Tuliowahi kupata pesa na kufilisika/kufulia, tujikumbushe hapa

Unaendeleaje na hicho kiasi...?
Dadeki bonge la mtaji.
 
Nimewahi kufanya kazi fulani nje ya Tz kwa miaka mitatu mpaka nakuja kukacha kazi nilikuwa nimesave $137,000 kitu pekee nilichofanikisha ni kujenga nyumba na kununua gari tu maana biashara niliyoanzisha ni kama ilinirudisha nyuma tu sahizi kwenye akaunti hata 10M sidhani kama itafika......anyway kitu cha muhimu nikichogundua kijana kama una nafasi ya kuwekeza fanya hivyo ingali bado hujaoa japo wapo wanaotoboa pia wakiwa kwenye ndoa
 
Ulikunja parefu sana ,vipi nyumba ya maana lakini?
 
Ulikunja parefu sana ,vipi nyumba ya maana lakini?
Mkuu nilishusha mansion ya kwenda maeneo ya kibada nikavuta na kausafiri kangu tako la nyani starehe zikanizidia mpunga umekata najipanga kuanza upya mzee but sio mbaya ilikuwa ni ujana na ninacho cha kujivunia kwamba muda wangu haukupotea bure....pesa inatafutwa tu mzee
 
Mil 300 plus mkuu aiseee..!!
 
Kama sio alex wewe sio bure....ulivyotoka Japan ulikuwa vizuri zaidi ya sana
 
Daah hela mwanaharamu aisee😂😂
 
Hii stori ya uncle unafurahisha sana aisee🤣🤣
 

[emoji302]Nimeufuatilia mjadala kwa ukaribu sana. Na kwa hakika haya ndiyo niliyojifunza.

1. Ukipata pesa bila kuwa na plan, ni ngumu sana kuitumia vyema.

2. Kuna uhusiano wa moja kwa moja Kati ya Pombe, Wanawake, Kampani mbovu na Starehe zingine katika kuua mafanikio ya kifedha. Kwa upande wa Wanawake kuna kitu kinaitwa "SEXUAL TRANSMITTED DEMONS" ambazo huweza kuharibu mipango ya mafanikio kwa asilimia kubwa.

3. Elimu ya kifedha ni muhimu sana Kwa kila mtu bila kujali level ya elimu,jinsia ama Umri.

3. Budget inapoheshimiwa na kufuatwa huweza kuzuia mianya ya upotevu wa pesa zisizo kwenye matumizi.

4. Unapoipata pesa jitahidi uiamrishe na siyo kukuamrisha.


5. Tunajifunza kutokana na makosa, usipoanguka huwezi kujifunza.

6. Kuna uwezekekano mkubwa wa mtu aliyefirisika kurudi katika hali yake ya zamani au hata zaidi ya Hapo, kwani nidhamu, kujiamini, maarifa, uthubutu na ukomavu huwa ni mkubwa sana.

7. Ni vyema kumshirikisha MUNGU katika mipango yetu ya kifedha ili atupe uwezo wa kuitumia vyema kwa manufaa bora zaidi.

[emoji302]Na mwisho niwatakie mafanikio mema wale wote walioamua kuanza upya, kwani uwezo wa kuinuka tena Upo. Lakini kwa ambao hawajawahi kufirisika wasiwaone waliofirisika kuwa ni wazembe ama hawana nidhamu. La hasha. Haya maisha ni fumbo. Hivyo badala ya kuwadharau kaa chini UJIFUNZE ili usije ukarudia makosa.

Asanteni.[emoji1666][emoji120]
 
Nimesoma page zote 88 za huu uzi,na sababu ya kunifanya nisome uzi huu ni kwa sababu na mimi ni katika wana wapotevu.

Kufulia ama kufilisika ni jambo hatari sana na kama ni mwepesi unaweza kujiua.

katika upotevu wangu na huu uzi nimejifunza mambo makuu yafuatayo.

1.ukiwa huna hela njaa huja mara kwa mara.,ukiwa una hela ya kutosha kula unajilazimisha unajikuta pesa ndio inakufanya uwe full all the time.

2. Ili ujue kama msoto uliopitia umekufunza kitu basi kipimo kiwe baada ya kuzipata tena pesa ndio utaona kama umejifunza au laa.
Kila mtu life likimpiga atajidai amejifunza ila true measure ni pale utakapopata tena fursa ndio utaona.

3.Tatizo sio kuwa na uthubutu wa kula na mipango kabla ya pesa bali tatizo ni kufuata mipango uliyoipanga,wengi tukifulia tunapanga vizuri ila tukizipata hatufuati mipango,sio tatizo ni kufuata ama kutekeleza ulichopanga.

Kila mtu anajua mambo ya msingi ya kufanya pesa inapopatikana na anajua mambo gani asifanye ili pesa ilipotee,TATIZO JE UTHUBUTU WA KUFUATA NA KUFANYA ZURI NA KUACHA BAYA UPO ?

4.ukifulia kuna possibility kubwa sana kya kuinuuka zaidi ya ulivyokuwa kabla endapo tu UTAJUA WAPI ULIFELI MWANZO NA UKAREKEBISHA SABABU HIZO ZA KUFELI MWANZO.

5.kitu kikuba unaweza kujivunia ukishafilisika ni AFYA YA AKILI kwani kama haupo njema unawez kujiua na kama upo vizuri unaweza ukalidogosha tatizo lako na kuliona kama funzo na kumove on.

6.Mara nyingi sana kujifunza kwa kuexperience mwenyewe ndiko kunaufundisha mwili vizuri kuliko kujifunza kwa kusimuliwa,hakuna mtu hajawahi kusikia kwamba starehe zinamaliza pesa,ila cha ajabu tukipata pes atunarudi huko hata kama tunajua yaani alimradi tujifunze kwa experience wenyewe.
 
Mwana mpotevu mwingine nipo hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…