Tuliowahi kukopa pesa kuanzisha biashara kisha biashara ikafa tukutane tujadili machungu

Duh Kaka Mimi nakumbuka ilikuwa 2012..aisee Bora ningechukua viwanja tu..biashara Bila busta Ni kupoteza muda tu
 
Wengi wameingizwa Mkenge kwenye Biashara na wale Motivation Speakers..,
Yani ile unakuja kutahamaki bidhaa Dukani zimeisha, inabaki Leseni ya Biashara inakuangalia tu!!!
Kinachobaki ni kufunga na kuja night kutoa Mabango yenye Jina lako...!!!
Halafu anatokea mpuuzi mmoja anasema vijana mjiajiri πŸ˜… mie sina background yoyote ya biashara najiajiri vipi
 
Alafu ukute ulikuwa na ajira tena serikali ni na mambo yamekuendea mrama..marafiki wanakucheka ndugu wanakuona kituko mke anajuta kuolewa na wewe.....serikalini ushapigwa ban kurudi daaah.
Hapa kinachofata ni kifo cha BP tu maana mfariji wako nae malkia wako kakugeuka!
 
Duh Kaka Mimi nakumbuka ilikuwa 2012..aisee Bora ningechukua viwanja tu..biashara Bila busta Ni kupoteza muda tu
Tatizo wengi tuna mitaji fixed! Ukiwa na mtaji fixed lazma ile kwako! Biashara mwanzoni ina hasara hasara nyingi sana ila mtu akikuwasha gari kuwa biashara flani inalipa unaweza wehuka ukiskia mishindo anayopiga yeye unaskia mie hamna hamna sikosi laki 9 kwa mwezi humuπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…! Hapo mwenzio ana mwaka wa 3 kwenye ramani na wateja kila kona!

Unakurupuka kuanzisha bila kujua kuwa biashara inatakiwa ijenge wateja kwanza kisha baada ya muda ndio iweze kujiendesha yenyewe!

We unashangaa mwezi wa kwanza biashara inasuasua, wa pili, tatu, nne ndio angalau ina break even kuanzia wa sita pashazoeleka ndio unaanza kula profits sasa kidogo kidogo πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… sasa mtu kabla hajafika mwezi wa 6 pumzi imeishia njiani hana hela ya kuisupport business lazma ife tu!
 
Duh Kaka Mimi nakumbuka ilikuwa 2012..aisee Bora ningechukua viwanja tu..biashara Bila busta Ni kupoteza muda tu
Biashara lazma uwe na kipato cha ziada yani ndio maana ukichunguza wanaofanikiwa sana ni wale ambao ana biashara moja successful kisha akaanzisha nyengine πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… hawa kuanguka sio rahisi sababu hata sehem ikihitajika support biashara isiyumbe ana hela za faida anachota kule na kuweka huku mpaka inasimama yani!

Au mtu mwenye kazi nzuri ambayo ina disposable income ya kutosha akianzisha biashara ni mara chache sana kufa kama anaifatilia kwa umakini! Sababu ikitaka maboresho hela ipo! Mpaka inasimama vizuri na kuanza kujiendesha na kujilipa yenyewe ila graduate mpe duka la million 3 tu kisha asiwe na extra ale hapo hapo na nauli uone kama itamaliza mwaka shelf hazijabakia wazi!πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
mkuu katika hili watu wanaofanyikiwa ni wachache sana, wengi tunaangukia pua
Mie pia nilishafanya biashara ambayo inataka regular improvements! Ilikuwa mini bar nikaweka almost 3 millions! Ilikuja kunifia ile biashara acha tu πŸ˜‚ sikuamini! Ilifika stage mtu anataka safari unachukua creti la Klimanjaro na kwenda kubadilisha dukani πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Wanaongeaga kirahisi sana aisee! Maumivu yake kwa tuliowahi kujaribu business tunayajua
 
Just for curiosity mkuu...disposable income nzuri ni kuanzia shingapi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…