewa kwa heshima Kubwa ukirudi hasa ukiwa na mnyama uliyewinda huko machungoni, yaani ilikuwa kijana anayechunga anajaliwa na kuheshimiwa nyumbani mda wote kabla ya kutoka na baada ya kurudi machungoni anapewa chakula kizuri cha kushiba bila kusahau maziwa ya kutosha hata kama chakula ni kidogo basi atakula mchungaji kwanza wengine mtasubiri baadae wasiowachungaji walitamani kuwa wachungaji kutokana na mchungaji anavyojaliwa pale nyumbani kwetu.
Kingine nilichokuwa nakipenda ni kutembea na jeshi la mbwa wakali waliofundishwa kuwinda huku kila mbwa akiwa kapewa jina lakie kama vile chui, simba, nyati, mbogo, mwitu, jeshi, polisi, n.k
Hawa mbwa kwanza wakati wa kwenda machungoni ilikuwa ni mwiko kuwapa chakula(asiwe mvivu kuwinda) yaani mbwa akiwa na njaa akifika porini dakika kumi nyingi digidigi kadakwa hapo utasikia mbwa akitoa mlio wa sauti kuashiria mimi niende kuna jambo limetokea kwani wakikamata mnyama yeyote hawamli hadi mimi niende nikamchukue kama ni kumalizia kumchinja nifanye mimi na hapo mbwa watafurahi sana kwani kichwa ,miguu,matumbo ya ndani ndio mlo wao yaani nilikuwa nawapikia supu moja matata mno, baada ya kuja huku dsm nimeshangaa kuona supu lile ndio linaitwa kongoro.
Aisee ninayo mengi, hebu share na wewe yako.
My favorite part ilikua ni wabhademi yaani ugali mkubwa wa moto wa kwenye chungu wa asubuhi ukute na maziwa au ng'homele aka bbq iliyopikwa na maziwa plus kisamvu cha kulala utachunga sana na njaa hutasikia hadi jua lizame
Mimi nimechungia kwetu ngoremeTupo hapa. Ulichunga upande wa serengeti (ngoreme) au upamde wa tarime?
Yaani wee!! acha tu! najua fika unacho waza kabisaaa!! kiukweli! Na baba yangu aliwaza hivo! hivooo!!! yaani hakuna mtu mbaya km Ndugu humu Duniani, unamsaidia unamnyanyua lkn mmm! ana akili sana aliyesema ''kikulacho.......Nyaru-sare
Hao mashangazi zako walikuwa wameshikwa akili na wasomali, iweje wauze mifugo kisha watokomee kufuatana tena na hao Wasomali?
Kama walikuwa mabinti, nishajua kilichokuwa kinaendelea!
-kupakana upupu kwenye nguo- ukizubaa mnapo ogelea nguo zako zikipakwa utakubali shoo yake- unaweza rudi nyumbani uchi...