Tuliowahi kufukuzwa kazi tukutane tupeane experience

Katambi ni jamaa yangu. Lakini tangu apate uongozi amekuwa mtu wa hovyo sana. Hata simu hapokei wala texts hajibu. Sijui huwa anadhani nitampiga mizinga πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Akili za kishamba sana
 
Mazoea ya wafanyakazi wenzako yaishie bar au kwenye nyumba za kupanga au kwenye kota na sio kuwapeleka kwenye bangaloo lako.Chuki na ubinafsi ni asili ya binadamu.Yeye yupo bize na kufungua zipu na vizibo vya bia wewe upo bize na mfuko wa cement Katu hawezi kufurahi.Wewe unakopa kwa maendeleo yeye anakopa kwa ajili ya zipu, kesho atakuchoma utahamishwa,fukuzwa,nk.

Kuna mtumishi alipata msiba wenzake wakaja kumpa pole baada ya mda kupita kijiti cha uhamisho kikamkuta.Boss yupo bize anashinda kukagua sketi wewe upo bize kuangalia vitu vya ujenzi kwenye hardware ni lzm akuumize.
 
Nikisoma komenti za humu jinsI wadau walivyoteswa na mabosi zao ninazidi kumshukuru sana boss wangu Chudasama wa kampuni niliyodumu nayo zaidi ya miaka mitano na boss wangu Tumaini nilikodumu zaidi ya mwaka mmoja, wamekuwa mabosi wema sana kwangu, Mungu Awape miaka mingi na mafanikio tele!!!

Kikubwa tu wakuu kufanya kazi kwa weledi na kuacha mazoea yaliyozidi kwa mabosi ama wafanyakazi wenza.
 
Kuna ndugu mmoja anapiga kazi kwa wahindi, Sasa anacheza na akili zao balaah!

Huyu jamaa kaporomosha mjengo mmoja hatar, na ana maduka mawili , Yan la bidhaa za kawaida na hardware, Sasa wahindi huwa wanatabia ya kutembelea wafanyakazi wao, ikifika zamu ya jamaa kutembelewa na maboss wake anaenda kwenye family moja jirani yake Kuna kijinyumba Cha slope chumba na sebule, anaweka viti vya kukunja na vijistuli viwili na meza ya Kiana, basi mda ukifika wale jamaa wanakuja anawakaribisha pale, Basi jamaa wanafrahia saanaah, wanamsifia eti ni mwaminifu Kwan Kila wakienda wanakuta hali ile ile, Hawa jamaa jinga sanah!
 
Ukiona unapedwa Sana bosi lazma uwe na vinasaba vya unafiki na umbea
 
Ndo maana nikasisitiza hili...kamwe co-worker asikanyage kwenye mjengo wako naongea haya thru experience [emoji848]

Hapa kuna bosi mmoja alifiwa na mamaake mzazi, ila akasingizia ni Bibi ake kafa hukoo kijijini kigoma kumbe msiba uko kwake kurasini (ni rafiki angu ndo maana mi nilijua)hataki kusikia habari za wafanyakazi na mabosi wenzake kukanyaga kwake
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787]...nimeipenda hii sijui niige kudadeki[emoji848][emoji848]

Jamaa alifukuzwa kazi kisa eti kavaa suti kwenye kiwanda cha mhindi asee ( alitusimulia)

Hivi wahindi sidhani kama ni binadamu [emoji848]
 
πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ Niliacha bila kumweleza mtu yoyote.Walipiga sana simu na vitisho juu.
 
Hawa jamaah inatakiwa uwe na akili kuwazidi, utatoboa TU,

Na SI wahindi tu, Kuna Mwamba tulikua tunapiga nae job Mahal , ikatokea from no where akatimuliwa Kama mbwa, imagine mbele ya staff na wateja kwa ujumla, cha ajabu Kuna baadh ya staff members walikua wanamnanga kinyama, ukapita mwaka mmoja, jamaah akarudi kutupa hai pale akidrive kwenye ndinga lake, jamaa hawaamini macho yao!

Kila kitu kinatokea kwa sababu, na hasa kumpandisha mtu!
 
Kuna mfanyakazi mmoja ameachishwa kazi baada ya kupata msiba watu wameenda kumpa pole kufika wakakuta mjengo wa maana
Alivyorudi kazini anaulizwa hela ya kujenga nyumba kama hii kaipata wapi
Ni kweli kabisa hili lipo wazi taasisi nyingi za kidini sio zote wana hizi tabia sana.
 
Alikuwa akiumia hata ukivaa nguo mpya ofisini wanamjua waliowahi fanya nae Kazi kabla.Kuna libosi limoja lilikuwa likiumia mkila kuku ofisini.Image mtu anaumia ukila kuku au kuvaaa nguo mpya ofisini atashindwa vipi kufurahi ukifukuzwa Kazi
Mkuu kuna sehemu unavaa nguo aina moja mpaka ikapauka wakaanza kusema ooh ona hii mbona sasa inakuwa hivyo.Jibu dogo tu sina hela..nasubiri nichangiwe ninunue mpya.Kiatu mpaka imefeuka mwendo mdundo...
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]jamaa alimtolea uvivu bosi mkuda
 
Dunia imejaa magap.
Jamaa alikua na kazi tatu puani kwake wakati mimi sijawahi kupata kazi hata moja na leo kijiweni (car wash) sijaosha hata gari moja, na bachelor ninayo tena ya Mathematics.

Kazi tatu puani akati jamaa yangu mmoja niliesomanae Math's anafanya internship TRA mwaka wa pili huu analipwa laki tatu kwa mwezi. Maisha haya.

Sio wivu ila naoanisha tuu kwamba ndugu yangu wakuzaliwa nae ana miaka sita tangu agraduate hajawahi kupata ajira. Amekata tamaa, amenunua nusu eka kijijini anataka akakae huko kwenye makuti.

Wanasemaga tuendelee kunywa mtori..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…