Mwaka 2013 nilikuwa natumia line hii 071X008580. Kuna deni nilikuwa nadaiwa kama Tshs.35,000/-, Nikamtumia mdai wangu kiasi hicho mida ya saa tano usiku, Sikupata meseji yeyote ya uthibitisho, kuwa ujumbe wangu umefika kwa mlengwa japokuwa salio langu lilikuwa limekatwa tayari, na nilipojaribu kupiga call centre niliambiwa kuna tatizo la network mafundi wanajaribu kulitatua, nitapata mrejesho baadaya ya masaa 24. Ilinibidi nizisubirie hizo saa, japokuwa mdai wangu alionyesha kama kutoniamini kwa kile nilichomwambia...baada ya masaa hayo kupita sikupokea ujumbe wowote..Nilifuatilia takribani mwezi bila ya majibu yenye uhakika..zaidi ya tatizo letu la kiufundi likitatulia utaona ujumbe huo mfupi. Nizungumzavyo mpaka leo sikupokea ujumbe wowote na hela yangu ilikatwa. ilipita mwaka sikuwa na imani tena na hii kampuni...Mpaka leo siitaki hata kuisikia...Majuzi nilipiga hiyo namba yangu ikapokelewa na bidada mmoja nasikia yupo mbeya.
Sent using
Jamii Forums mobile app