Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Huwa nawaonea huruma wazee wastaafu waliofilisika,unakuta alilamba M150.Halafu hazijafika hata miaka miwili zimeisha,kinachofuata n kuongea barabarani.
Ujue pesa ina shida fulani. Kama hujazoea kuimiliki, siku ukiipata ghafla lazima uchizike. Usipokuwa na adabu na pesa yako, itakutesa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2016 nilikuwa na m5 nikalima shamba nipande mahindi tulikuwa share mtu 2 tukalima acre 9 kimvua kikaanza tukapanda indi limetoka tu mvua ikakata tukapoteza 2 na ushee, tukaingia kulima vitunguu mkoa tunafanya kutuma hela kwenda shamba at a alijalimwa hapo tumepoteza kama 1.tukaingia wenyewe kulima tukipata mda tunaenda tukaambulia nusu asara hatukukata tamaa tukalima tena vitunguu hapo ndio nilirudi dar Kwa mguu ila sikukata tamaa nikaanza na kibiashara kingine kidogo baadae mtaji ulivyokuwa nikafungua biashara nyingine na nyingine,nilichojifunza: biashara ni usimamizi : isikate tamaa na usiangalie macho ya watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi saizi ndio nimetoboa nna hela balaa sasa sina hata mood ya kujenga sababu naona nilipo kama hazitakata vile kuna demu nimelipata linakunywa pombe balaa hili nataka nilipige chini naona kama litanifilisi. da haina mbaya mwakani ntaanza ujenzi
Sijawahi kizani kuwa unatumia avater ya kike alafu kumbe mshkaji..we jamaa una roho ngumu.

However you may not start conversation with the following recipient;Tairus
 
Kati ya mwaka 2011-2015 nilikuwa ktk standard nzuri kiasi kimaisha, biashara nzuri, usafiri binafsi na viwanja 2 mjini, pesa ya kuzungukia mjini na mafuta haikuwa shida..ninapoandika comment hii kesho sifahamu nakula nini! Nimefilisika! Hakuna hata ndugu anaenipigia simu tena maana naonekana kituko.

Wakuu tuombeane tu..kufilisika kuna maumivu ambayo si rahisi kuyaandika hapa.
 
Yupo mzee mmoja tulifahamiana kupitia kazi zangu za udalali, siku moja akaniita tukutane baa moja mjini, kufika, mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo:
Mimi: mbona umeipa barabara mgongo?
Mzee: naogopa vishawishi hahahaaa
Mimi: hahahaaaa, shikamoo
Mzee: marahaba, umewahi vizuri, agizia kinywaji
Mimi: Waiter nipatie grand malta baridi
Mzee: Unajua nakaribia kustaafu, bado miezi miwili, nimetoka semina ya maandalizi ya kustaafu dodoma, wametueleza mambo mengi, nikasema nikirudi lazima nije niongezee na za kwako.

Mimi: Umeshazishika sasa?
Mzee: bado kijana, lazima uset mipango kwanza
Mimi: mipango sio matumizi mzee wangu
Mzee: najua, ila hiyo ni kwa vijana kama nyinyi, wazee kama sisi, ukiset umeset
Mimi: ulishajenga?
Mzee: kibanda tu cha vyumba vitatu kipo mkuranga, ila siwezi kimbia jiji kisa nimestaafu, tutabanana hapahapa
Mimi: mkeo anastaafu lini na yeye?
Mzee: yeye ni mama wa nyumbani, tuna watoto watatu, wote wameshaolewa
Mimi: kwakifupi huna anaekutegemea zaidi ya mkeo?
Mzee: haswaa

Mimi: mbali na ajira yako, una chanzo kingine cha mapato?
Mzee: ni hiyo nyumba ya mkuranga, nimepangisha, nachukua kodi, sina cha zaidi
Mimi: si haba, unadhani siku ya kwanza ukiamka na kugundua ulishakabidhi ofisi na hutakiwi uende tena ofisini kwako, ungependa urudi ulale au uamke ukafanye shughuli flani?
Mzee: bado nina nguvu, ningependa kwenda kufanya shughuli za hapa na pale, hususani za usimamizi, nisingependa niwe mtendaji sanasana
Mimi: kwahiyo kama baa hii ingekuwa yako, ungependa uwe meneja na sio mhudumu?
Mzee: haswaaaa

Mimi: umewahi kufanya biashara serious na ilikuwa na mtaji wa kiasi gani?
Mzee: hapo nyuma niliwahi kufuga kuku wa kisasa, nikaacha, sikuona faida yake kivile, wateja walinikatisha tamaa, mtu unampelekea kuku anakwambia mbona mwepesi hivi, nitakupa 3500. Walipoisha nikaachana nayo hiyo baishara
Mimi: Jenga kindergarten mzee. Tafuta walimu na wahudumu, gari la shule na dereva, inalipa mjini hapa.

