Tuliowahi kufukuzwa kazi tukutane tupeane experience

Sijui huwa ni nini unapokuwa huna kazi utasota kupata kazi, ukiwa nayo tu ofa zingine za kazi zinakufuata.

Ndiyo hapo utaelewa kuwa mwenye nacho huongezewa.
 
Aisee hii thread imenigusa imebidi nijiunge na jamii forum baada ya kuwa guest kwa miaka takriban 7.
Ipo hivi mwaka 2014 nilimaliza chuo na kupata degree ya Marketing.basi bwana nikakaa home mpka 2015 mwezi ya tano nikapata kazi kwenye hoteli moja jina nitalificha five star kule Toure Drive Oysterbay Wahindi kibao tena wengine hawana vibali wanakuja tz hawajua kiingereza wala kiswahili na kuwekwa humohumo ndani ya hoteli hawatoki hata njee hadi mahitaji kama ya nguo wanaomba waswahili wawasaidie kununua kko mimi na degree ya marketing niliingizwa miezi mitatu wanione kama nafaa au la basi nikafanya kazi miezi mitatu kimya sioni dalili yoyote ya kutoswa siku ya siku ya kumaliza miezi mitatu naambiwa kwaheri nikauliza sababu sikupewa, aliyenifukuza hata si HR. ni mdada Msouth Afrika machozi yalinitoka nakujiona sina bahati. baadae nafata mshahara wangu maana mshahara wa tarehe 30 unalipwa tarehe 7 mwezi unaofata Hr mdada mswahili ananiambia wewe si ulimtolea njee Msouth wa kiume. dah,kusema ukweli huyo msouth wa kiume hakunitongoza ila alianza mazoea ya kishenzi nikamkazia .fast forward 2016 nikapata kazi mshahara mara tatu zaidi ya kule na baada ya miaka miwili nikaacha mwenyewe kujiajili na pesa kidogo nilisave huku nyingine Mr akinipiga tafu.
Lesson. usikatishwe na tamaa juu ya hawa binadamu maana kama ningebaki pale huenda ningechelewa kufika hapa nilipo.
Nb.kama itatokea umeenda sehemu za hoteli kubwa kubwa usiagize chakula chenye samaki,kuku,sambusa maaana mara nyingi huwa si fresh aisee ile hoteli ilikuwa ina samaki kwenye fridge wa miezi hadi 6 huwa si fresh kama unavyodhani bora ule kwa mama ntilie.
 
Hapa mwisho uneongea nukta muhimu sana.
 
Nimejifunza kitu aiseeee
 
Haya mavyakula yanakaa kwenye freezer miez 8 ndo wanatuandalia eti buffet....[emoji848][emoji848]
 
Sio kule ulikimbia baada ya boss kukuambia umfanyie massage?
 
Pole sana mkuu,
.. Waafirka sisi ni wapumbavu sana
 
Kiongozi hii thread yako imenikumbusha machungu Makubwa sana.

Nilivomaliza chuo nikapata sehemu ya kujishikiza bn, nikapiga kazi miezi mitatu tu nikapandishwa hadhi kidogo bana. Kazi ikaendelea, baada ya Mwaka mmoja kuisha, Kiongozi mmojawapo katika ofisi yetu akapa nafasi ya kuajiriwa serikalini, kampuni ikanipa nafasi yake. Kumbe ile hali wenzangu ambao tulikuwa tunafanya nao kazi walichukia sana. Why me?

Sijawa na hili wale like, mdogo wangu akauugua, wadogo zangu wengine walikuwa wanasoma bado secondary, so ikabidi nichukue likizo ya siku 14 kwanza nikamuuguze, bahati mbaya haikuwa riziki akafariki. Baada ya kumaliza matanga, nilirejea kazini, lakn haikuisha hata mwezi mama akaugua.

Akapelekwa hospital, akawa anakaa na dada yangu, kila wikend lazima niwe huko, nikalazimika kumhamishia kwangu (getho) pamoja na sista, afu Mimi nikawa nalala kwa mpangaji mwezangu msela. Uguza weee, hadi hela ikakata. Kazi nikiwa naendelea nayo lakini.

Basi bana nakumbuka ilikuwa Tarehe 1/10 tukaenda kuchukua mshahara, nilivyofika kwa mhasibu akanipa mshahara wangu na barua. Kuifungua, eti nimeachishwa kazi!

Kosa silijui. Basi ile hela yote nikamtibia mama, lakini haikufua dafu. Nikauza kabati la nguo laki 100,000/, nikauza sofa langu elfu 70, latop hp, 150,000,, uza king'amzi na TV, na dish lake 170,00, friji 70,000 nikaendelea kumtibia mama. Nilivyoishiwa kabisa, mama akapona!

Basi tukarejea kijijini, nikaanza kulima nyanya. Nikipeleka maombi ya ualimu hata shule za kata nakataliwa! Naambiwa nitaitwa lakn siitwi. Nyanya hakuna wanunuzi. Ikabidi nianze kuvua samaki, lkn wapi.

Wale watumishi wenzangu hata hawapokei simu yangu, kila surauali sasa hainitoshi, mwonekano umeshazidi umri wangu halisi. Nimezeeka balaa.

Sema ndo hivo siku hazifanani, nilikuja kupata pa kujishikiza na maisha yanaendelea. Lakn ukweli kuamka bila kujua pa kwenda ni shida.
 
Sasa sabb ya kufukuzwa ilikuwa ni nini?[emoji848]
 
Sasa sabb ya kufukuzwa ilikuwa ni nini?[emoji848]
Hadi leo sijui sababu witnessj. Nafikir kuna mjinga mmoja alikuwa ananichawia. Maana sikuwa na kosa lolote kabisa.

Bahati mbaya na hiyo taasisi yao ilishakufa , iliniuma sana kusikia wamefilisika, kwa sababu pamoja na kwamba walinifukuza bila kosa lolote lakini ni ukweli kwamba walinisaidia kupata pa kuanzia.
 

Hilo jibu ulilompa boss wako mi hoi [emoji23]
 
Kuna mfanyakazi mmoja ameachishwa kazi baada ya kupata msiba watu wameenda kumpa pole kufika wakakuta mjengo wa maana
Alivyorudi kazini anaulizwa hela ya kujenga nyumba kama hii kaipata wapi

[emoji23] binadamu hatupendani mweeee
 
Alikuwa akiumia hata ukivaa nguo mpya ofisini wanamjua waliowahi fanya nae Kazi kabla.Kuna libosi limoja lilikuwa likiumia mkila kuku ofisini.Image mtu anaumia ukila kuku au kuvaaa nguo mpya ofisini atashindwa vipi kufurahi ukifukuzwa Kazi

Duu huo muda mpaka wa kuhesabiana nguo hadi ujue leo huyu kavaa nguo mpya watu huwa wanatoa wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…