Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Huu uzi unanisuta mm. Enzi hizo kila club unayoijua hapa mjini nilikuwa napewa hashima na mameneja. Nimemtajirisha sana mbowe pale bills. Meza yangu ilikuwa haipungui watu 5. Nikaja nikaishiwa hata mia sina, ninachohukuru nilijenga nyumba ya maana. Jamaa zangu wote wakanikimbia. Inafika hatua uko nyumni kwenye jumba zuri hata mia huna. Unaanzaje kwenda kukopa kwa mangi wkt jamii inakuona mdosi!!!! Hajahahaha maisha haya. Msoto mkali miaka 3 mfululizo. Baada ya hapo nikaanza kupata vidili vya kuinhiza 2mil kwa week. Nafanya kazi lkn hela inaishia wapi sijui

Baada ya kutafakali sana nikaona niache kunywa c/lite. Hahahaha sasa nimeona nianze kunywa chibuku. Hata niwe na milion mfukoni nanunua kopo zangu tatu kwa shs 3000 tu natinga home nameza zangu chibuka. Namshukuru wife alinivumilia kipindi kile.

Bila kufulia huwezi jua dunia ikoje
Naomba. Tuwasiliane mtaalam Dm
 
Starehe mnazipenda ila mwisho wake MBAYA. Wengi wameteketea kwa kuendekeza UMALAYA.

Ishi vizuri, kula vizuri, fanya mazoezi na umrudie Muumba wako.

___________________________________________________________

Nikiwa na miaka 24 pindi tu baada ya kuhitimu elimu yangu ya chuo kikuu niliingia mtaani, akilini na moyoni nikiwa na hari ya kuanzisha kampuni yangu. Ndoto niliyokuwa nayo tokea naingia form 3 ambapo niliacha masomo ya sayansi na kufwata kile moyo ulichoniambia KUWA MFANYABIASHARA MKUBWA.

Basi bana mwaka wa kwanza ukaisha nipo kitaa, moja haisimami mbili haikaii. Mwaka uliofwata nikiwa mtaani, nikaaanda mpango wangu biashara (ambao kwa sasa nikiusoma naona makosa mengi sana) nikaongea na wadau wawili watatu kupata mtaji wa biashara. Mungu si athumani wala hadija nikafanikiw kupata mtaji wa shillings 60,000,000.

Nikaingia kwenye biashara ya ununuzi (ulanguaji al-maarufu KANG'OMBA) korosho huko Mtwara wilaya ya Masasi. Simu wa kwanza mambo yalienda vizuri hela ilirudi. Nikaamua kwenda Uganda kufanya utafiti biashara ya mchele kule sasa mambo ndipo yaliponiendea kidogo kombo maana nilianza kupoteza taratibu pesa.

Long story short, nilikuja kupoteza pesa Million 60 shwwaaaaaa zikapotea zoootee kwenye korosho pale mzee baba (sijui huko alipo ni kiongozi wa malaika au anapigwa kama ngoma au ameenda kuwa umbwa marekani) aliposema serikali inaubavu wa kununua korosho (nyooo walijuta kilichowakuta)

Nimekaa miaka 5 kitaa sina uelekeo zaidi ya kuwa chawa kwa mwanangu wa ukwelii . Ila nilichojifunza ukianguka chukua mda kunyanyuka angalia mazingira ulipodondokea ukiwa bado chini,yatadhmini mazingira husila kisha ndio unyanyuke.

IMEKUWA MAUMIVU MAZITO ILA AKILI YA KUYASHINDA NILIJAALIWA NA MUNGU
Elezea zilipoteaje
 
Mi sister angu aaah alikua anahongwa hadi mil 50, mil 20, mil kumi......Kuna rfk ake na Ridhiwani Mzungu mmja hiv kam spoil sana sister sir tupo tunatoa mimacho tu.....eeh ukimuona sa hv sister angu yani sio yule R Dangote yani hata ukimwambia ccy twende ukanispoil anakwambia mdg angu sina ubavu huo

Mim kuhongwa pesa kubwa kabisa ni mil 5 nkahongwa mara ya pili tena mil 3 nkaongezea nkafungua biashara siku ya siku nliibiwa kila kitu dukani nlikua chizi fresh
Sister Yako aliachana naye au jamaa alifilisika
 
Very touching mi nakumbuka nilikuwa nina kifaa changu kilichokuwa kinaniingizia pesa nikakiuza baada transaction kukamilika yule bro aliyeniunganisha na mteja akawa kama ana wasiwasi kuwa zile pesa zitazifanyia biashara niliyopanga guess what zile pesa sijui zimepotelea wapi still nina regrets sababu nilishaanza kupata loyal customers kupitia kile kifaa
Kifaa gan
 
Ulifika fedha kiasi gani ukapoteza, hiyo itanipa msingi wa ushauri.

Unanikumbusha ipo siku nauguliwa na mtu kisha nampigia simu mtu ninaemuamini nikope laki 2 nimtibu mgonjwa ananijibu hana kitu ilihalu nilikuwa na uhakika anayo, nilikaa sehemu nililia sana, nikajisemea hela nilizokuwa nazo mimi wa kukopa mtu leo laki mbili nimtibie mtu ninyimwe.