Mzee: safi kijana, hilo wazo murua kabisa kabisa, sasa nikupe kazi, tafuta eneo, nije nilicheki, nitafute na fundi anichoree ramani, anipe na bei ya ujenzi, nijue itanikosti bei gani
Mimi: hapana, chukua kwanza hii namba, huyu mtu na yeye ana kindegarten mjini hapa, anazo tatu, yupo vizuri sana, ngoja nimpigie nimjulishe kuwa utamtafuta akupe mwongozo, ukishaelewa somo, ndio tuje kwenye utekelezaji. Au vp?
Mzee: haswaaa. Taifa linahitaji vijana kama wewe unajua
Mimi: ni kweli mzee wangu.
Nikapiga simu kwa tajiri mwingine, nikamweka sawa, nikampa namba na yeye, nikahakikisha wamewasiliana nikiwepo na kupeana apointment ya kukutana ili mzee akale somo ya namna ya kuanzisha kindercare yake, mimi huyoo nikasepa.

Wiki, mwezi, hatimaye mwaka ukapita mzee hakunicheki tena, miaka tano baadae nakutana nae stendi moja pembezoni mwa jiji akiwa ndani ya suti ya dereva wa daladala, aliponiona alitamanigi kulia, alikuwa amechongoka flani, na kapauka. Kwakifupi alinieleza namna alivyozipata milioni zake 185 za kustaafu na namna alivyozipukusa kwa kamari na totoz, nilimhurumia sana, kisha nikamkumbusha, nilikwambia mipango sio matumizi, akasema aaah ni ujinga wangu mwenyewe, yaani sasa nimeajiriwa kama dereva hapa basi tena.
185M ileeeeeeeeeeeeeee.
 
Kati ya mwaka 2011-2015 nilikuwa ktk standard nzuri kiasi kimaisha, biashara nzuri, usafiri binafsi na viwanja 2 mjini, pesa ya kuzungukia mjini na mafuta haikuwa shida..ninapoandika comment hii kesho sifahamu nakula nini! Nimefilisika! Hakuna hata ndugu anaenipigia simu tena maana naonekana kituko. Wakuu tuombeane tu..kufilisika kuna maumivu ambayo si rahisi kuyaandika hapa.
Pole mkuu.
 
Wiki, mwezi, hatimaye mwaka ukapita mzee hakunicheki tena, miaka tano baadae nakutana nae stendi moja pembezoni mwa jiji akiwa ndani ya suti ya dereva wa daladala, aliponiona alitamanigi kulia, alikuwa amechongoka flani, na kapauka. Kwakifupi alinieleza namna alivyozipata milioni zake 185 za kustaafu na namna alivyozipukusa kwa kamari na totoz, nilimhurumia sana,
five years?,ungemtafuta kwakua ulitaka umsaidie!
 
Hapo unamaanisha nilipaswa niwe namcheki kumuuliza vipi mzee ushapokea? No way!
Yeye baada ya kupokea alipaswa akumbuke mipango yake, na kutushirikisha wadau wake.
Kitendo cha kupokea na kukaa kimya, tafsiri yake ni kwamba aliamini kichwa yake zaidi.
mipango inakuwepo mingi tuu,hela zikishakaa mkononi matumizi ndo yanatawala,kwa maswali uliokua unamuuliza ni wazi mzee alikua hajitambui,hukusima kwenye nafasi yako,yawezkana matapeli (matumizi yasio rasmi)yalimtafuta wewe mwerevu (mipango ya maendeleo)ukajifungia na alikua muwazi kwako 100%
 
Kati ya mwaka 2011-2015 nilikuwa ktk standard nzuri kiasi kimaisha, biashara nzuri, usafiri binafsi na viwanja 2 mjini, pesa ya kuzungukia mjini na mafuta haikuwa shida..ninapoandika comment hii kesho sifahamu nakula nini! Nimefilisika! Hakuna hata ndugu anaenipigia simu tena maana naonekana kituko. Wakuu tuombeane tu..kufilisika kuna maumivu ambayo si rahisi kuyaandika hapa.
Mkuu tafadhali tuandikie tujifunze. Uzur humu hakuna wa kukufahamu ila tu matukio ambayo yanaweza kukufanya ujulikane ya-skip. Uzi muria sana huu
 
Back
Top Bottom