Mafian cartel
JF-Expert Member
- Nov 19, 2021
- 3,876
- 7,118
Duh2017 hapo nikiwa bado nipo chuo na penzi limekolea kwa mpenzi wa Maisha yangu. Ananipa mtaji wa sh laki 1 na 50 nikanunua dagaa Nyasa wale ili niwe nauza Dar.
Kabla ya hiyo biashara nilishafanya biashara kama kuuza sabuni na yebo yebo nilikua napeleka Masasi na Mwanangu James Ila akaja nidhulumu nikapotezea.
Basi bwana kwenye Maisha yangu sikuwahi kuwaona dagaa nyasa hapo kabla so Mara ya kwanza nikawaona nilipoenda songea nikawapenda.. Hivyo nikamuomba mchumba anisaidie mtaji ili niwalete Dar niuze kweli nikachukua sampuli dumila 10 nikaja nao dar kisha nikaenda kwenye magenge makubwa yale kuwapelekea wengi walikataa ikabidi niwape bure kisha wauze kama watanunulika basi tufanye biashara hapo baadae bado walikataa[emoji16] Ila magenge manne yakakubali nikaacha na namba za simu basi hazikuzidi siku 3 nikapigiwa simu tukaongee.
Basi bila hiyana nikajivuta tukakubaliana niwe napeleka mzigo nawaachia wanauza ukiisha Nafuata pesa.. Aisee nakiri wazi Moja Kati ya biashara ambayo siwezi isahau ni ile ilikubali nikawa napata mshiko wa maana(kiuanafunzi) Maisha yakabadilika japo mwanafunzi kusafiri Mara kwa Mara nikichukua mzigo wa laki 2 faida laki 2 ikaja mpaka Kule nilipokua nanunua wakawa wananipa mzigo kwa Mali kauli kutoka na mzunguko mkubwa.kufipisha stori niliweza kumiliki 3M+ bank zilizotokana na biashara ile nikiwa mwanafunzi na pikipiki(bodaboda) pia geto Kali Lakini vilipotea ndani ya wiki Moja tu baada ya kutapeliwa kwa mtu niliyemuamini kupita kiasi.
Shukrani kwa brother wangu alinihifadhi kwake na kunifariji maana ningejitundika kwa mawazo ule mwaka 2018 nilipoteza kila kitu mwishowe hata shule ningepoteza. Nilikuja kuinuka tena 2019 mwishoni Ila nikaja kupigwa na kitu kizito kwa uchawi qmmake ile unapika chakula Asubuhi mchana kimechacha Maisha ni Vita.