Tuliowahi kudhulumiwa na Mtandao wa Tigo Tanzania tukutane hapa

Mwaka jana mwezi wa 11 nilinunua kifurushi cha tigo 5000 kwa njia ya tigo-pesa mpaka leo sijapata hiyo huduma nimepga huduma kwa wateja mpaka leo naambiwa 24hrs
Huu ndio mchezo wao Mimi naugulia kwa zaidi ya wiki 2 sasa
 
Naamini TCRA watapita katika uzi huu na kujiuone vilio vya Watanzania wachache tunaowakilisha wengi walionje ya JamiiForums
 
Kumbe hili janga ni kubwa. Tigo jitokezeni mtoe majibu ya utapeli huu
 
Mzee si unaona nimeweka hadi tarehe? Unadhani sijui ninachoandika
 
Kumbe ndio dawa yao
 
Na Mimi jana nimeunga bundle la Internet kupitia Tigo Pesa hadi leo sijapata na Huduma kwa Wateja wanasema wanashughulikia najua ndio imetoka hii
 
Na Mimi jana nimeunga bundle la Internet kupitia Tigo Pesa hadi leo sijapata na Huduma kwa Wateja wanasema wanashughulikia najua ndio imetoka hii
Pole sana Mkuu, karibu tuungane kufichua utapeli wa Tigo Tanzania
 
Hata Vodacom Wana tabia ukifuatilia wanakupiga kalenda.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
daaahh pole sana rafk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tarehe hiyo hiyo mimi nimenunua luku 10 000 sijapata token wala hela haijarudi nimekua nikipiga simu kila siku mpaka customer care wakanitukana na uzuri nimewarikodi so kama kuna njia yeyote ya kupata haki yangu nijulishe nasubiri wanirudishie tu hela yangu ili nikafute usajili
 
me nilikwangua vocha vibaya nikawapelekea mwaka 2O13 nikaja kupigiwa simu ya kupewa vocha yangu mwaka 2O19 hata nilishasahau hivyo hata wewe vumilia tu,issue yako itasovika tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mimi na kampani yangu soootee tumeshajitoa tigo ni bora KUBAKI BILA MAWASILIANO KULIKO KUWA NA TIGO na ndio maana tumehamia 073 home sweet home
 
me nilikwangua vocha vibaya nikawapelekea mwaka 2O13 nikaja kupigiwa simu ya kupewa vocha yangu mwaka 2O19 hata nilishasahau hivyo hata wewe vumilia tu,issue yako itasovika tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaaa serious? 2013 had 2019 mbona wana utani hawa watu.

Bas wacha niwasubrie siku wakinikumbuka watanirudshia hela yangu
 
Nilinunua kifurushi cha mini Kabang cha Sh 650 kupitia TIGOPESA, wakaja kunikata shilingi 8000. Yaani nimenunua mara moja, ila zinaingia SMS kadhaa za TIGOPESA muamala kila moja imemega salio hadi ikafika 8000.

Ilikuwa mwaka 2015 hii, nikajaribu kuwasiliana na huduma kwa wateja kupitia facebook maana kuwapigia hadi waje wapokee ni majanga. Huko wakaniambia wanashughulika nalo, ila sikuona lolote. Nikiwa nikija kuwakumbusha kuhusu hela yangu, halafu mtu mwingine yeyote akireply comment yangu wanamjibu. Ila kwangu wanauchuna kama vile hawakuiona. Tena kidharau


Nilikuja kulalamika miaka miwili baadaye yaani 2017 nikawatajia hadi mwezi tatizo lililotokea wakaniambia watanipigia simu ila hadi leo kimya.

Kiukweli namiliki line ya Tigo tu kwasababu ina watu wengi wanaijua na ndiyo namba yangu kongwe, ila isingekuwa hivyo ningekuwa nishabadili natumia line na kuivunjilia mbali

Halafu huduma kwa wateja wana mwanamke akipokea, sijui ana ugomvi huko alipotoka. Nakumbuka mwaka 2016 nilipiga nilipopata tatizo la kifurushi kupitia TIGOPESA, nilijibiwa kimkato tena kwa kisirani kisha simu ikakatwa. Yaani kama vile unamsumbua mwanamke kwa kumtongoza, akaamua kukukatia simu. Ndiyo alichofanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…