Tuliowahi kufukuzwa kwa watu/kwa ndugu tukumbushiane ilikuwaje

Wengine tu matendo...nimetoka zangu kijijini nikaenda mjini kumtembelea uncle...ukipakuliwa ugali kwenye hotpot wanakukaribisha mezani halafu wao wanabaki wakizugazuga...unaambiwa kapakue chakula...ukiangalia chakula cha kula peke yangu nisishibe naambiwa niwaachie na wao...basi nikawa nakula kidogo halafu naingia kwa mama ntilie nashindilia nguna ya kutosha...kwa watu hakufai
 
Hahahaha unafanya vitu kibabe sana, ndo uanaume huo
 


Haha baada ya kufanyiwa ukatili nyumbani kwa baba mkubwa, na ww ukaenda kuhamishia kisasi chako kwa mama Mdogo wako snowhite
 
Safiii
 
nimejikuta nimekupenda tu aiseeh. Wewe dhujaa sana. Binadamu wengi hatuna imani aiseeh.
 
Haloooo... Nimekuvulia kofia.
Ila damu ni nzito kuliko maji ati. Inauma sana ndugu yako akiteseka.
Mdogo wangu akiadhibiwa hata na wazazi huwa naumia sana sasa sijajua mtu back itakuwaje.
 
Hivi hao (kwa watu) ni wakina nani?
Utashangaa na hao (kwa watu ) mnaowazungumzia wamewatesa na hao wanakuja hapa kuhadithia walivyoteswa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].
Huu Uzi nimecheka sana ngoja niuweke alama.
 
Nilikaa kwa mama yangu mkubwa, nilikuwa mchapakazi sana, alinipenda mno. Mwanae akaona wivu akaanza kumpelekea maneno ya uongo.. Sikujali. Baadae niliondoka km vile hawanijui hata kunisindikiza tu stand na nilikuwa mgeni ilikuwa shida, nikaondoka kinyonge nikilia gari zima. Nakumbuka ilikuwa Air Jordan Mwanza - Arusha

Nimekaa kwa shz na uncle, natimiza tu wajibu wangu kma
Kufua nguo za nyumba nzima,
Kupika,
Kudeki
Vyombo,
Bustani nk.. Bila kusahau kufundisha watoto.
Nilipendwa saaaaana!! Na km walikuwa na vi element vya kuninyanyasa, wanashindwa sababu nachapa kazi haswa, hata hivyo, sikusahau kuwapenda sana, binamu zangu maana ndio mioyo ya ndugu zangu, ukitaka kumshika MTU pabaya PENDA MWANAE.... Haya shemeji yenu na mid tukajifanya Twapendana km Adam na Hawa, nikapata mimba..ohooooo!!!! Naishipa hapa. MUNGU NI WA WOTE, WENYE DHAMBI NA WAKOSEFU, MASIKINI NA MATAJIRI.
 
Hivi hao (kwa watu) ni wakina nani?
Utashangaa na hao (kwa watu ) mnaowazungumzia wamewatesa na hao wanakuja hapa kuhadithia walivyoteswa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].
Huu Uzi nimecheka sana ngoja niuweke alama.
[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Humu ndani hapajawahi kupotea kitu, halafu ww ndo mgeni ndo kwanza una siku nne.
 

Umenivutia. Sipendi unafki na hasa issue inayoniumiza, provided humtukani mtu. Japo ni vizuri kuwa na kiasi lakini uwe na msimamo. Hongera mama.
 
Mimi nilikaa na Ndugu yangu.
nilimpenda mno, Nilikuwa najinyima Ili yeye apate.
yeye alikuwa hana kazi me ndo Nilikuwa na kazi.
nilijitahidi sana kumtimizia mahitaji yake. Japo me ni mdogo yeye mkubwa.

Kuna siku alikuwa anachati na ndugu zangu wengine. Anawaambia me namnyanyasa,
Kibaya zaidi dada zangu wakawa wananifwowadia SMS zake zote alizowatumi.
Sikuamini yaani.
Fikiria mtu unarisk maisha yako Ili mtu Fulani ale vizuri na kuishi vizuri, Kisha akuseme vibaya kwa nduguzo. Iliniuma sana.

Nikashtukia tu kwangu kahama. Mpaka leo sitamani kuishi na ndugu Yoyote yule.
Ndugu ni lawama sana..
 
We ni binti jasiri sana.

Safi sana
 
Haloooo... Nimekuvulia kofia.
Ila damu ni nzito kuliko maji ati. Inauma sana ndugu yako akiteseka.
Mdogo wangu akiadhibiwa hata na wazazi huwa naumia sana sasa sijajua mtu back itakuwaje.
Alifanya vyema na haki saaana.
Mimi shule walizosoma wadogo zangu kote walinijua, nna kamwili tu ka kinyonge lakini walipowatendea visivyo wadogo zangu vurugu lake kila kitu kinasimama hapo shuleni. Walimu wananichukia mpaka wenyewe wanaanza kunipenda.
 
Haha baada ya kufanyiwa ukatili nyumbani kwa baba mkubwa, na ww ukaenda kuhamishia kisasi chako kwa mama Mdogo wako snowhite
Nooo ,alikuwa anamtesa dogo!!
Imagine upon shule mtoto wa darasa LA sita anakuandikia barua hapewi chakula!
Upuuzi!!
Ilibid nirudi likizo despite nilikuwa na Necta ahead!!
Nikachimba biti,nikaenda shule!!
Nilivorudi nikakumbushia biti langu.
Mdogo wangu sa hiz
Mchukulie mwanamke atakuelewa,ukimmisstreat dadake ,ANAWEZA AKUFANYE MISHKAKI!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…