Yupo mzee mmoja tulifahamiana kupitia kazi zangu za udalali, siku moja akaniita tukutane baa moja mjini, kufika, mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo:
Mimi: mbona umeipa barabara mgongo?
Mzee: naogopa vishawishi hahahaaa
Mimi: hahahaaaa, shikamoo
Mzee: marahaba, umewahi vizuri, agizia kinywaji
Mimi: Waiter nipatie grand malta baridi
Mzee: Unajua nakaribia kustaafu, bado miezi miwili, nimetoka semina ya maandalizi ya kustaafu dodoma, wametueleza mambo mengi, nikasema nikirudi lazima nije niongezee na za kwako.
Mimi: Umeshazishika sasa?
Mzee: bado kijana, lazima uset mipango kwanza
Mimi: mipango sio matumizi mzee wangu
Mzee: najua, ila hiyo ni kwa vijana kama nyinyi, wazee kama sisi, ukiset umeset
Mimi: ulishajenga?
Mzee: kibanda tu cha vyumba vitatu kipo mkuranga, ila siwezi kimbia jiji kisa nimestaafu, tutabanana hapahapa
Mimi: mkeo anastaafu lini na yeye?
Mzee: yeye ni mama wa nyumbani, tuna watoto watatu, wote wameshaolewa
Mimi: kwakifupi huna anaekutegemea zaidi ya mkeo?
Mzee: haswaa
Mimi: mbali na ajira yako, una chanzo kingine cha mapato?
Mzee: ni hiyo nyumba ya mkuranga, nimepangisha, nachukua kodi, sina cha zaidi
Mimi: si haba, unadhani siku ya kwanza ukiamka na kugundua ulishakabidhi ofisi na hutakiwi uende tena ofisini kwako, ungependa urudi ulale au uamke ukafanye shughuli flani?
Mzee: bado nina nguvu, ningependa kwenda kufanya shughuli za hapa na pale, hususani za usimamizi, nisingependa niwe mtendaji sanasana
Mimi: kwahiyo kama baa hii ingekuwa yako, ungependa uwe meneja na sio mhudumu?
Mzee: haswaaaa
Mimi: umewahi kufanya biashara serious na ilikuwa na mtaji wa kiasi gani?
Mzee: hapo nyuma niliwahi kufuga kuku wa kisasa, nikaacha, sikuona faida yake kivile, wateja walinikatisha tamaa, mtu unampelekea kuku anakwambia mbona mwepesi hivi, nitakupa 3500. Walipoisha nikaachana nayo hiyo baishara
Mimi: Jenga kindergarten mzee. Tafuta walimu na wahudumu, gari la shule na dereva, inalipa mjini hapa.
Mzee: safi kijana, hilo wazo murua kabisa kabisa, sasa nikupe kazi, tafuta eneo, nije nilicheki, nitafute na fundi anichoree ramani, anipe na bei ya ujenzi, nijue itanikosti bei gani
Mimi: hapana, chukua kwanza hii namba, huyu mtu na yeye ana kindegarten mjini hapa, anazo tatu, yupo vizuri sana, ngoja nimpigie nimjulishe kuwa utamtafuta akupe mwongozo, ukishaelewa somo, ndio tuje kwenye utekelezaji. Au vp?
Mzee: haswaaa. Taifa linahitaji vijana kama wewe unajua
Mimi: ni kweli mzee wangu.
Nikapiga simu kwa tajiri mwingine, nikamweka sawa, nikampa namba na yeye, nikahakikisha wamewasiliana nikiwepo na kupeana apointment ya kukutana ili mzee akale somo ya namna ya kuanzisha kindercare yake, mimi huyoo nikasepa.
Wiki, mwezi, hatimaye mwaka ukapita mzee hakunicheki tena, miaka tano baadae nakutana nae stendi moja pembezoni mwa jiji akiwa ndani ya suti ya dereva wa daladala, aliponiona alitamanigi kulia, alikuwa amechongoka flani, na kapauka. Kwakifupi alinieleza namna alivyozipata milioni zake 185 za kustaafu na namna alivyozipukusa kwa kamari na totoz, nilimhurumia sana, kisha nikamkumbusha, nilikwambia mipango sio matumizi, akasema aaah ni ujinga wangu mwenyewe, yaani sasa nimeajiriwa kama dereva hapa basi tena.
185M ileeeeeeeeeeeeeee.