Tuliowahi kuchunga wakati tukiwa wadogo tukutane hapa

Hakuna mfugo uliokuwa unanikera kama mbuzi kipindi tunachunga..mbuzi wetu hao sijui walikuwa ni mbuzi wa aina gani,ukienda nao maporini huko wanakupa kashkash sana , Mara mbuzi ishrini wamekimbia vle,kumi wameingia mashambani yan tafrani tu walikuwa hawashib sijui na huku una kazi ya kufanya umepewa shuleni inabidi uifanye huko huko machungoni mana ukirudi bomani kwenu hamna uhakika wa kusoma kwani taa ni moja tu na labda utumie na kuni za jikoni...ila porini ilkuwa raha kwa kiasi chake michezo na matunda ni bwerere,shida wengine ilkuwa ni kusoma halafu muda huo huo unatakiwa uchunge mbuzi kibaooo....
 
Machungani 'tumebada' sana panzi, tega sana ndege na samaki (mumi/kambale), winda sana kware... tumeiba sana viazi na miwa.

Raha iliyoje kuchunga na mademu, ni zamu kwa zamu tu... kazi yako ni 'kuwanyamilija' tu unapewa tunda!
 


Wewe hujui sababu ya watu kuitwa wanakondoo wa Bwana na sio Wanambuzi wa Bwana???!🤣--- mtu yeyote aliyewahi kuchunga mbuzi maishani basi mtu huyo lazima awe mvumilivu katika maisha yake.

Mbuzi ni balaa.
 
sitasau siku ambayo niliona uvivu kuchunga ng'ombe nikaamua niwakatie majani wale ndani maana walikuwa wachache, kasheshe ikaja nikapita mahali kumbe ni bwawa ila juu mina mihani inakuwa kama miti imejifungafunga ina utomvu sana.

katika kutembea nikatumbukia mahali uzuri niliwaki kusambaza mikono juu ya yale majani kujishika lkn wakati huo kichwa, mikono na mabega tu ndio nipo juu, na kuanzia kiunoni kwenda miguuni ni maji tu.

nilikuwa mwenyewe nilipambana hadi nikatoka kumbe pale mahali watu wanakuja na panga wanakata yale magugu alafu upana fulani alafu wanaweka ndoano ili kuvua.
 
Karibia kila aliyewahi kuchunga amekutana na hizo tamu na changamoto za kuchunga.
Binafsi kwetu kulikuwa na wachungaji lakini tulikuwa tunatoroka tunawafuata malishoni.
Mimi nilikuwa napenda kuona yule fahari (Nzagamba) akiwapiga madume wa makundi mengine ya ng'ombe.
Pia kula matunda ya asili pamoja na kuwinda.
Kero kubwa ilikuwa nyakati za mvua hasa inayonyesha kidogokidogo kwa muda mrefu (nzumbi)
Shule ilinifanya nichukie kuchunga kabisa mpaka leo sipendi!
 
Aisee kero ya kuchunga ni ifike kwanzia saa nane Hadi saa kumi jioni kuna vi inzi huwa vinasumbua masikioni na machoni,halafu sasa ukute mbuzi wanasumbua,huku punda Wana ng'atwa na jamii flani ya nyuki halafu wanakimbia hovyo aisee utajuta.

Raha ya kuchunga ni Kula matunda porini,kunyonya maziwa ya ng'ombe uchungajini,kupanda punda wakati wa kurudisha mifugo nyumbana nk.
 
Tumechunga sana kwenye majaruba ya mpunga kule Sengerema mwanzoni mwa miaka ya 90. Life ya kuchunga was so awesome.... Many things were happening including kukutana na wanyama wakali kama nyoka pamoja na kuzama mtoni.
Wewe bila shaka ulikuwa unachunga ng’ombe wa shule SESESCO
 
Maisha ya machungani yalitujenga ukomavu unakutana na changamoto ya mifugo kula mazao ya watu mhusika anakulamba stick unarudi maskani kama hakuna chochote kilichotokea manake kosa hilo kama ni mpirani sawa na beki kuokoa mpira kwenye 18 kwa mkono
 
Machungani 'tumebada' sana panzi, tega sana ndege na samaki (mumi/kambale), winda sana kware... tumeiba sana viazi na miwa.

Raha iliyoje kuchunga na mademu, ni zamu kwa zamu tu... kazi yako ni 'kuwanyamilija' tu unapewa tunda!
"kuwanyamilija tu"[emoji3][emoji3]usukumani raha sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenikumbusha mbali, tulishawai kuteka wapitanjia wadada wawili na kuwarazimisha watoe mzigo hapo fimbo zipo barabarani tumeweka madogo miaka minne tu wakawasimamisha ss tumejificha wakawaamuru wawasalimie wakagoma baadae biti mmoja akakapiga kammoja tukatokezea wazee wa kazi chini ya ulinz fimbo kama tano za mgongo tukaamuru watupe mzigo mbona walishalegea wameanza kuvua akatokeza mtu mzima tukala kona ndo ilikua pona yao.
 
Ufugaji wa namna hii mara nyingi Kanda ya ziwa mikoa mingine kwa wamasai,, yaani nimekumbuka mbali sana! Maisha yale niliyafurahia sana kwa kipindi chote kile,,wazee wa lubaga mpo???
 
Tumechunga sana kwenye majaruba ya mpunga kule Sengerema mwanzoni mwa miaka ya 90. Life ya kuchunga was so awesome.... Many things were happening including kukutana na wanyama wakali kama nyoka pamoja na kuzama mtoni.
Kizugwangoma,mwabaluhi,mwabayanda nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…