Anyway yule mgonjwa akafa.
Pole sana
 
Tupe story tajiri na mtaalam

Story yake inajulikana sana mkuu ,miaka ya 2004/5 jamaa alianza kushika pesa sana hadi kuna kipindi accounts zake zilikuwa zinacheza na 300m enzi hizo 2004(Approximately 750m kwa sasa).

Kila siku mziki kwake sinza ,chawa kama wote ,asubuhi anaamshwa na mademu kwa ajili ya masaji ,msafara wake una magari si chini ya 10 halafu wote bill kwake kula kunywa kulala halafu ni daily.
 
Story yake inajulikana sana mkuu ,miaka ya 2004/5 jamaa alianza kushika pesa sana hadi kuna kipindi accounts zake zilikuwa zinacheza na 300m enzi hizo 2004(Approximately 750m kwa sasa).

Kila siku mziki kwake sinza ,chawa kama wote ,asubuhi anaamshwa na mademu kwa ajili ya masaji ,msafara wake una magari si chini ya 10 halafu wote bill kwake kula kunywa kulala halafu ni daily.
Da huyu alikuwa mwamba alipataje pesa
 
Nimesoma comments zote kiukweli zinafurahisha,kuhuzunisha na kukejelisha pia[emoji28].

Ebu mie niwape yangu japo Mungu alijua kurudisha Upinde kwangu baada ya kuuvunja wa mwanzo.

2000's (censored) nipo mwaka wa Mwisho chuo,napokea simu ya mzee "maliza uje kuna kazi nimekutafutia uje uanzie maisha".

Mwana tii!! Nadondoka job kwa cheo kikuubwa (ambacho wewe kama unge apply wangetaka 5 yrs experience,4.5+ GPA na makolokolo kibao)[emoji28],mie hiyo nimezama sijapata hata gamba chuoni litakuja mbele ya safari chezeea!!

Salary per month around 2M+ na mashehena kibaoo hapo toa madili na vishoka somewhere!!

Mchawi/wa kumlaumu ni "dereva wa bajaji" dogo junk flani hivi ..mwanzoni mwanzoni hapo natafuta pipi tu sijavuta hata kigoda cha mzungu aka Ndinga...huyo dogo ndio alikuwa ananitoa home mpaka job na kunirudisha kwa malipo ya mwezi kipande cha MIKOCHENI hapo...

Kipindi naanza job full kupiga kazi hasa mpaka mida ya saa mbili usiku hukoo ndio naachia ofisi...dogo wa bajaji hyo ratiba alikuwa anaijua...pia alijua mausha yangu yote kama nipo single...siku ya siku akanichoreshea kiramani flani "braza kwaninj uteseke kurudu home night wakat kuna pande flani unaweza kupozi na ukala matunda ya peponi"[emoji28].

Kwa kuanzia nikapelekwa "Massage Parlor" moja matata mnooo yani yani yani yani acheni tu.!!!

Kuingia watoto wa kila rangi afu wamesimama kama mwibaa hasaaa....(wazuri)..dogo akamuita matroni[emoji28][emoji28] "braza haya mambo ni mpya,mpe Menu atakayo shindwa kuisahau milele" ...matroni[emoji860]"yupo njema?!!"...dogo[emoji860]"weee mama wewee mie sitembeagi na wauza matunda[emoji28]"

Matroni[emoji860]"kama vipi na mie naingia mzigoni na vijana wangu kama 2 3 hv tusimamie show ya mgeni muheshimiwa mpya"

Dogo[emoji860]"fanya hivyo utakuja kunishukuru badae mchizi ana jiwe hasaa"

FUPISHA STORY:

Wanangu ee wa JF
Watoto wa hiyo parlor walichukua namba yangu wakaanza kuwa wananitafuta privately kila mmoja anataka kutumia opportunity kibinafsi.....

Dogo akanipeleka saloon hiyo wananyoa Mastaa tu full vidada vya instagram na bongo movie kibaoo hapo

Picha linaanza naingia tu kutupa jicho mwanangu Byser huyo hapoo mbele!! Sijacheki pembeni Nyandu tozy yule paleee naanza kuambaa ambaa Naona kiti cha kupumzikia ka chill Young dee paka rapper!!!

Nilivyotoka kunyoa pale naanza kupokea meseji kibao "braza mie msanii,najua kuimba nisimamie"
Mwingine "kaka mie ni model nahitaji support ya mavazi,location na cameraman wa maaana"!!

ITAENDELEA
But now Mungu kanipa second chance although najua laana zote za hapa bongo kupitia huyo "dogo wa bajaji"....
Una elimu gani sio Kwa ulivyoandika hivyi
 
Nimejifunza kitu hapa ili umiliki hela inatakiwa na karohoo mbaya kawepo halafu uwe mtu wa kulialia shida ili watu wasikufate kukukopa halafu kuepuka beer za round ni mbaya kuliko maelezo.
Umeshawai kusikia watu wanasema

"Tuna ndugu yetu ni MASIKINI LKN ANA ROHO MBAYA?"

always huwa wanasema

"TUNA NDUGU YETU ANA HELA LKN ANA ROHO MBAYA "

poleni sana Wanangu mliwai kupata pesa na MKAFILISIKA
 
Back
Top Bottom