hahaha umenikumbusha mbali sana, kuna kampuni moja niliajiriwa pale ile kampuni ya jamaa flan kutoka ASIA, aise sio siri watanzania wananyanyasika nchini kwao. yule jamaa anafoka sana, tena kilugha chao, nikauliza maneno anayosema nilitamani siku moja nimtukane pia ila kwa kuwa nilikuwa pale kwa sababu, mshahara laki 900k nakuja yote after makato. ila nilishindwa ile kazi , miezi 3 niliona mwaka hahaha. hakuna kuumwa, ukiumwa unakatwa mshahara, dada akipata ujauzito anafukuzwa kazi, wazee wanatukanwa, mimi kilinisaidia elimu yangu tu
baadae alikuja kunikufukuza kazi, bila hata barua wala nini, hapo ndipo aliponipa nafasi ya kujipatia hela nyingi coz alinifukuza nikiwa ndani ya mkataba miezi 6 mbele na kwa kosa la kipuuzi . nimeomba ruhusa, akanipa, narudi anasema nimechelewa kazini, nafasi yangu ina mtu tayari, go home yaan hapo hapo on the spot bila hata kujitetea. nikasepa zangu home, nikawacheki mawakili, kazi ikaanza. mshenzi yule adabu aliipata.
n mbaya zaidi akanikata hela kwa siku mbili ambazo sikuwepo, hapa alinipa hasira za kwenda kwa mawakili fala yule. n wakati ananifukuza nilikuwa pia na kazi nyingine ya online ambayo kule pia nilikuwa na kitengo kizuri tu , hivyo life kwa muda ule halikuwa tight.
Ila wazee, tukijiajiri, TUFANYE KAZI KAMA VILE TUMEAJIRIWA PIA, YAANI NASEMA HIVI, UKIAMKA ASUBUHI UFIKE KAZINI KWAKO, UKICHELEWA USEME UTAFUKUZWA KAZI, USIPOFUNGUA OFISI WAZA BOSS ATAKUFUKUZA KAZI.