Tuliowahi kufukuzwa kazi tukutane tupeane experience

....nyama tutazikuta chini[emoji848][emoji848]

Ila pole mkuu dunia haiko fair at all
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hii nchi kumbe tuna matatizo makubwa kuliko tunavyofikri?
 
hahaha umenikumbusha mbali sana, kuna kampuni moja niliajiriwa pale ile kampuni ya jamaa flan kutoka ASIA, aise sio siri watanzania wananyanyasika nchini kwao. yule jamaa anafoka sana, tena kilugha chao, nikauliza maneno anayosema nilitamani siku moja nimtukane pia ila kwa kuwa nilikuwa pale kwa sababu, mshahara laki 900k nakuja yote after makato. ila nilishindwa ile kazi , miezi 3 niliona mwaka hahaha. hakuna kuumwa, ukiumwa unakatwa mshahara, dada akipata ujauzito anafukuzwa kazi, wazee wanatukanwa, mimi kilinisaidia elimu yangu tu

baadae alikuja kunikufukuza kazi, bila hata barua wala nini, hapo ndipo aliponipa nafasi ya kujipatia hela nyingi coz alinifukuza nikiwa ndani ya mkataba miezi 6 mbele na kwa kosa la kipuuzi . nimeomba ruhusa, akanipa, narudi anasema nimechelewa kazini, nafasi yangu ina mtu tayari, go home yaan hapo hapo on the spot bila hata kujitetea. nikasepa zangu home, nikawacheki mawakili, kazi ikaanza. mshenzi yule adabu aliipata.

n mbaya zaidi akanikata hela kwa siku mbili ambazo sikuwepo, hapa alinipa hasira za kwenda kwa mawakili fala yule. n wakati ananifukuza nilikuwa pia na kazi nyingine ya online ambayo kule pia nilikuwa na kitengo kizuri tu , hivyo life kwa muda ule halikuwa tight.


Ila wazee, tukijiajiri, TUFANYE KAZI KAMA VILE TUMEAJIRIWA PIA, YAANI NASEMA HIVI, UKIAMKA ASUBUHI UFIKE KAZINI KWAKO, UKICHELEWA USEME UTAFUKUZWA KAZI, USIPOFUNGUA OFISI WAZA BOSS ATAKUFUKUZA KAZI.
 
Mkuu uliwafanyaje hao wa asia

Advocates walifata procedure zipi na outcome ilikuwaje?
 
Mkuu uliwafanyaje hao wa asia

Advocates walifata procedure zipi na outcome ilikuwaje?
kuna tararibu za kumfukuza kazi mtu, huwezi kumfukuza kazi mtu bila ya onyo wala kumuita ktk katika kakao cha maadili, so hapa sheria ilikuwa inanilinda, umenipa ruhusa, na bado unanifukuza. taratibu zipo kama kumwandikia barua ya madai, hapa wakili wako asiwe na njaa maaana mawaili wengine sio waaminifu, anaweza kwenda huko akapigwa mpunga akaishia kukuambia kesi huwezi toka wakati sheria inajieleza na ipo wazi. outcome yake nilipata hela haki yangu. bahati nzuri wakili ni rafiki yangu, mbuzi alifia kwa muuza supu

kuna kesi kama hii ilitokea pia kwa rafiki zangu, walifukuzwa kazi ikiwa bado miezi mitatu, mwenye kampuni anasema kampuni inajiendesha kihasara. unafukuza mtu bila ya kumpa notice, hii kampuni ilikuwa kampuni ya nje, jamaa aliishia kulipa hela miezi 3, hela ya likizo sujui surveillance pay na cheti cha utumishi na hii ni ndani ya wiki moja tu aliwapa hela zao kwasabau pia jamaa alikuwa na makando kando akaogopa tena enzi za mzee Marehemu ndio kabsaaaa

n kwa kua adabu alishikishwa, next time alipotaka kufunga kampuni alifuata taratibu

ukiwa sahihi hawa waajiri utawashinda kesi.
 
Niko private. Niko kazini toka saa 1:30 asubuhi. Ninavyoandika sasa hivi ni saa 1:13 usiku/jioni ndio kazi za leo zimekwisha. Nafanya kazi kama punda lakini mwisho wa mwezi ukifika, machungu yote yanakwisha. Karo za watoto, bima, nk wanalipa. Wenzangu wa serikalini wanasema wana usalama wa kazi na wanatoka kazini kadiri wanavyojisikia lakini mwisho wa mwezi kamshahara hakafiki mwisho wa mwezi. Mshahara wangu wa mwezi mmoja, baadhi yao watafanya kazi mwaka mzima ili kuupata. Watoto wao kusoma kwenye shule nzuri ya binafsi ni ndoto. Kwa hiyo chaguo ni lako.
Haya maisha sio ya kubweteka na kaajira ka private unafanyishwa kazi zaidi ya masaa 8 kwa siku na hakuna cha mafao wala nini.
 
Huku kazini kwetu wao wameanzisha utaratibu wa kutoa mikataba ya miaka miwili miwili

Mkataba ukiisha wanakuandikia barua ya kutokukuongeza mkataba

In that case unakua huna ubavu wa kusema umefukuzwa kazi
 
Huku kazini kwetu wao wameanzisha utaratibu wa kutoa mikataba ya miaka miwili miwili

Mkataba ukiisha wanakuandikia barua ya kutokukuongeza mkataba

In that case unakua huna ubavu wa kusema umefukuzwa kazi
Ni watu wote wanafanyiwa ivyo au baadhi? Ina maana kampuni haina watu wenye zaidi ya miaka miwili kazini? Je kila mwezi kuna staff wanaondoka na wanao ajiriwa? Maana naamini mikataba ya watu huisha miez tofauti tofauti. Hebu nijibu apo kwanza
 
Mbona Zanzibar hawapo?
 
Kampuni nyingi za kizungu ziko vizuri sana regardless ya uswahili wa waajiriwa wake.

Sisi watu weusi aliyeturoga ni yule aliyechungulia uchi wa baba yake maanq zake.
Ushafanya kazi na wataliano?
Nilifanya kazi nao hawana tofauti na waswahili, Mtoto wa mwenye hotel na Gm wake wananikubali sana toka na utendaji wangu, ila huyo mzee mwenye hotel ni kichefuchefu hanipendi hataki hata kuniona, akinikuta sipo eneo la kazi anauliza nimekwenda wapi? Atajibiwa niko kwa HR atanifata kuhakikisha kama kweli niko kwa HR, na akinikuta aongei lolote ataniangalia nafanya jambo langu mpaka namaliza ananisindikiza na macho. Anaweza akaja eneo lako la kazi akavuta kiti akakaa akakukodolea macho hata nusu saa nzima halafu asiseme lolote akaondoka(na kukutazama kwake unaona kabisa ni kwa chuki)
Anatembea na tarehe ya mwisho ya mikataba ya watu asiowapenda, then kila asubuh akikutana na anao wapenda(hasa wadada)anawaonesha huyu na huyu mkataba wake ukiisha siwaongezi ni akaza(nyumban).
Kisa cha kunichukia nimenenepa ni tofauti na nilivyokuja nilikua mwembamba.

Siku 14 kabla ya mkataba kuisha nikiwa kwenye staff bus nikawaza nikiziona hizo siku ni nyingi kama mwaka, sikuona haja ya kuendelea na hiyo kazi, nikashuka getini nikadaka daladala nikarudi nyumbani. Siku tatu mbele nikadaka kazi nyingine.
Ilikua 2013
 
.

.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…