Starehe mnazipenda ila mwisho wake MBAYA. Wengi wameteketea kwa kuendekeza UMALAYA.
Ishi vizuri, kula vizuri, fanya mazoezi na umrudie Muumba wako.
___________________________________________________________
Nikiwa na miaka 24 pindi tu baada ya kuhitimu elimu yangu ya chuo kikuu niliingia mtaani, akilini na moyoni nikiwa na hari ya kuanzisha kampuni yangu. Ndoto niliyokuwa nayo tokea naingia form 3 ambapo niliacha masomo ya sayansi na kufwata kile moyo ulichoniambia KUWA MFANYABIASHARA MKUBWA.
Basi bana mwaka wa kwanza ukaisha nipo kitaa, moja haisimami mbili haikaii. Mwaka uliofwata nikiwa mtaani, nikaaanda mpango wangu biashara (ambao kwa sasa nikiusoma naona makosa mengi sana) nikaongea na wadau wawili watatu kupata mtaji wa biashara. Mungu si athumani wala hadija nikafanikiw kupata mtaji wa shillings 60,000,000.
Nikaingia kwenye biashara ya ununuzi (ulanguaji al-maarufu KANG'OMBA) korosho huko Mtwara wilaya ya Masasi. Simu wa kwanza mambo yalienda vizuri hela ilirudi. Nikaamua kwenda Uganda kufanya utafiti biashara ya mchele kule sasa mambo ndipo yaliponiendea kidogo kombo maana nilianza kupoteza taratibu pesa.
Long story short, nilikuja kupoteza pesa Million 60 shwwaaaaaa zikapotea zoootee kwenye korosho pale mzee baba (sijui huko alipo ni kiongozi wa malaika au anapigwa kama ngoma au ameenda kuwa umbwa marekani) aliposema serikali inaubavu wa kununua korosho (nyooo walijuta kilichowakuta)
Nimekaa miaka 5 kitaa sina uelekeo zaidi ya kuwa chawa kwa mwanangu wa ukwelii . Ila nilichojifunza ukianguka chukua mda kunyanyuka angalia mazingira ulipodondokea ukiwa bado chini,yatadhmini mazingira husila kisha ndio unyanyuke.
IMEKUWA MAUMIVU MAZITO ILA AKILI YA KUYASHINDA NILIJAALIWA NA MUNGU