[emoji302]Nimeufuatilia mjadala kwa ukaribu sana. Na kwa hakika haya ndiyo niliyojifunza.
1. Ukipata pesa bila kuwa na plan, ni ngumu sana kuitumia vyema.
2. Kuna uhusiano wa moja kwa moja Kati ya Pombe, Wanawake, Kampani mbovu na Starehe zingine katika kuua mafanikio ya kifedha. Kwa upande wa Wanawake kuna kitu kinaitwa "SEXUAL TRANSMITTED DEMONS" ambazo huweza kuharibu mipango ya mafanikio kwa asilimia kubwa.
3. Elimu ya kifedha ni muhimu sana Kwa kila mtu bila kujali level ya elimu,jinsia ama Umri.
3. Budget inapoheshimiwa na kufuatwa huweza kuzuia mianya ya upotevu wa pesa zisizo kwenye matumizi.
4. Unapoipata pesa jitahidi uiamrishe na siyo kukuamrisha.
5. Tunajifunza kutokana na makosa, usipoanguka huwezi kujifunza.
6. Kuna uwezekekano mkubwa wa mtu aliyefirisika kurudi katika hali yake ya zamani au hata zaidi ya Hapo, kwani nidhamu, kujiamini, maarifa, uthubutu na ukomavu huwa ni mkubwa sana.
7. Ni vyema kumshirikisha MUNGU katika mipango yetu ya kifedha ili atupe uwezo wa kuitumia vyema kwa manufaa bora zaidi.
[emoji302]Na mwisho niwatakie mafanikio mema wale wote walioamua kuanza upya, kwani uwezo wa kuinuka tena Upo. Lakini kwa ambao hawajawahi kufirisika wasiwaone waliofirisika kuwa ni wazembe ama hawana nidhamu. La hasha. Haya maisha ni fumbo. Hivyo badala ya kuwadharau kaa chini UJIFUNZE ili usije ukarudia makosa.
Asanteni.[emoji1666][emoji120]