Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Duh
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Pole
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hii kali kuliko
 
Wakati nimemaliza form 6 mwaka 2015 nikapewa mchongo wa kwenda kuuza nguo maeneo ya machimbo nyamongo so nikatoka Dar nikanunua mzigo nikaenda .

Kufika Kule ikanibidi nichukue kijifremu elf 30 kwa mwezi nikalipa miezi 3 nikaweka nguo zangu muda huo home wananiuliza mbona siendi nikawadanganya napiga temporary shulen!!!

Basi nikaanza kuuza nguo but watu wakitoka kutafuta wakipata ndio wanakuja.. badae akaja jamaa mmoja tulikuwa tushazoeana akaniambia why unapigwa dolo HV twende kesho kutafuta mali!!

Basi kesho yake tukaenda ebwana wee kazi ngumu kichizi mnasubiri magari yakimwaga mzigo kutokea ndani kwenye mgodi wa mzungu tu mpo mnatafuta

Siku hiyo kama mungu alikuwa ananionyesha utajiri basi kuna jiwe nikalishika hata sijui chochote akaja jamaa yangu akaliweka kwenye mfuko kmy kmy kumbe yeye anajua.

Baada ya muda akasema tuondoke tukaenda mpaka dukani tukaingia Chemba nilikokuwa nalala akaniambia tumepata mali ananionyesha mawe yake mawili na langu moja ila yake yalikuwa madogo akasema twende kupima tukaenda lakin badae akasita akasema twende mwanza muda huu huu uku watatuibia tukapanda gari ndogo mpaka tarime then tukachukua basi kwenda mwanza mimi hata sielewi chochote ikabidi tulale maana ulikuwa usiku kesho yake tukakutana na huyo bosi wake mwanza hotel tukauza milioni 105 yale mawe

Wakaniuliza una account nikasema ndio ninayo zikaweka zile milioni 50 cash halafu nikapokea sms then nikapewa milioni 2 kwenye bahasha jamaa ananiambia mimi siondoki kama unarudi sawa we rudi.

Nikasema mimi naenda home kwanza!! Sawa tukaachana badae nikawaza niend bank nione kama mzigo upo?

Nukaenda nikajatibu kutoa nikatoa lakin 6 ikatiki na nikucheki salio milioni 49 na ushee hivi!!

Uyo home nikanunua mazaga kama ya milio 1 HV nafika home watu wananishangaa yaani wamepagawa nilivyoshusha Mazawadi .

Baada ya hapo nilichukua milioni 10 nikatoa nikampa Mama na milioni 10 nyingine baba zilizobaki nilinunua Kiwanja cha milioni 2 nyamongoro baada ya hapo ndani ya miezi 2 milioni 29 sijui ilienda wapi ila nakumbuka nililala kila hotel nzuri mwanza,serengeti, nairobi na Kampala watoto wa watu waliniita bosi mtoto.

Mshua na mather walijenga mjengo mwingine kupitia pesa yangu ila niligundua ulikuwa utoto watu wazima miaka 50+ hawachezei pesa aisee.

Pia pesa nzuri mtu kumiliki ni Ile inayoanzia from the scratch other wise ni uongo kupata milion50 hivi ujapanga cha kufanya ni wachache!

Nashukuru Mungu nilienda chuo nikamaliza now niko na angalau financial stability katika familia yangu ila nikikumbuka uwa naumia Sana pengine ningekuwa mara 3 ya sasa ila ukifilisika ndio mwanzo wa kutajirika nimegundua hivyo!!.
 
Kuanguka ndo kujifunza
 
Sorry ila nakumbuka Kuna thread kama sio hii, ulipata investor waliokuchangia mtaji ehh??,

Nimefurahi Kama unaendelea vyema mpendwa
Ndio kaka.walinichangia na namshukuru MUNGU kupitia mtaji huohuo ndo naendelea Nao[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]..
 
Ndio kaka.walinichangia na namshukuru MUNGU kupitia mtaji huohuo ndo naendelea Nao[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]..
Ubarikiwe pia, Ni Jambo jema kukuona bado unaendelea na mapambano

Samahani kwa kuweka taarifa zako za zamani wazi🙏🙏
 

[emoji23][emoji23][emoji23] kuna mengi ya kujifunza hapa
 
Wakuu nimefiliska tena, madeni madogo madogo lakini mengi.
Naomba namna ya kuongea nao nisichukuliwe hatua mpaka niwalipe taratibu.
Pia mwenye chochote kidogo asiache kunijari.

Kwa hali niliyonayo sion tatizo hata kupost namba yngu humu kwa mawasliano(0657313529)
Ndani ya post hii niliwah kueleza ni kwa vipi niliyumbishwa na maisha hadi waleo sijakaa mkao tena!
Natanguliza shukran kwa wale watakao kuwa waelewa,naomba JF iwe ni uwanja salama kwa wote hata wahitaji!
 
Mkuu yalikuwa ni madini gani hayo?
 
Ikawaje mkuu?
 
Saivi upoje mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…